Hivi Maandamano Yanaogopwa Hivi? Ningekuwa Mimi, Ningewaruhusu na Ulinzi Ningewapa na Kuwakaribisha Ikulu!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,443
113,452
Wanabodi,

Nimeogopeshwa na lugha kali za kuyapinga maandamano ya huyu dada Mange Kimambi!, kumbe Mange anaogopwa hivi?!. Yaani anahamasisha maandamano ya mtandaoni tuu kuwa watu wataandamana kwenda Ikulu kupindua nchi!, halafu watu kweli wa Ikulu yetu ya kweli, wanatishika!, hadi kuyapiga marufuku kwa maneno mazito, makubwa makali kwa lugha kali kiasi hiki?!.

Kiukweli ningekuwa ni mimi, kwa jinsi rais Magufuli anavyokubalika, ningeyaruhusu hayo maandamano, tena ningewapatia ulinzi!, kisha waje Ikulu kupitia geti la pale, na rais mwenyewe ayapokee, ili kupima kiwango cha utimamu wa Watanzania, maana ni Watanzania wasio na akili timamu ndio wanaweza kukubali kuandamana kwenda kumtoa rais Magufuli Ikulu!. Hata yale maandamano ya UKUTA yaliyokuwa ni maandamano ya nchi nzima, na mikutano ya non stop ya nchi nzima, ningekuwa mimi, ningeruhusu tuu, ili kuyatumia maandamano hayo kama kupimo cha kiwango cha joblessness yetu kwa kupima ni watu wangapi wasio na kazi, wenye muda wa kuandamana maandamano ya non stop siku zote na kuhudhuria mikutano nchi nzima kutwa kucha!.

Kwa maoni yangu, dada Mange, amepewa promo na undue attention kubwa ya bure isiyo na sababu, kwa Watanzania ninaowafahamu mimi, kuna Watanzania gani wa kuandamana kwenda Ikulu kupindua nchi?!. Hivi kweli hayo maandamano yalikuwa ni tishio hivi kiasi cha kutolewa kwa kauli kali hivi za kuyapinga?. Tena kauli inatoka kwa rais mwenyewe?!. Jamani nyie wasaidizi wa rais wetu, timizeni wajibu wenu wa kumshauri rais wetu vitu vya kusema na vitu vya kupuuzia!. Japo Mbunge Mhe. Livingstone Lusinde ni darasa la saba tuu, kuna vitu very sensible huwa anaongea, mfano Mange akiibukuwa na hoja kuwa jamaa hajafanyiwa sunna, jee utaitoa hadharani kuonyeshea umefanyiwa?.

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .

Mhe. Rais Magufuli, waite wapinzani uwakaribishe Ikulu, wapige juice na vitavunwa kama alivyokuwa anafanya mtangulizi wako JK, ila sio kuwaomba wajitoe vyama vyao na kujiunga CCM kama ulivyomuita Lowassa, bali zungumza nao, zisikilize hoja zao, waache watoe dukuduku zao, waahidi utazishughulikia.

Lengo la hatua hii sio kuonyeshana nani zaidi, mtu ambaye ni zaidi, siku zote ni zaidi, hana haja ya kuzungumza kwa lugha za ukali sana kuonyesha yeye ni zaidi, hata akizungumza kwa upole tuu kwa kutumia pasuasive language kama JK, bado atabaki ni Zaidi, uzoefu unaonyesha watu wakiishaalikwa Ikulu. wakanywa juice, chai na vitafunwa, siku zote wakitoka huwa wanatoka huku wana smile, hata Lowassa mwenyewe, tangu siku ile umemkaribisha Ikulu, he is not the same Lowassa, huwezi kuamini ni Lowassa huyu aliyesema maneno haya,
Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!.
ndiye Lowassa huyu huyu aliyeitwa Ikulu na kutoka ana smile!.

Mhe. Rais, ruhusu mikutano ya siasa, ipo kwa mujibu wa katiba, ruhusu maandamano, achia freedom of expression, waite wapinzania, wakaribishe ikulu waje wanywe juice za Ikulu wakiisha kunywa juice za Ikulu na vitafunwa, wata easy the tension, wataondoka wamefurahi with a big smile na ni wao wenyewe wata call off maandamano yao. Kama Uhuru na Odinga Wameweza, sisi tunashindwa nini?.

Paskali
 
wanaweweseka maandamano yenyewe bado kama wiki saba yaanze ,Ila mpaka AMRI JESHI anaogopa..... Mimi nilikuwa naona kama commedy fulani watu wanajifurahisha mitandaoni hivi ,ila naona wakuu wanapanic...
Je kwanini WANAOGOPA?
Kwanini wasimuonye mratibu wa maandamano amabaye anajulikana ni MANGE?
Hebu tusubiri hiyo 26/04 kama kuna watu watadai Tanganyika yao na Zanzibar YAO.
 
Wanabodi,

Nimeogopeshwa na lugha kali za kuyapinga maandamano ya huyu dada!, kumbe anaogopwa hivi?. Yaani anahamasisha maandamano ya mtandaoni kupindua nchi, halafu watu wanatishika na kuyapiga marufuku kwa lugha kali kabisa!.

Kiukweli ningekuwa ni mimi, kwa jinsi rais Magufuli anavyokubalika, ningeyaruhusu hayo maandamano, tena ningewapatia ulinzi!. Hata yale maandamano ya UKUTA yaliyokuwa ni maandamano ya nchi nzima, na mikutano ya non stop ya nchi nzima, ningekuwa mimi, ningeruhusu tuu, ili kuyatumia maandamano hayo kupima kiwango cha joblessness yetu kwa kupima ni ni watu wangapi wasio na kazi, wenye muda wa kuandamana maandamano y non stop na kuhudhuria mikutano nchi nzima kutwa kuccha!.

Kwa maoni yangu, dada amepewa promo na undue attention kubwa ya bure isiyo na sababu, kwa Watanzania ninaowafahamu mimi, kuna Watanzania gani wa kuandamana kupindua nchi?!. Hivi kweli hayo maandamano yalikuwa ni tishio hivi kiasi cha kutolewa kwa kauli kali hivi za kuyapinga?.

Mhe. Rais Magufuli, waite wapinzani uwakaribishe Ikulu, wapige juice na vitavunwa kama alivyokuwa anafanya mtangulizi wako JK, ila sio kuwaomba wajitoe vyama vyao na kujiunga CCM kama ulivyomuita Lowassa, bali zungumza nao, zisikilize hoja zao, waache watoe dukuduku zao, waahidi utazishughulikia.

Lengo la hatua hii sio kuonyeshana nani Zaidi, mtu ambaye ni Zaidi, siku zote ni Zaidi, hana haja ya kuzungumza kwa lugha za ukali sana kuonyesha yeye ni Zaidi, hata akizungumza kwa upole tuu kwa kutumia pasuasive language kama JK, bado atabaki ni Zaidi, uzoefu unaonyesha watu wakiishaalikwa Ikulu. wakanywa juice, chai na vitafunwa, siku zote wakitoka huwa wanatoka huku wana smile, hata Lowassa mwenyewe, tangu siku ile umemkaribisha Ikulu, he is not the same Lowassa, huwezi kuamini ni Lowassa huyu aliyesema maneno haya,
Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!.
ndiye Lowassa huyu huyu aliyeitwa Ikulu na kutoka ana smile!.

Wakaribishe wapinzani juice ya Ikulu wakiisha kunywa juice ya Ikulu na vitafunwa, wata easy the tension, wataondoka with big smile na ni wao wenyewe wata call off maandamano yao. Kama Uhuru na Odinga Wameweza, sisi tunashindwa nini?.

Paskali
Tatizo ni njia iliyomweka mtu. Ukishajua waliowengi hawako na wewe uwezi kuyakubali Paskal
 
Hayo bila shaka ni maandamano ya kiburi na wala sio ya wananchi bali ya wachache wenye nia mbaya, wanatumia kivuli cha jina la wananchi, maneno yanayotumika kuhusu kusudio la hayo maandamano ni wazi sio watu wema bali wana ajenda yao.

SASA DAWA YA KIBURI NI JEURI. Waandamane waone, tuko bize tunafanya watanzania.
 
Hayo bila shaka ni maandamano ya kiburi na wala sio ya wananchi bali ya wachache wenye nia mbaya, maneno yanayotumika kuhusu kusudio la hayo maandamano ni wazi sio watu wema bali wana ajenda yao.

SASA DAWA YA KIBURI NI JEURI. Waandamane waone, tuko bize tunafanya watanzania.
Aibu sana Mwanaume uliyechaguliwa na watanzania milioni 8 kubishana na mwanamke aliye mbali huko!

Kwa analysis ya kawaida hapa hata yasipofanyika bado Mange anaonekana amefaulu kwa kiasi flani
 
IMG_20180307_17862.jpg
 
Aibu sana Mwanaume uliyechaguliwa na watanzania milioni 8 kubishana na mwanamke aliye mbali huko!

Kwa analysis ya kawaida hapa hata yasipofanyika bado Mange anaonekana amefaulu kwa kiasi flani
Kumbe mnafahau alipata kura milioni 8, sasa povu huwa lawatoka la nini?

Aandamane mtu aone!
Mwanaume keshasema, wewe na Mange wako mtajijua wenyewe.
 
Back
Top Bottom