Hivi Luhanjo,Jairo, Ngereja na Malima Wanasubiri nini kujiuzuru?

Hakikwanza

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
4,034
1,003
Kwangu binafsi nilijua ile siku ya jumamosi jioni wangekuwa wamemaliza mchakato wa kujiuzuru kwa jinsi walivyo ihujumu Tanzania. Lakini mpaka saa hivi kimya au ndio kanyaga twende Watanzania ni wepesi kulalama na kusahau
 
Tanzania hatuna culture ya kujiuzulu. It becomes even more so when you feel you are close to the man occupying Ikulu.
 
nyie endeleeni kulialia tuuuu wenzenu wanakula kuku na familia zao,tz uwaziri au uongozi wowote wa juu siyo UWAJIBIKAJI bali ni "DILI" so wewe upo tayri kupoteza "DILI ZAKO" So kama wewe huwezi kwa nini wenzako waweze????
 
unaweza kuona jinsi gani majamaa yalivyo makauzu,
kwa ile hotuba walilazimika kuandika barua siku ile ile.
 
Cha kushangaza zaid mtendaji mkuu wa shughuli za serikali bungen hasemi lolote yani kweli na CAG!!? Akatoa taarifa za ovyo bungen what kind of leaders we hv? Utasikia 2 wamepewa likizo tena ya malipo!!!
 
gazeti moja la leo limeandika kuwa
  • Malima kasema hatajiudhuru ng'o kwani hakufanya kosa
  • Luhanjo simu inaita hapokei
 
Nimefutilia uchambuzi wa magazeti kwenye tv na pia redioni,matarajio yng ni kusikia taarifa za ngeleza' na wenzake wote kuwa wamejiuzulu! Kwa njisi ilivyo naona bado wako ktk tafakuri ya kina juu ya maamuzi gn wachukue!
 
wakati report ya tume teule ya bunge inasomwa ngeleja alionyesha hufu kubwa sana
 
Tanzania hatuna culture ya kujiuzulu. It becomes even more so when you feel you are close to the man occupying Ikulu.

sio suala la culture, bali ni upuuzi wa viongozi wa juu kuwashinikiza hao wezi kujiuzulu., mbona lowassa, msabaha, idd simba walijihuzuru.
 
unaweza kuona jinsi gani majamaa yalivyo makauzu,
kwa ile hotuba walilazimika kuandika barua siku ile ile.

Wanafuata ushauri waliopewa, nafikiri ulisikia kutoka kwa most of MPs kuwa wasijiuzulu, kujiuzulu siyo suluhu ya matatizo ambayo yalitokea. Tusubiri...soon something will happen!
 
Wanasubiri kushauriana na "Mheshimiwa Dr Dr Dr...." ili wakubaliane way forward...Mzee Mzima Luhanjo yeye atavuta muda then tutaambiwa anastaafu, hao wengine tusipoangalia yatakuwa yale yale ya kuhamishiwa sehemu ingine ili waendelee na ulaji! Tusubiri Tuone!
 
Wanafuata ushauri waliopewa, nafikiri ulisikia kutoka kwa most of MPs kuwa wasijiuzulu, kujiuzulu siyo suluhu ya matatizo ambayo yalitokea. Tusubiri...soon something will happen!

haya mambo bwana bora kama unaroho ngumu mtu anakuzingua we mpige risasi tuangalie plan b lakini tunaishia tu kupost na kujichosha kwa vitu ambavyo unaambulia dharau..

bora nipende mapenzi na bongofreva siasa stress tupu by First Born
 
Wanafuata ushauri waliopewa, nafikiri ulisikia kutoka kwa most of MPs kuwa wasijiuzulu, kujiuzulu siyo suluhu ya matatizo ambayo yalitokea. Tusubiri...soon something will happen!

Rejao,
Wabunge wengi walisema watuhumiwa wote wawajibike. Alafu usipotoshe kuhusu dhana ya uwajibikaji. Kiongozi wa kisiasa anavyowajibika si lazima kwamba ndio suluhu ya tatizo au yeye ndio chanzo cha matatizo yaliyotokea. Kujiuzuru ni njia mojawapo ya kuonyesha umma kwamba hufurahii na unachukua yaliyofanywa na watendaji walio chini yako.

ukiamua kupiga risasi kwa nchi yetu hii utapiga viongozi wangapi? mm nafikiri cha kufanya ni viongozi wote kurudia maadili na kuwa na hofu yamungu.Hii itasaidia sana
 
Rejao,
Wabunge wengi walisema watuhumiwa wote wawajibike. Alafu usipotoshe kuhusu dhana ya uwajibikaji. Kiongozi wa kisiasa anavyowajibika si lazima kwamba ndio suluhu ya tatizo au yeye ndio chanzo cha matatizo yaliyotokea. Kujiuzuru ni njia mojawapo ya kuonyesha umma kwamba hufurahii na unachukua yaliyofanywa na watendaji walio chini yako.

Kuwajibika ni dhana pana sana. Tuwaachie wahisika wenyewe waamue, kama dhamira zao zitawatuma kufanya hivyo basi watafanya.
 
Acha wale kuku mpaka tutakapowafikisha mahakamani, ndo watu wengine watajifunza nini maana ya kuwa kiongozi wa umma.
 
Hawana wasiwasi wala hawaogopi kabisa na sitegemei kama watajiuzuru, wana power
 
nyie endeleeni kulialia tuuuu wenzenu wanakula kuku na familia zao,tz uwaziri au uongozi wowote wa juu siyo UWAJIBIKAJI bali ni "DILI"
Ni kweli Ngeleja anakula kuku na familia yake wakati hapa Mwanza familia moja yatima hawana raha ya maisha kutokana na misukosuko wanayopata kutoka kwa ngeleja na diwani wake wa ccm juu ya nyumba yao.Wao na pesa zao za ufisadi wanaona kuwa wana haki ya kuingilia uhuru wa watu.kama unataka laana na watoto wako endeleza unyama unaowafanyia hao yatima wa mungu kwani ss hv nyumba yao inaweza kuanguka wakati wowote kwani nusu imezungukwa na maji uliozuia yasiingie kwenye jengo lako kuharibu vifaa vya thamani vya hotel yako vilivyoshushwa juzi na semi trela 3 vikitoka china.Kijana unacheza na moto hao yatima ni waislam tangu enzi za mababu zao, kamwe hutaiweza hiyo vita wakiinuka
 
nyie endeleeni kulialia tuuuu wenzenu wanakula kuku na familia zao,tz uwaziri au uongozi wowote wa juu siyo UWAJIBIKAJI bali ni "DILI"
Ni kweli Ngeleja anakula kuku na familia yake wakati hapa Mwanza familia moja yatima hawana raha ya maisha kutokana na misukosuko wanayopata kutoka kwa ngeleja na diwani wake wa ccm juu ya nyumba yao.Wao na pesa zao za ufisadi wanaona kuwa wana haki ya kuingilia uhuru wa watu.kama unataka laana na watoto wako endeleza unyama unaowafanyia hao yatima wa mungu kwani ss hv nyumba yao inaweza kuanguka wakati wowote kwani nusu imezungukwa na maji uliozuia yasiingie kwenye jengo lako kuharibu vifaa vya thamani vya hotel yako vilivyoshushwa juzi na semi trela 3 vikitoka china.Kijana epuka laana ww unakula raha na watoto wako huku unawapa taabu wa wenzio ukiendelea na tabia hii tutaweka hadharani kila kitu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom