Hivi madini ili yatoke huko ardhini lazima yachimbuliwe na wawekezaji toka nje?

Stream line

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
393
239
Ukisikiliza vilio vya watanzania wengi ambo ni wachimbaji wadogo vinafanana. Wanasema tulikuwa tukilima au tukitafuta kuni msituni tukagundua madini na tukaanza kuyachimbam baadaye DED anaingiloa kati anawekwa mwekezaji na wao wanafukuzwa! Pengine ma DED wanakwenda mbali na kudai mwekezaji anatafiti.

Swali langu ni, je, madini yanapoanza kuchimbwa huwa hayatoki hadi aje mwekezaji?
Sisi ni masikini katika kulima tukaokota madini. Kwanini Ma-DED wasiwaunganishe hao wagunduzi wa kwetu waliokuwa wakulima waliookota bahati wakawasaidia kuvuna huo utajiri? Mali niokote mimi lakini anapewa jirani kwa kisingizio kisichoeleweka.

USHAURI; Sasa tuseme basi.

Kwa wawekezaji hawa wafilisi pia Ma -DED wenye madini waungane na kuanzisha kiwanda cha kuchakata madini. Ili huyu aliyeokota utajiri shambani mwake aagane na maisha mabovu. Naona uchungu sana. mf. Rais kasema hawa wachimbaji wa shinyanga wasiondolewe, Leo mkuu wa mkoa/wilaya/DED shinyanga anawaondoa bila sababu inayoeleweka. Hiyo ni kuwakosanisha wananchi na serikali yao.
 
Ukisikiliza vilio vya watanzania wengi ambo ni wachimbaji wadogo vinafanana. Wanasema tulikuwa tukilima au tukitafuta kuni msituni tukagundua madini na tukaanza kuyachimbam Baadaye DED anaingiloa kati anawekwa mwekezaji na wao wanafukuzwa!! Pengine ma DED wanakwenda mbali na kudai mwekezaji anatafiti.
Swali langu ni, je, madini yanapoanza kuchimbwa huwa hayatoki hadi aje mwekezaji?
Sisi ni masikini. ktk kulima tukaokota madini. Kwa nini Ma-DED wasiwaunganishe hao wagunduzi wa kwetu. waliokuwa wakulima waliookota bahati. wakawasaidia kuvuna huo utajiri? Mali niokote mm lakini anapewa jirani kwa kisingizio kisichoeleweka!
USHAURI; Sasa tuseme basi
kwa wawekezaji hawa wafilisi. pia Ma ded wenye madini waungane na kuanzisha kiwanda cha kuchakata madini. Ili huyu aliyeokota utajiri shambani mwake aagane na maisha mabovu. Naona uchungu sana. mf. Rais kasema hawa wachimbaji wa shinyanga wasiondolewe, Leo mkuu wa mkoa/wilaya/DeD shinyanga anawaondoa bila sababu inayoeleweka. Hiyo ni kuwakosanisha wananchi na serikali yao.


Utachimba kwa vidole?
 
Sio lazima, ila inabidi ujiukize kwanza kuhusu kiwango cha teknolojia nchini kinakidhi mahitaji? Pia angalia wawekezaji wa ndani wana mitaji ya kutosha kuendessha shughuli za uchimbaji wa madini
 
Unadhani ni mihogo hiyo??! Wewe nenda sehemu za migodi uone kazi inavyofanyika mitambo hiyo siyo ya nchi hii!! Kuchimba visima vya maji tu vimetushinda sembuse madini!
 
Sio lazima, ila inabidi ujiukize kwanza kuhusu kiwango cha teknolojia nchini kinakidhi mahitaji? Pia angalia wawekezaji wa ndani wana mitaji ya kutosha kuendessha shughuli za uchimbaji wa madini
Tanzania kama nchi imepeleka nje au kusomesha wataalam wangapi wa kuchimba madini ili tuwe na uhakika wa kujitegemea kuchimba wenyewe huko mbele
 
Sio lazima, ila inabidi ujiukize kwanza kuhusu kiwango cha teknolojia nchini kinakidhi mahitaji? Pia angalia wawekezaji wa ndani wana mitaji ya kutosha kuendessha shughuli za uchimbaji wa madini
kama anataka uchimbaji mkubwa atafute kama trillioni moja na ushee, hapo bado fweza za uendeshajii.
 
Tatizo sio wataalamu wa kuchimba madini,tatizo kubwa ni capital ndugu.kuchimba madini sio kuchimba mihogo inahitaji fedha nyingi na miundo mbinu ya kutosha.
 
Back
Top Bottom