Hivi maamuzi ya Bunge kuhusu CAG hayawezi kuhojiwa mahakamani?

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Wanasheria na wanaharakati tusaidieni katika hili, hivi maamuzi ya Bunge juu ya CAG hayawezi kuhojiwa mahakamani?

Yawezekana wapo wanaosema mihimili haingiliani lakini lazima tutambue hakuna muhimili ambao "unavikwa uungu" kwa mantiki ya kwamba kile wanachokiamua basi ndio final and binding.

Kwa bahati mbaya mimi sio mwanasheria hivyo siwezi kujua kifungu kipi kinatoa fursa lakini naamini mihimili inasimamiana na kutoa fursa ya maamuzi ya chombo kimoja kutazamwa kwa mapana na chombo kingine hasa ikichukulia mgogoro wa CAG na Wabunge ulivyokaa ni vigumu kwa upande mmoja unohusika kutika mgogoro huu kutoa tafsiri sahihi ya upange kinzani katika mgogoro huu.

Kila mmoja wao atasimamia tafsiri inayobeba maana anayoisimamia.

Mgogoro huu ulianza ukiwa ni jambo dogo lakini sasa limekua na kuonekana kuzidi kukua na kwa ushauri wangu ni wakati muafaka wa kuomba tafsiri ya mahakama kwenye jambo hili.

Ninapendekeza wanaharakati kama kituo cha sheria na haki za binadamu kulipeleka jambo hili mahakamani.
 
What is SWOT and why kila organization inafanya SWOT analysis hasa wakati wakuandaa Strategic Plans? Je yaweza kuwa organizations nyingine zina miss baadhi ya vitu au kitu katika SWOT?
 
What is SWOT and why kila organization inafanya SWOT analysis hasa wakati wakuandaa Strategic Plans? Je yaweza kuwa organizations nyingine zina miss baadhi ya vitu au kitu katika SWOT?

Hapa jambo la msingi ni ukichukua mahojiano ya CAG aliyoyafanya, Chukua swali aliloulizwa CAG, chukua jibu alilojibu CAG na wewe kama ni mtu huru ambaye hauko upande wowote wa mgogoro huu je unadhani hapa tulipofikia leo palistahili tufike hapa? na je tunahitaji chombo kitakachokuwa huru kutazama jambo hili kwa maslahi ya taifa bila kuegemea upande wowote?

mimi ninadhani tunahitaji mahakama ifanye tafsiri ya jambo hili kwa maana wahusika wamelikuza kuliko lilivyoonekana mwanzoni.
 
Back
Top Bottom