Hivi maendeleo ya nchi siku hizi hayatakiwi kusikika hadharani?

jakomala

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
514
367
Juzi kati hapa waziri wa mawasiliano na uchukuzi mhandisi ISSACK KAMWELE alitamka mbele ya media kuwa mwandishi wa habari akamatwe kwa kutoa taarifa ya ndege yetu kuwasili nchini ,Na akadhibisha kuwa wa kutoa habari ni ATCL wala syo mtu mwingine.
Jana nilipofika nyumbani nikawasha tv yangu,nikasema niangalie igizo ITV kwa sababu ni wikendi cha kusangaza nikakuta ndege yetu aina ya BOIENG kutoka kampuni ya marekani inapokelewa uwanja wa JULIUS NYERERE TERMINAL3 na Baba yetu mpendwa pamoja na wakuu wa nchi.

Ilibidi nijiulize mbona kimyakmya syo kama zamani tulikuwa tunatangaziwa tarehe ya ndege kufika hasa kwa wakazi wa Daresalaam Baba Makonda alikuwa akitamka"woteee tufike julius nyerere kupokea ndege yetu"
Sasa najiuliza mbona tunaanza kufichana maendeleo ya vitu kwa ajili ya nchi yetu pendwa?

Kama nitakuwa sina kumbukumbu basi wadau mnikumbushe....
Screenshot_20191027-134835_Flight%20Radar%20%26%20Tracker.jpeg
 

Attachments

  • IMG-20191025-WA0051.jpeg
    IMG-20191025-WA0051.jpeg
    39.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom