Hivi Madini yalitoka wapi?

PLATO MAGELE

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
203
54
Hivi jamani madini kama dhahabu, almasi, shaba, chuma n.k. yalipatikanaje hapa duniani?(i.e. How were/are they formed?). Maana Nchi kama Tanzania ina dhahabu, almasi, uranium na madini mengine mengi tu, ndio tuseme Mungu ametupendelea au kuna namna fulani ambayo haya madini yanapatikana.
 
Madini ni molecules or elements ambazo zimebaki chini ya ardhi kwa miaka kadhaa kutokana na Geological history. Hakuna cha Mungu anapendelea wala nini. Vitu kama almasi ni carbon molecule ambayo ikiwa under intense pressure and temperature inatengeneza almasi. Almasi haina tofauti na graphite au mkaa bali ni formation yake ni tofauti. Fikiria kama mchele na mpunga. Dhahabu ni rahisi kupatikana kwa sababu gold element sio reactive kama metali nyingi.

Hizi elements zinatokana wapi? Nuclear fusion. Historia ya ulimwengu ilianza kama hydrogen. Hydrogen ina fuse kutengeneza helium. Hivo hivo helium ina-fuse kutengeneza elements higher in the periodic table. Nyota ikifa, huwa inalipuka na kurusha elements na baadhi ya hizo elements zina-angukia kwenye new stars kutokana na gravity.

Hii nimerahisisha ila ni somo refu ambalo linataka had degree. Kama unahitaji somo zaidi nishtue!
 
Kumbe yametokana na certain forces, watu wengi wanaamini ni Mungu aliyaumba. Kumbe nilichojifunza hakuna cha Mungu Katika formation zake. Asante sana ndugu. Yawezekana kumbe Mungu amehusika na umbaji wa viumbe hai tu.
 
Mkuu pamoja na maelezo ya kijiolojia uliyotoa mbona upatikanaji wake ni wanaeneo fulani tu, i.e they are not equally distributed. Why? Kwa mfano, kuna baadhi ya nchi zinamadini mengi sana, zingine hakuna au upatikanaji wake ni kidogo.
 
anzia kwenye climatic conditions utapata majibu.....climate inavary from one place to another [hapa pana sababu zake pia ]...
Pia rejea sababu za kufanyika kwa miamba
 
Wakuu, nimesoma the way how the universe evolved( kuanzia kwenye Big bang) na kuona jinsi gani heavy elements zimeformika kutokana na light elements. Pia nimesoma jinsi viumbe hai walivyopatikana kutokana na simple molecules kutoka kwenye planetary remnants. Yote haya sijaona popote pale Mungu amehusika, kwa mantiki hiyo naweza kusema kuna utata kuhusu uwepo wa Mungu. Maana hata location ya mbigu (heaven) kwenye universe haipo. Au wakuu mnasemaje?
 
anzia kwenye climatic conditions utapata majibu.....climate inavary from one place to another [hapa pana sababu zake pia ]...
Pia rejea sababu za kufanyika kwa miamba

Asante sana, nimefanya kulingana na maelekezo uliyoyatoa; nimepata mwanga kidogo.
 
Nickia harufu ya shetani ime tanda leo humu ndani!

Hiyo harufu ikoje? Je, waweza kukithibitisha unachokiamini wewe? Unauhakika gani na huyo Mungu waliomleta wazungu wakati wa ukoloni ndiye Mungu wa kweli? Najua umeaminishwa bila proof yoyote. Na huyo Mungu unayeamini umeletewa na wazungu wakati wa ukoloni ili waweze kuchuma mali za waafrika kiulaini. Maana wamishenari walikuwa agent wa ukoloni waliweza kuhubiri kutokuwachukia(kuwa na upendo kwa kila mtu) ili wachukue malighafi bila kusumbuliwa na mtu, mkikaririshwa kuwa "sisi sote ni ndugu katika Bwana" kumbe wizi mtupu. Kila kitu ni cha kusadikika tu, no evidence, no what...
 
Kwa nini unaulizia madini??
Kwa nini sio udongo...au mawe...!
 
Kwa nini unaulizia madini??
Kwa nini sio udongo...au mawe...!

Kinachomfanya mtu asome Pharmacy ni nini badala ya kusoma Chemistry na Biology? I.e kwa nini asome applied science( pharmacy) badala ya kusoma natural science (Chemistry and Biology)?
 
Katika vitu vinavyonifanya niwe na aibu ya kuwa mbongo ni faraja yetu katika ujinga. Mtu anafurahia kuambiwa kuwa Mungu ndio sababu ya kila kitu. Kuanzia magonjwa mpaka madini. Kasome Geography kidogo na biology. Kuna vitu ambavyo hata mlei wa kawaida ataelewa tu. Kafungueni vitabu wakubwa. Vitakufikisheni mbali.
 
kiongozi usicheke jamaa ameshitukia u-freemason katika hili!!

Jamani badala ya kusema u-freemason, jaribu hata kidogo kuwa na ufahamu wa kishule. Maana inavyoonekana hujawahi hata kusoma kitu kinachoitwa Geography au Biology kwa O-level. Angalau ungekuwa hata na kaufahamu kadogo katika mambo haya. Kweli inasikitisha sana maana inaonesha kuwa baadhi ya watu hawajapata fursa ya kwenda shule. Nasikitika sana kwa kucheka na kusema u-freemason. Kweli safari bado ndefu. Ama kweli Faith is very dangerous.
 
o-level ndo nini!mm siamini katika hiyo sayansi ya dunia,naamini katika hiyo uliyoiita faith!
 
o-level ndo nini!mm siamini katika hiyo sayansi ya dunia,naamini katika hiyo uliyoiita faith!

Sayansi sio imani, it has facts proved by various experiments. Kwa hiyo chochote kinachohusu sayansi kimethibitishwa sio ujanja ujanja tu. How can you believe something which can not be proved? Hata hivyo hicho unachokiamini ilikuwa ni ujanja wa wazungu kufanikisha wizi wao wa malighafi ili waendeleze viwanda vyao na kufanya afrika kuwa soko la bidhaa zao. Historia hiyo hata shule ya Msingi inafundishwa, walianza explorers(wapelelezi), wakafuatia missionaries(wamishenari) baadaye traders. Kwa hiyo kundi la pili ndilo lililoacha imani unayoiamini ambayo malengo yake kwa kipindi hicho ni tofauti na sasa. Kwa hiyo Mungu aliyekuwa anatunyonya na kutupora vitu vetu kipindi hicho kupitia wamishenari kwa sasa ameshabadilika! Jamani, tafakari.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom