Hivi lini na mimi nitapenda????

Wa Bagamoyo

Senior Member
Apr 2, 2012
118
12
Eti jamani huu ni ugonjwa au ni nini mana sijawahi penda mwanamke, hua nasikia tu mapenzi yanaumiza bt me sijui hiyo kitu ipo vipi. Me ni single boy ukinipenda namaliza.leoleo túu. Je nitaweza badilika jamani mana umri wa kuoa umefika?
 
Serikali ya mtu ni mawazo yake mwenyewe..bila kusahau dunia yako chaguo lako!
 
ebu jaribu kuanzisha mapenzi na mwanaume mwenzio uone kama yananoga au hayanogi,kwa ushauri zaidi unaweza kuinbox..
 
hujawahi penda but mtu akikupenda unamaliza leo leo... ndiyo unamaanisha nini hapo?
 
Kupenda ni mazoea yanayotokana na malezi toka ukiwa mtoto, inavyoonyesha ulikosa kitu kinachoitwa mapenzi toka kwa wazazi.
Tunashukuru mungu katika kipindi chetu hiki kuna majarida mengi tu ya kimapenzi yanofundisha jinsi gani mtu unavyoweza toka hali moja kwenda nyingine ya kimapenzi.
Jibihidishe kutafuta hayo majarida ili uweze pata shule ya mapenzi.
 
Inawezekana una matatizo ya kisaikolojia, nenda kwa wataalum wa saikolijia na akili za watu wanaweza kukufanyia 'kanseling' ukaondokana na hilo tatizo ...
 
Kwenye swala la kupenda wanaume wengi huwa hatupendi kusema ukweli.

Tunapenda tuonekane tuna moyo migumu kuliko binadamu wa kawaida, ni wanaume wachache ambao tuna huwezo wa kusema hadharani kuwa tume fall in love au tulisha wai ila kutokana na kutendwa hatu amini kwenye mapenzi.

Nawasifu sana wakina dada wao wako wazi sana kama wametendwa watasema,kama wanapenda watasema, kama hawaamini kwenye mapenzi baada ya kutendwa wataweka wazi.

Sisi wanaume ni wagumu kusema ukweli.
 
Kaka hauko pake yako,ila kwa uzoefu tunatofautiana,mwenzio hisia za mapenzi zilikufa pale mchumba wangu aliponisaliti na nikajidai kupoza machungu kwa kuwa mlupo bahati nzuri sikuyakanyaga,mwisho nikajiuliza kama sitapenda tena ni nani atakayekuwa mama wa watoto wangu..??Nikatafuta mtaalamu wa ushauri na sasa niko katika hatua nzuri tu ya kutengeneza uchumba na mungu akijaalia ndoa itafuata kwa mchumba ambaye nimekutana naye hapahapa JF.Tafuta washauri watakusaidia,kwa kuanzia nenda pale Muhimbili kama uko Dar,kuna kitengo cha Wendawazimu,ulizia kuna wataalamu wazuri sana na nina imani wanaweza kukusaidia katika tatizo lako..
 
Sasa unamaanisha hii hali ni ukichaa???
 
Back
Top Bottom