Hivi Lulu yuko katika hali gani kwa sasa?

nimejivika uhusika wa Lulu kwa kesi inayomkabili,nahisi ningekua ni mimi kabla ya hiyo tarehe13 Nov ndugu zangu wangekua wamenizika tayari kwa msongo wa mawazo
ila nampongeza kwa kuwa strong mpaka dakika hii.
Umehakikishaje kuwa yuko strong?
 
Kwa mujibu wa sheria namba..... Kifungu..... Mshtakiwa aliua bila kukusudia, na adhabu yake kwa mujibu wa sheria namba...., adhabu yaweza kifungo cha miaka....,au faini....., lakini kutokana na ushahidi......., Mahakama imeamua kumuachia huru Mshtakiwa!!!!!
mmh,mkuu Mahakama haiwezi kukutia hatiani halafu hapo hapo itoe Order ya kuachiwa huru...simply order inaweza kuja ktk moja style zifuatazo.

-Mshtakiwa Elizabeth Michael (Lulu) alishtakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia kinyume na kifungu cha....cha Kanuni ya Adhabu,Sura ya...ya Mwaka....Inadaiwa kuwa siku ya tarehe...mwezi wa....mwaka....Elizabeth Michael akiwa maeneo ya Sinza vaticani, Wilaya ya Kinondoni,Mkoa wa Dar es salaam bila kukusudia alimuua Steven Kanumba.

Katika kuthibitisha kesi yake upande wa mashtaka ulileta mashahidi watatu...kwa upande wa utetezi mshatakiwa alileta mashahidi wawili.

1) Baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili mahakama imeona kuwa upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha kesi dhidi ya mshtkiwa pasi na shaka..na hivyo mahakama hii inamtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kuuwa bila kukusudia. Mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka 5 jela. Haki ya rufaa imeelezwa kwa ambae hajaridhika na maamuzi.

2) Baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili mahakama imeona kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi ya mshtkiwa pasi na shaka..na hivyo mahakama hii inaona kuwa mshtakiwa hana hatia, hivyo inamuachia huru mshtakiwa, na inaamuru aachiwe mara moja isipokuwa kama atakamatwa tena kwa mujibu wa sheria. Mshtakiwa upo huru.
Haki ya rufaa imeelezwa kwa ambae hajaridhika na maamuzi haya.

NB: hapo ni baada ya Jaji kusoma mwenendo mzima wa kesi na maelezo ya mashahidi,na kuuchambua ushahidi wote,na pia kuweka reasoning zake kwa kila issue atayoiframe na pia kuchambua maoni ya wazee wa baraza...mwisho kabisa ndo anakuja kutoa moja kati ya hizo order kutegemeana na sababu atazokuwa amezieleza kwenye judgment yake.
 
Duh! Halafu nilishasahau kwamba nimeweka namba za akina Kamanda Sirro JF!!
Mkuu wewe ni nouma, nilipiga cm nikamuita "Lulu darling" asee nilisikia sauti moja ya ukakamavu...saiv niko offline mpk wiki ijayo labda
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom