Hivi Magufuli angekuwa ni Rais wa mojawapo ya Nchi Wahisani, angetoa misaada kwa nchi zinazoendelea?

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,164
2,000
Hijui serikali yako inapanga Bajeti inayotegemea hela za wahisani miaka 60 baada ya uhuru?
Kwani usichoelewa ni nini? Hivi we kwa akili yako mzungu bepari akupe hela ya bure (msaada) kwani we ni mwana wao? Iko hivi kwa kila sh moja wanayokupa wao wanapata sh mbili na zaidi. Juzi Bill Gates kasema use billions to save trillions! Kwa ufupi ni kwamba hao wazungu hata watoto wao waliotoka viunoni mwao hawawapi pesa ya bure wakishafikia umri fulani. Wakupe wewe kwani we ni nani?

Huo unaouita msaada si msaada kama unavyofikiria. Kwa uchumi waliofikia (ukizingatia pia sehemu ya uchumi wao inategemea nchi zinazoitwa maskini za Afrika) ni faida kwao kurejesha kiasi katika nchi zinakotoka malighafi za uchumi wao.
 
ruaharuaha

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
2,230
2,000
Unahitaji vitu vitatu tu kupata maendeleo kwa kasi: mifumo ya Reli, Umeme wa kutosha na kilimo bora.

Magufuli akijaribu kufanya hayo nyie ndo wakwanza kupinga. Nyie pamoja na vizazi vyenu mtamshukuru JPM kwa reli ya SGR na Nyerere hydropower station.
Na barabara, hospitali, shule (elimu), kuzuia Rushwa, nidhamu serikalini, kuondoa ukiritimba. Huduma chap chap.

Kuna vitu bado inabidi viangaliwe hasa TRA, bandari, JNIA. Tutumie wachumi kujua how we get maximum taxes while helping our people.

Inawezekana kufanya vyote kwa ufanisi mkubwa na kuwaongezea watu vipato. Ndani ya muda mchache sana na serikali kukusanya mapato zaidi.
 
Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,996
2,000
Kwanini tusizipokee sisi ambapo wakiwa wakimbizi ndio tutakaoathirika zaidi?

Unajua wangapi wamekufa, maisha ya vijana cut short.

Maisha ya wanajeshi, vijana wetu unaweza kuyawekea thamani gani?

Tunajitolea maisha yetu, ya vijana wetu kuwalinda.
Unajua maana ya kujitolea lakini?
Yaani unajitolea alafu unalipwa mamilioni ya dola?
Kwani wakimbizi wakija TZ unadhani nchi inakua inatoa ardhi bure nk..Jielimishe zaidi.
 
Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,996
2,000
Kwani usichoelewa ni nini? Hivi we kwa akili yako mzungu bepari akupe hela ya bure (msaada) kwani we ni mwana wao? Iko hivi kwa kila sh moja wanayokupa wao wanapata sh mbili na zaidi. Juzi Bill Gates kasema use billions to save trillions! Kwa ufupi ni kwamba hao wazungu hata watoto wao waliotoka viunoni mwao hawawapi pesa ya bure wakishafikia umri fulani. Wakupe wewe kwani we ni nani?

Huo unaouita msaada si msaada kama unavyofikiria. Kwa uchumi waliofikia (ukizingatia pia sehemu ya uchumi wao inategemea nchi zinazoitwa maskini za Afrika) ni faida kwao kurejesha kiasi katika nchi zinakotoka malighafi za uchumi wao.
Basi mpe wewe huyo mzungu bepari pesa bila masharti
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom