Hivi leo Mwalimu Nyerere angekuwepo angejisikiaje?

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Ni wazi Siasa za Tanzania zimejiongezea wasifu wa ZeComedy! Jinsi CCM wanavyochukua Wabunge na madiwani wa Ukawa-Chadema ni kama enzi za vita baridi za kuibiana majasusi. Lakini kuitisha mkutano usiku wa manane katangaza ni aibu.

Kama Bwana Humphrey Na Serikali Yao Wangekua kweli Wanawajari Hawa Wananchi Wanaowaita Wanyonge Tafadhari Wangesitisha Hii Biashara Ya Ununuzi Wangesubiri Mpaka 2020. Kwa Sababu Inagharimu Sana Pesa Zetu Ambazo Zingeenda Kwenye Maendeleo Mengine Waheshimuni Wananchi Wenu Basi.

Huwezi ukawa chama tawala imara kama unauwa upinzani na kudhani ndiyo siasa! CCM ya sasa ni mbovu na oga kuliko zote zilizowahi kupita... huwezi ukawa muoga kiasi hiki na hii ni dalili ya udhaifu sanaaa.

Ni haki ya kikatiba ya raia kujiunga na Chama atakacho Wakati wowote. Pia naamini ukiwa Kiongozi wa kuchaguliwa unapoteza haki binafsi kadhaa. Hama hama ya Wabunge, Madiwani nk inakatisha tamaa Wananchi. Inapelekea raia kuchukia Siasa. Ni hatari kwa usalama wa nchi yetu.

Mbunge Aliomba Kura Kwa Wananchi Mchana Hadharani Na Kwa Unyenyekevu Wote, Wananchi Wakamuamini Na Kumpa Ili Awatumikie, Leo Bila Hata Ya Kuwaomba Radhi Wale Wananchi Ana Bagain Biashara Na Mnunuzi Wa Mbuzi Usiku.. Mnunuzi Anafanya Yake Na Habari Imeishia Hapo. PUMBAVU

CCM wafanye marekebisho ya Katiba. Turudi kwenye chama kimoja. Baba wa Taifa alilazimisha ajenda ya vyama vingi. Hatukuwa tayari. Na hatuko tayari hata sasa.

mr mkiki.
 
Nyerere angeona aibu kwa kutucheleweshea maendeleo baada ya kuleta limfumo libaya la "ujamaa"sasa hivi mzee mkuu analeta maendeleo kwa kasi ya mwanga,kwa ufupi nyerere angepata tabu sana wakati huu.mtoa post umesema wabunge na madiwani wa upinzan wananunuliwa!,na mimi naomba kuuliza hivi ni nani aliwanunua Lowasa,Sumaye, na Nyalandu?
 
We are not in the past!
songa mbele kijana mdogo!
That’s all!
 
Wasingefanya haya mbele ya Mwalimu. Kuna kipindi ticha alitoka Butiama moja kwa moja hadi dodoma akawakuta wamejifungia ndani wanatafuta Rais wa nchi; akaingia moja kwa moja mbele na cha kushangaza yeye ndiyo akawa mwenyekiti. Kuna maswali??? Tunaendelea.....

Yaliyotokea hapo waliokiwamo wanajua.
 
wengi nyerere mmemsoma kwenye vitabu na kumsikia kwenye hotuba zilizojaa propaganda tu. yeye ndio baba wa udikteta nchi hii, yeye ndio mwasisi wa CCM na "fikra za mwenyekiti", yeye ndio mtunzi mkuu wa katiba tunayoitumia sasa inayomfanya rais kuwa mungu mtu. Hivyo basi angekuwepo angefurahi kwelikweli kuona CCM inavyoendesha nchi, tena angefurahia zaidi urafiki wa vijana wake "jiwe" na "PK"
 
Nyerere angekuwepo chadema kwanza isingekuwepo, hata chadema ishukuru Nyerere hayupo, hata kulikuwa na tetesi walioko chadema walimmaliza Nyerere ili waweze kupata nafasi ya kuingia madarakani na kuiba, lkn walikosea stepu sasa hivi nchi yetu haiibiki ng'o na hata hizo ruzuku zetu mnazoiba na kuzitumia kwa matumizi binafsi mtapigwa stop!
 
Utafika mda utashindwa hata kuongea then utajua kuwa wewe ni kiumbe gani. Endelea kujichetua
 
Wasingefanya haya mbele ya Mwalimu. Kuna kipindi ticha alitoka Butiama moja kwa moja hadi dodoma akawakuta wamejifungia ndani wanatafuta Rais wa nchi; akaingia moja kwa moja mbele na cha kushangaza yeye ndiyo akawa mwenyekiti. Kuna maswali??? Tunaendelea.....

Yaliyotokea hapo waliokiwamo wanajua.
.....
 
Ulishawahi kujiuliza kuhusu hili neno "ulimwengu watatu"..?
ndio huu tunamoishi!
heri alieomba malaika ashuke aje azime mitandao angeomba malaika wa uangamizi ashuke apambane na mafisadi lkn zimwi kwa zimwi hayalani!

Kama wanakubali kununulika basi si viongozi wenye uzalendo,kama wananunua basi si wazalendo,.. Mkuu kufikia 2020 watanunuliwa wa bei ya chini wale wa khanga,chumvi,myekundu miwili,tisheti n.k sahivi bidhaa imepanda.
 
Nyerere kafa 1999 unataka mambo yaendelee kufanyika kama tuko 1999.
Demokrasia ni gharama na mliichagua na kuyavulia maji sasa myaohe.
 
Nyerere angekuwepo chadema kwanza isingekuwepo, hata chadema ishukuru Nyerere hayupo, hata kulikuwa na tetesi walioko chadema walimmaliza Nyerere ili waweze kupata nafasi ya kuingia madarakani na kuiba, lkn walikosea stepu sasa hivi nchi yetu haiibiki ng'o na hata hizo ruzuku zetu mnazoiba na kuzitumia kwa matumizi binafsi mtapigwa stop!
GPA 32 UTAKUWA NAYO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom