Elections 2010 Hivi maamuzi yetu ya kuwachagua viongozi yatachakachuliwa hadi lini?

Mwanapori

New Member
May 14, 2008
4
0
Inasikitisha sana kuona kila unapofanyika uchaguzi mkuu wa kuwapata viongozi, maamuzi ya wananchi juu ya kuwachagua viongozi wao kuanzia Madiwani, Wabunge hadi Rais huwa hayaheshimiwi.

Unakuta nchi inatumia rasilimali nyingi sana za wananchi(walipa kodi) katika kuandaa uchaguzi, ambapo fedha hizi zingeweza kutumika kutoa huduma mbali mbali kwa wananchi.

Wananchi wanapofanya maamuzi ya nani wanamtaka awe kiongozi wao, Tume ya Uchaguzi inahujumu (inachakachuwa) maamuzi ya wapiga kura!

Hivi hii Tume ya Uchaguzi ipo kwa maslahi ya nani katika nchi hii?

Maamuzi ya wananchi ya kuwachagua viongozi wao yataendelea kuhujumiwa hadi lini?

Je tuendelee kukaa kimya tu na kubaki kuitazama Tume ya Uchaguzi ikiamua itakavyo?

Wanajamii wenzagu naomba tutafakari na kutafuta suluhisho la haya yote.
 
Back
Top Bottom