Hivi laki 2 na nusu itanitoa kimaisha nikisave kwa mwezi?

AHAKU

Member
Jan 28, 2010
26
0
Salam wanajamii wenzangu. Naamini humu hakuna wachoyo wa msaada wa mawazo. Ni kwa matarajio haya naomba kuuliza mimi nafanya kazi sekta binafsi kama mwajiriwa mwisho wa mwezi naweza ku save laki mbili na nusu
Ninauliza hivi kwa kiasi hiki ninawezaje kukitumia ili angalau miaka michache ijayo niweze kuwa na kabanda kangu na kisha angalau kamkoko kamoja kupunguza adha ya usafiri hapa mjini
Nawashukuru sana
 
ChiefmTz

JF-Expert Member
Apr 15, 2008
2,904
2,000
Hizo Laki 2 na nusu ndizo take home au ndo ballance baada ya kutoa mahitaji muhimu ya mwezi.
 
MLATIE

Senior Member
Apr 14, 2010
179
195
kaka mipango tu unapunguza starehe unasave kwenda mbele watu wanapokea 150,000 na wanasomesha watoto sekondari.punguza anasa mzigo unatosha huo
 
AHAKU

Member
Jan 28, 2010
26
0
hicho kiasi mkubwa ni baada ya kutoa gharama zingine kama kuendesha familia, usafiri na mengineyo. Yaani huwa nabakiwa na mshiko huo baada ya kugaharamia vitu vyote muhimu vya mwezi
 
hashycool

JF-Expert Member
Oct 2, 2010
6,574

A bank is a place that will lend you money if you can prove that you don't need it.....akili kumkichwa
 
Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,523
2,000
Kama ndo take home baada ya matumizi yote basi we dume endelea tu kuweka!
 
birungi

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
390
195
hizo nyingi,kama una uwezo chukua mkopo mzuri ujenge nyumba hata uitumie kwa biashara.nadhani kila mwisho wa mwezi watakua wanakukata kama hiyohiyo laki 2 na nusu ambayo ni ziada kwako.baada ya mda ile nyumba itakua inakulipa kidogokidogo.au unaweza ukajenga ukaishi mwenyewe utakua umeokoa ile kodi yako.
 
Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
7,004
2,000
hicho kiasi mkubwa ni baada ya kutoa gharama zingine kama kuendesha familia, usafiri na mengineyo. Yaani huwa nabakiwa na mshiko huo baada ya kugaharamia vitu vyote muhimu vya mwezi
Ingawa inatarajia na kiwango chako cha mshahara, lakini kwa standard za wengi humu, ikiwamo na mimi mwenyewe, Mkuu unapata mshahara mkubwa sana. Sijaona ni jinsi gani naweza kubakiwa na laki mbili unusu mwisho wa mwezi nikitoa gharama zote... sana sana nahitaji kiasi kama hicho zaidi ili kukamilisha mahitaji. Endelea kuserve mkuu, utatoka baada ya muda mfupi tu, si tu kwa kujenga nyumba, bali pia kuanzisha biashara yako mwenyewe.
 
ejogo

JF-Expert Member
Dec 19, 2009
990
225
Kwanini usiende banki kuchukua mkopo ambao makato yake yasizidi laki mbili kwa mwezi ambayo ndio saving yako ya mwezi! Ukisema udundulize hiyo itakuchukua ages kutimiza ndoto zako. Au unaweza kufikiria biashara fulani ambayo itakuwezesha kuizalisha hiyo pesa na hatimaye kutimiza ndoto zako.
 
Mkeshahoi

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
2,471
1,225
Salam wanajamii wenzangu. Naamini humu hakuna wachoyo wa msaada wa mawazo. Ni kwa matarajio haya naomba kuuliza mimi nafanya kazi sekta binafsi kama mwajiriwa mwisho wa mwezi naweza ku save laki mbili na nusu
Ninauliza hivi kwa kiasi hiki ninawezaje kukitumia ili angalau miaka michache ijayo niweze kuwa na kabanda kangu na kisha angalau kamkoko kamoja kupunguza adha ya usafiri hapa mjini
Nawashukuru sana
huna extended family inakutegemea ukuachilia mbali familia?
 
Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,273
2,000
hicho kiasi mkubwa ni baada ya kutoa gharama zingine kama kuendesha familia, usafiri na mengineyo. Yaani huwa nabakiwa na mshiko huo baada ya kugaharamia vitu vyote muhimu vya mwezi

Oa kwanza ili upate wa kushauriana naye kimawazo na kupunguza kula hotelini ili hiyo akiba iongezeke
 
Next Level

JF-Expert Member
Nov 17, 2008
3,154
1,195
Ingawa inatarajia na kiwango chako cha mshahara, lakini kwa standard za wengi humu, ikiwamo na mimi mwenyewe, Mkuu unapata mshahara mkubwa sana. Sijaona ni jinsi gani naweza kubakiwa na laki mbili unusu mwisho wa mwezi nikitoa gharama zote... sana sana nahitaji kiasi kama hicho zaidi ili kukamilisha mahitaji. Endelea kuserve mkuu, utatoka baada ya muda mfupi tu, si tu kwa kujenga nyumba, bali pia kuanzisha biashara yako mwenyewe.

MN,

Nipo nakubaliana na hoja yako mkuu....napata mshahara mkubwa sana kwa viwango vya bongo....lakini, hata mwezi mmoja sijaweza fanikiwa kuwa na surplus....ingawa hata baada ya kulamba mkopo bank nimekuwa hivyo hivyo, huwa na break even tu au kuwa na deficit.....!

So nafikiri huyu jamaa mambo yake mazuri....250k is a lot of savings.........! anaweza lamba hata mkopo wa 10m au hata 20 or 30 m kulingana na basic salary yake akafanya mambo makubwa sana......! Hata akisave hiyo 250k....kwa mwaka atakuwa na 3m, akifanya miaka mitano atakuwa na 15m.....a very good money kuanzisha business ndogo aiseee!
 
Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
1,500
MN,

Nipo nakubaliana na hoja yako mkuu....napata mshahara mkubwa sana kwa viwango vya bongo....lakini, hata mwezi mmoja sijaweza fanikiwa kuwa na surplus....ingawa hata baada ya kulamba mkopo bank nimekuwa hivyo hivyo, huwa na break even tu au kuwa na deficit.....!

!

Mkuu next level hauko serious juu ya kuweka akiba; unaonekana wewe ni mtu ambaye unatumia kadili unavyopata, which to me is not good kama kweli una malengo ya kufanya kitu fulani baadae!

Nina rafiki yangu mmoja anaishi DSM, wakati akipokea mshahara wa laki sita take home alikuwa anasema mshahara anaolipwa unamtosha tu kuishi basi. Alipoongzewa mshahara mpaka kufikia take home ya milioni moja na laki mbili akabadili life style kwa kuhama Tandika alikokuwa anaishi na kuhamia Sinza, pia akanunua na gari GX100. Mwaka huu mwanzoni kapata kazi nyingine kampuni moja ya nje analipwa take home ya 3.5 milioni. Tayari hivi majuzi kahama Sinza na kuhamia Mikocheni, kachukua mkopo wa gari nyingine aina ya Toyota Harrier huku akimwachia mke wake atumie ile GX100.

Next level nimetoa mfano huo mrefu kidogo kutaka kukueleza namna ambavyo waafrika walio wengi wanavyoshindwa ku manage pesa zao vipato vinapoongezeka. Wengi wakipata kipato zaidi wanabadilisha bar wanazokunywa pombe, mademu wa matawi ya juu, na magari. Hii yote ni ulimbukeni kama ongezeko la kipato hali justify kihivyo ongezeko la matumizi ya anasa!!

Mi nashauri jamaa aende kwa banker wake kwa ajiri ya kusolicit mkopo ili ajengee nyumba kwa sababu kuweka tu akiba kidogo kidogo kuna hatari ya kuja kuitumia kwenye dharula kama vile misiba, kuuguza mgonjwa n.k.
 
narudia tena..A bank is a place that will lend you money if you can prove that you don't need it.....akili kumkichwa....laki mbili pesa ya kaunta!
 
PayGod

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
1,259
1,225
chukua mkopo bank, ila kabla ya kuchukua panga mipango ya kuifanyia hiyo ela , ndo ukachukue huo mkopo
 
Neytemu

Member
Nov 7, 2010
83
0
Mkuu next level hauko serious juu ya kuweka akiba; unaonekana wewe ni mtu ambaye unatumia kadili unavyopata, which to me is not good kama kweli una malengo ya kufanya kitu fulani baadae!

Nina rafiki yangu mmoja anaishi DSM, wakati akipokea mshahara wa laki sita take home alikuwa anasema mshahara anaolipwa unamtosha tu kuishi basi. Alipoongzewa mshahara mpaka kufikia take home ya milioni moja na laki mbili akabadili life style kwa kuhama Tandika alikokuwa anaishi na kuhamia Sinza, pia akanunua na gari GX100. Mwaka huu mwanzoni kapata kazi nyingine kampuni moja ya nje analipwa take home ya 3.5 milioni. Tayari hivi majuzi kahama Sinza na kuhamia Mikocheni, kachukua mkopo wa gari nyingine aina ya Toyota Harrier huku akimwachia mke wake atumie ile GX100.

