Hivi lipo wapi jopo la viongozi wetu wastaafu?

Kamtwanje H

Member
Oct 16, 2010
15
12
Kwa namna mambo yanavyoendelea hususani kweli hili suala la CAG na SPIKA nimekuwa nikijiuliza sana hivi wazee wetu wastaafu ambao mara nyingi wamekuwa wakishauri sana kwenye nyakati ngumu za uongozi wa nchi yetu hili jambo ni kwamba wameliona la kawaida au wanaacha ili waone mwisho wake?.

Kwanini wasiziite hizi pande mbili wakaondoa hii aibu ambayo taifa inalipata kwa malumbano yasiyo na tija?

Watu badala ya kukaa na kubishana namna ya kutatua shida za wananchi wanakaa kuzozana kwa nn unaniita hivi na huyu nitaendelea kuita kama viongozi mnaleta taswira gani kwa nchi yetu?

Mbona hii nchi ilishajijengea hekima na busara na kwa muda mrefu viongozi waliepuka misuguano isiyo na tija?.

Au wazee mna shida gani aswa inayowaweka kimya kiasi hiko mpaka mnaacha vijana wenu wakipoteza dira ya uongozi wa nchi yetu?.

MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRIKA.
 
Mkuu ngoja nikuulize swali moja, ivi kati ya hao wawili ni nani mwenye busara na ni nani ambae hana busara?ingawa niko nje ya mada kidogo.

Kwa maono yangu SPIKA si kwamba hana busara ila hakupaswa kupanic kwa namna ambayo amepanic. Kwa sababu ata adhabu ambayo bunge imelitoa ni kama vile katoa yy maana yy ndie aliyedictate suala alipeleke kwenye kamati jambo ambalo nadhani angeweza kwanza kumalizana nje ya sheria yy na mzee mwenzake na mambo yasingefika kama yalivyo sasa.
 
Mkuu umeongea point, halafu ukizingatia ni watu wazima ni wazee wetu walipaswa waongee yamalizike kimya kimya kama kipindi kile kamati ya bunge na maadili ilivomwita na kumhoji CAG mambo yakawa kimya, heshima zikawa zimewarudia wote, lakini kwa sasa wameshaharibu.
 
Kwa maono yangu SPIKA si kwamba hana busara ila hakupaswa kupanic kwa namna ambayo amepanic. Kwa sababu ata adhabu ambayo bunge imelitoa ni kama vile katoa yy maana yy ndie aliyedictate suala alipeleke kwenye kamati jambo ambalo nadhani angeweza kwanza kumalizana nje ya sheria yy na mzee mwenzake na mambo yasingefika kama yalivyo sasa.
Na yule kapanic kwasababu ya hii mitandao yetu kumsema sana.
 
Leo nilivyoisikiliza hotuba ya spika kwa waandishi wa habari na ruhusa ya kuulizwa maswali, ndiyo nimeelewa vizuri kiini cha tatizo.

Ndugai kajitahidi sana kufafanua mambo ya kimsingi na namna hoja zinazowasilishwa na Cag Bungeni na jinsi zinavyofanyiwa kazi kwa mapana yake.

Nimemuelewa vizuri sana, maana nilisikiliza kwa makini kutafuta point kama nipo darasani.

Spika kafafanua kuwa Assad anaposema kuwa bunge ni dhaifu anakuwa amemjumuisha hadi rais mteuzi wake pamoja na baraza lake la mawaziri ambao kwa ujumla wao ni sehemu ya bunge.

Kwa maelezo hayo tu, nimegundua kuna tatizo, na kwa muktadha wa sakata hili kumbe, Assad yupo peke yake.

Ndugai hawezi kukurupuka na kubwabwaja na waandishi wa habari kwa kujiamini namna hiyo bila ya kuwa na baraka flaniflani kutoka sehemu flani.

Kwa maelezo ya spika, bado Cag kapewa angalizo namna ya kuweza kumaliza soo hili, lakini sidhani kama ataweza kuifanyia kazi 'home work' hiyo, kwa kuwa kala yamini kuendelea kulitumia neno hilo na hataki kujishusha kwa 'samahani' ya aina yoyote ile.

Nionavyo mimi kulivalia njuga sakata hili na kupata ushindi wa aina yoyote kwa Assad hakutamletea tija.

Hivyo basi ajishushe na aende kwa Jpm akaombe radhi mambo yawekwe sawa yaishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe na ndugayi ni mtu na mdogo wake

Au

Na wewe ni mnufaika na huu mgogoro

Hauhitaji akili ya namna yoyote kubaini bwana ndugai anapoteza mda, pesa na heshima ake kwa kukubali kutumiwa , alikataa kupokea taarifa iliyokuwa na saini ya huyu mzee kipi kilichomfanya aipokee
 
Mimi sina uhusiano na Ndugai wala si mnufaika.
Ila mkuu comment niliyotandaza hapo nimeifanyia evaluation baada ya kusikiliza hotuba ya Ndugai kwa makini sana kipindi cha mchana wa leo.
Hayo unayoendelea kuyauliza kayajibu tu vizuri.
Ninakuomba ingia you tube tafuta hiyo hotuba uichambue ili tujadili kwa pamoja. Ahsante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo nilivyoisikiliza hotuba ya spika kwa waandishi wa habari na ruhusa ya kuulizwa maswali, ndiyo nimeelewa vizuri kiini cha tatizo.

Ndugai kajitahidi sana kufafanua mambo ya kimsingi na namna hoja zinazowasilishwa na Cag Bungeni na jinsi zinavyofanyiwa kazi kwa mapana yake.

Nimemuelewa vizuri sana, maana nilisikiliza kwa makini kutafuta point kama nipo darasani.

Spika kafafanua kuwa Assad anaposema kuwa bunge ni dhaifu anakuwa amemjumuisha hadi rais mteuzi wake pamoja na baraza lake la mawaziri ambao kwa ujumla wao ni sehemu ya bunge.

Kwa maelezo hayo tu, nimegundua kuna tatizo, na kwa muktadha wa sakata hili kumbe, Assad yupo peke yake.

Ndugai hawezi kukurupuka na kubwabwaja na waandishi wa habari kwa kujiamini namna hiyo bila ya kuwa na baraka flaniflani kutoka sehemu flani.

Kwa maelezo ya spika, bado Cag kapewa angalizo namna ya kuweza kumaliza soo hili, lakini sidhani kama ataweza kuifanyia kazi 'home work' hiyo, kwa kuwa kala yamini kuendelea kulitumia neno hilo na hataki kujishusha kwa 'samahani' ya aina yoyote ile.

Nionavyo mimi kulivalia njuga sakata hili na kupata ushindi wa aina yoyote kwa Assad hakutamletea tija.

Hivyo basi ajishushe na aende kwa Jpm akaombe radhi mambo yawekwe sawa yaishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Akaombe radhi kwa kosa lipi ?
 
Tujikumbushe kidogo Cjui ni siasa kipindi kile cha primary, civics secondary, Gs n.k
Tulisoma kuwa kuna MIHIMILI MITATU, Serikali, Bunge na Mahakama ambayo haiingiliani, na iko hivyo siku zote.
Huyu spkr anaposema kajumuisha serikali ni kutaka kuupa mgogoro nguvu mpya lakini kiukweli sivyo ilivyo.
Kama kwa mujibu wa spker kuwa serikali ni sehemu ya bunge basi ni kweli HAWAWEZI KUIWAJIBISHA na kutokua na nguvu ya kuwawajibisha jitafutie mwenyewe neno la kuweka hapa (......)
Dr Rwaitama ameeleza juzi kuwa ili umwajibishe mtu haitakiwi awe sehemu ya wewe, kunahitajika sana kuireview katiba na kuweka haya mambo sawia.
CAG yuko sahihi kusema bunge ni dhaifu ma spkr anakiri kabisa udhaifu uliopo ni kuwa kesi ya ngedere anaamua nyani! Tunataka nini tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
una uhakika gani kama wamekaa kimya? au ni vile kwamba mimi na wewe hatujaona kwenye vyombo vya habari na social media?

Nilitarajia kama wamewekwa chini na wazee basi asingetokea yeyote kati yao ambae angeongea na vyombo vya hbr kurusha maneno kwa mwenzake. Sanasana wangeweza kuitisha mjutano wa pamoja wa vyombo vya hbr wakatoa neno la pamoja. Ingeleta faraja sana kuliko hivi ilivyo.
 
Leo nilivyoisikiliza hotuba ya spika kwa waandishi wa habari na ruhusa ya kuulizwa maswali, ndiyo nimeelewa vizuri kiini cha tatizo.

Ndugai kajitahidi sana kufafanua mambo ya kimsingi na namna hoja zinazowasilishwa na Cag Bungeni na jinsi zinavyofanyiwa kazi kwa mapana yake.

Nimemuelewa vizuri sana, maana nilisikiliza kwa makini kutafuta point kama nipo darasani.

Spika kafafanua kuwa Assad anaposema kuwa bunge ni dhaifu anakuwa amemjumuisha hadi rais mteuzi wake pamoja na baraza lake la mawaziri ambao kwa ujumla wao ni sehemu ya bunge.

Kwa maelezo hayo tu, nimegundua kuna tatizo, na kwa muktadha wa sakata hili kumbe, Assad yupo peke yake.

Ndugai hawezi kukurupuka na kubwabwaja na waandishi wa habari kwa kujiamini namna hiyo bila ya kuwa na baraka flaniflani kutoka sehemu flani.

Kwa maelezo ya spika, bado Cag kapewa angalizo namna ya kuweza kumaliza soo hili, lakini sidhani kama ataweza kuifanyia kazi 'home work' hiyo, kwa kuwa kala yamini kuendelea kulitumia neno hilo na hataki kujishusha kwa 'samahani' ya aina yoyote ile.

Nionavyo mimi kulivalia njuga sakata hili na kupata ushindi wa aina yoyote kwa Assad hakutamletea tija.

Hivyo basi ajishushe na aende kwa Jpm akaombe radhi mambo yawekwe sawa yaishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali ina mihimili mitatu,mmoja wapo ni bunge,ukisema rais ni sehemu ya bunge ni kweli lakin haihalalishi kua neno dhaifu naye linamuhusu kama inavyotafsiriwa anachokifanya Ndugai. kumuhusisha rais ni kutafuta support yake ili kumchochea Mkulu ionekane na yey katukanwa na CAG.Neno dhaifu kwa taaluma yake yey limetumika kukosoa upungufu uliopo katika bunge kama taasisi nyingne, Pia CAG ikumbukwe kazi yake ni kukosoa kasoro zilizopo katika izi taasisi zote anazozikagua sio bunge peke yake hivyo bas kumtaka CAG ajiudhuru ni kudhulumu haki ya taasisi nyingne ambazo zimekosolewa na zimekaa kimya au zilienda kimya kimya ofisi ya CAG kufahamu udhaifu wao na sio kushout ktk vyombo vya habari..Mwisho kabisa nilitegemea Bunge lingeanza kuuliza UDHAIFU wao ni upi walioambiwa na CAG kabla ya kulikataa neno dhaifu ambalo naamin hata wew mtoto wako anapokuletea ripoti kutoka shule hua ina sehemu ya Vizuri sana,vizuri, wastani na " "dhaifu", Je wazaz nao waandamane huko mashuleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo nilivyoisikiliza hotuba ya spika kwa waandishi wa habari na ruhusa ya kuulizwa maswali, ndiyo nimeelewa vizuri kiini cha tatizo.

Ndugai kajitahidi sana kufafanua mambo ya kimsingi na namna hoja zinazowasilishwa na Cag Bungeni na jinsi zinavyofanyiwa kazi kwa mapana yake.

Nimemuelewa vizuri sana, maana nilisikiliza kwa makini kutafuta point kama nipo darasani.

Spika kafafanua kuwa Assad anaposema kuwa bunge ni dhaifu anakuwa amemjumuisha hadi rais mteuzi wake pamoja na baraza lake la mawaziri ambao kwa ujumla wao ni sehemu ya bunge.

Kwa maelezo hayo tu, nimegundua kuna tatizo, na kwa muktadha wa sakata hili kumbe, Assad yupo peke yake.

Ndugai hawezi kukurupuka na kubwabwaja na waandishi wa habari kwa kujiamini namna hiyo bila ya kuwa na baraka flaniflani kutoka sehemu flani.

Kwa maelezo ya spika, bado Cag kapewa angalizo namna ya kuweza kumaliza soo hili, lakini sidhani kama ataweza kuifanyia kazi 'home work' hiyo, kwa kuwa kala yamini kuendelea kulitumia neno hilo na hataki kujishusha kwa 'samahani' ya aina yoyote ile.

Nionavyo mimi kulivalia njuga sakata hili na kupata ushindi wa aina yoyote kwa Assad hakutamletea tija.

Hivyo basi ajishushe na aende kwa Jpm akaombe radhi mambo yawekwe sawa yaishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na ww unaingia kwenye mkumbo wa spika kutaka huruma ya serikali ili imsaidie kumwajibisha CAG. Na sijui kama ulisoma hapa nchini maana shule ya msingi ama sekondari, tumesoma kuwa kwa mujibu wa katiba, kuna mihimili 3 ambayo haiingiliani, kwamba mihimili hiyo ni bunge, dola (serikali) na mahakama. Sasa unaposema kuwa CAG kusema bunge ni dhaifu ameijumuisha serikali , siyo sahihi, labda uniambie kuwa katiba imebadilika na kwamba bunge na serikali ni muhimili mmoja. Katika mnyukano huu, binafsi naona spika ndo anaukuza, ile kumwita CAG kwenye kamati ya bunge pamoja na maazimio yote yaliyotoka, ilikuwa inatosha. Sasa kuibua tena hoja hii ni kutaka kuonyesha ukuu wake kwa CAG kama ambavyo huwa anafanya kwa baadhi ya wabunge. Kwakua tayari walishamwita na kumwazimia, hiyo inatosha, aache kuwagawa Watanzania katika mzozo huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa maono yangu SPIKA si kwamba hana busara ila hakupaswa kupanic kwa namna ambayo amepanic. Kwa sababu ata adhabu ambayo bunge imelitoa ni kama vile katoa yy maana yy ndie aliyedictate suala alipeleke kwenye kamati jambo ambalo nadhani angeweza kwanza kumalizana nje ya sheria yy na mzee mwenzake na mambo yasingefika kama yalivyo sasa.
Samahn tena mkuu mda wa spika kuongoza unaisha lin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom