Hivi Magufuli angekuwa ni Rais wa mojawapo ya Nchi Wahisani, angetoa misaada kwa nchi zinazoendelea?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,985
144,312
Ukweli ni kwamba, nchi zetu hizi zinazoendelea, hasa hizi za Afrika, hazipigi hatua kubwa kimaendeleo na kuondokana na umasikini kutokana na mambo kama rushwa, ubinafsi wa viongozi, kukosekana kwa utawala bora, demokrasia,katiba mbovu,vipaumbele vibovu, n.k. huku chanzo kikuu kikiwa ni nchi nyingi za kiafrika kuwa na watawala wabovu.

Ushahidi wa hili ni uwepo wa baadhi ya nchi za Asia zilizopata uhuru katika miaka ambayo nchi nyingi za kiafrika nazo zilikuwa zinapata uhuru ila leo ziko mbali sana kimaendeleo mfano, Malaysia, Singapore,n.k.

Sasa najiuliza, kama Magufuli angekuwa ni Rais katika mojawapo ya Nchi Wahisani, angekubali kuendelea kutoa misaada kwa hizi nchi masikini au angezisimanga kwa maneno makali kuwa zinaendekeza umasikini na hivyo nchi yake isingetoa misaada?

Nawaza sana.
 
Nafikiri aliwapa msaada Msumbiji walipopata majanga, tunawapa msaada DRC kwa kuwalinda, South Sudan kuwapa wataalamu wetu, Comorro to keep law and order intact.

Tanzania pamoja na kasoro zake, uwezo wake, ni nchi inayojari jirani, kuliko nchi nyingi duniani.
Hiyo misaada ni kuwa mingi uliyotaja ni kwamba tunalipwa
 
Kule kunaweza kuwa Na nchi zaidi ya 20 mpaka kina Niger. UN Ndio wanatoa fedha.
Sasa point ni ipi? Tanzania imekuwa ikisaidia nchi zingine kwa hali na mali tangu ipate uhuru.

Na itaendelea kufanya hivyo aijalishi Rais ni nani. Inategemewa. Expected to step foward, is trusted, have moral authority.

UN labda wangeamua wangeichagua Rwanda, Burundi, Sudan, Congo Brazaville etc.
 
Nafikiri aliwapa msaada Msumbiji walipopata majanga, tunawapa msaada DRC kwa kuwalinda, South Sudan kuwapa wataalamu wetu, Comorro to keep law and order intact.

Tanzania pamoja na kasoro zake, uwezo wake, ni nchi inayojari jirani, kuliko nchi nyingi duniani.
Nashangaa hapa wanaosem.asingeweza kam.hayo kafanya hiv wabong.tunann jaman
 
Back
Top Bottom