Next level nimetoa mfano huo mrefu kidogo kutaka kukueleza namna ambavyo waafrika walio wengi wanavyoshindwa ku manage pesa zao vipato vinapoongezeka. Wengi wakipata kipato zaidi wanabadilisha bar wanazokunywa pombe, mademu wa matawi ya juu, na magari. Hii yote ni ulimbukeni kama ongezeko la kipato hali justify kihivyo ongezeko la matumizi ya anasa!!

Mi nashauri jamaa aende kwa banker wake kwa ajiri ya kusolicit mkopo ili ajengee nyumba kwa sababu kuweka tu akiba kidogo kidogo kuna hatari ya kuja kuitumia kwenye dharula kama vile misiba, kuuguza mgonjwa n.k.

yap!maelezo za brooklyn yana muongozo mzuri ila kweli kudunduliza itamchukua mda mrefu sana kufanikicha ndoto yako.kama kuna uwezekano upate salary loan itakusogeza. HONGERA kwa Kuweza kufanya savings kwa kiasi hicho
 
Kweli

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,151
1,500
Salam wanajamii wenzangu. Naamini humu hakuna wachoyo wa msaada wa mawazo. Ni kwa matarajio haya naomba kuuliza mimi nafanya kazi sekta binafsi kama mwajiriwa mwisho wa mwezi naweza ku save laki mbili na nusu
Ninauliza hivi kwa kiasi hiki ninawezaje kukitumia ili angalau miaka michache ijayo niweze kuwa na kabanda kangu na kisha angalau kamkoko kamoja kupunguza adha ya usafiri hapa mjini
Nawashukuru sana

hicho kiasi mkubwa ni baada ya kutoa gharama zingine kama kuendesha familia, usafiri na mengineyo. Yaani huwa nabakiwa na mshiko huo baada ya kugaharamia vitu vyote muhimu vya mwezi

Kwanza nakupa hongera kwa kujenga utamaduni wa kujisevia, ili ufanikiwe kusevu vitu 3 muhimu lazima uwe navyo: NIA, Utekelezaji na Kuamini. Kisha:
1. Uwe na malengo (goals) - andika "blueprint" in details yale yote unayokusudia kufanikisha katika muda ulioupanga. Ila uwe realistic mfano baada ya miaka 5 uweze kumiliki nyumba ya millioni 15 mpaka 20 na sio ndoto ya hekalu la billioni 3.
2. Andaa strategies na routine na ukomae nayo, usitetereke: Lengo katika hili ni kubana matumizi na kuifanya saving yako iongezeke zaidi, unapoanza kujisevia jambo la kwanza muhimu sana kujifunza ni ujanja wa kujua nini tofauti baina ya "thamani"(Assets) na "hasara" ( liabilities) thamani = kitu ambacho kina uhakika wa kuongeza kipato na hasara = kile ambacho kinahitaji fedha kujiendesha na hakileti tija, mfano mtu kakuuzia dhahabu bei bwerere hio ni thamani, gari ya millioni 7 inauzwa kwa millioni 3 hio ni thamani, ila unatakiwa uwe mjanja na makini sana katika hili. vitu kama TV, Hi-Fi system, Fenicha, gari ni hasara kwa sababu gari linahitaji mafuta, Tv, fenicha hata ukitaka kuuza ni taabu na mara nyingi hautopata faida, ni bahati hata ku break-even.
3. Live frugaly - Matajiri wa kujitengeneza wengi wamefika huko kwa sababu waliishi kwa kujibana - sisemi kama unataka utajiri ila the same rules apply for Savers, Kama ulikuwa unakula chips kuku kila usiku, jitahidi iwe alau usiku mmoja na badala yake uanze kujipikia, andaa bajeti yako ya kula kila wiki na uangalie wapi unaweza kubana zaidi, mfano kama unanunua viungo gengeni, jaribu kwenda pale sokoni usiku mmoja k/koo na ujinunulie kwa jumla. Kama mtu wa ulabu punguza mahudhurio Pub, jinunulie jumla bia zako kwa wiki na utulie nyumbani usiku.
Ukizingatia haya ambayo ni basics bila shaka utafanikisha malengo, wengi tulianza hivi hivi mpaka kufikia kumiliki vibanda nk.
 
Neytemu

Member
Nov 7, 2010
83
0
kama haujaoa ukioa inaweza kupunguza savings na hata kusababisha deficit kubwa!we kopa ufanye kitakachowezekana kwa wakati huu.Vinginevyo uchambuzi yakinifu unahitajika kumpata huyo wa kukushauri positively na aje akiwa anaelewa maana ya kufanya savings
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom