Hivi kwenye hili bomba la mafuta Kati yetu na Uganda sisi tunapata Nini na kwanini?

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,240
9,527
Biashara inayoongelewa kwenye bomba la mafuta Kati ya Tanzania na Uganda inaonekana Kama ya wadau wawili, ila nasikia na Mkenya akiongelewa na Mmarekani pia, hawa jamaa vipi? Ni story tu au wana chao?

Tanzania na Uganda zimegawana 50% ya share 25% kila mmoja. Hizo 50% nyingine wapo kina nani na wanachangia nini?

Tanzania imeshakubali kutoa eneo lake kwaajili ya hili bomba, imetoa pia miaka ishirini ya 'tax depreciation holiday' na VAT ya Sifuri(0).
Hao wadau wengine wenye asilimia 75% (majority) wametoa nini?

Kuna anayeweza kutuambia haya mambo yakoje tofauti na zile story za dada zetu kupata kazi ya kuuza chakula?

Na issue ya kuwa ugunduzi wa gesi tutafaidika nao zaidi kwaajili ya hili bomba imekaaje?
Kwanza tuna gesi ya ziada ya kuuza kwenye huu mradi kwa maana ya nishati?
Hivi kuna ukweli wowote, hata kidogo?

Usije kuwa mradi mwingine wa kumuimbia Jiwe utukufu na sifa wakati waimbaji hatupati kitu!!
 
Kwa vile bomba litapita Tanzania kwa sehemu Kubwa,basi watanzania watapata ajira,hilo moja
 
Hizo percentage ni kwa ajili ya umiliki WA refinery, Afrika mashariki wanataka mafuta yao yaweyanatoka Uganda hapo
 
Kwani hata likipita bure na mwishowe bandari yetu kutumika kusafrishia tatizo liko wapi?
 
Biashara inayoongelewa kwenye bomba la mafuta Kati ya Tanzania na Uganda inaonekana Kama ya wadau wawili, ila nasikia na Mkenya akiongelewa na Mmarekani pia, hawa jamaa vipi? Ni story tu au wana chao?

Tanzania na Uganda zimegawana 50% ya share 25% kila mmoja. Hizo 50% nyingine wapo kina nani na wanachangia nini?

Tanzania imeshakubali kutoa eneo lake kwaajili ya hili bomba, imetoa pia miaka ishirini ya 'tax depreciation holiday' na VAT ya Sifuri(0).
Hao wadau wengine wenye asilimia 75% (majority) wametoa nini?

Kuna anayeweza kutuambia haya mambo yakoje tofauti na zile story za dada zetu kupata kazi ya kuuza chakula?
Kwenye hizo hamsini... Assume...

Wanaume wana 40%

Jiwe 5%

Bashite 1%

Mkapa 3%

Wengineo 2%

Una swali lingine?
 
Biashara inayoongelewa kwenye bomba la mafuta Kati ya Tanzania na Uganda inaonekana Kama ya wadau wawili, ila nasikia na Mkenya akiongelewa na Mmarekani pia, hawa jamaa vipi? Ni story tu au wana chao?

Tanzania na Uganda zimegawana 50% ya share 25% kila mmoja. Hizo 50% nyingine wapo kina nani na wanachangia nini?

Tanzania imeshakubali kutoa eneo lake kwaajili ya hili bomba, imetoa pia miaka ishirini ya 'tax depreciation holiday' na VAT ya Sifuri(0).
Hao wadau wengine wenye asilimia 75% (majority) wametoa nini?

Kuna anayeweza kutuambia haya mambo yakoje tofauti na zile story za dada zetu kupata kazi ya kuuza chakula?
Tanzania na Uganda wamegawana share za nini? Nani atajenga na kumiliki bomba?
 
Umewahi kufanya biashara yeyote?
Hata ya kuuza mandazi?

Inaelekea hata mradi wenyewe hauelewi kujifanya much know tu, sisi ni transit land na hatuna uhusiano wowote na Mafuta ya Uganda, ni kwamba ardhi na Bandari yetu ndo itatumika, na m kwa vyote viwili tutalipwa na ajira kuzalishwa kote wakati wa ujenzi na baada ya kukamilika hivyo hatuna cha kupoteza zaidi ya kufaidika tu!
 
Sababu ya kuuliza swali langu ilikuwa kujaribu kujua Kama unafahamu faida inapatikana vipi kwenye biashara au ujira kwenye kazi.
Swala la kusema sisi ni transit tu... Linakaa Kama hii ardhi inayotumika ni yako na jiwe.
Kilimanjaro kwato ya ng'ombe kwenye shamba la mtu inalipiwa elfu tano.
Usijekuta biashara mliyofanya ni ya chini kuliko Kama tungewakodisha wamasai wakapitisha ng'ombe??
Ndio sababu ya kutaka kujua tunapata nini na kwanini?
 
Hilo swali lako halina maana yoyote kwani hilo swala limeshaoongelewa sana na Serikali na hata hapa JF, unaweza hata kugoogle pia, sisi hatutoi hata shilingi ispkuwa ardhi tu hivyo hata kama wanapitisha bure bado hatujapoteza kitu kwani watatumia Bandari yetu ya Tanga kwa import&export, hiyo ni faida tosha kabisa, hayo mambo ya uchagani kwenu ya sijui kutozana mia 500 mtajuana wenyewe, sisi hayatuhusu!
 
Baba akifanya biashara ya kuuza nyumba ya familia na kwa namna yeyote akiwa hayuko katika utimamu wa akili, hiyo biashara na huo mkataba unakuwa sio halali bila kujali umejadiliwa kwenye vijiwe vingapi vya 'lisonge liende'!
Sijui utanielewa???
 
Tuna gas yetu, tena nyingi, kwa ushujaa wa kijinga, tumewakimbiza wawekezaji wameamua kuwekeza heavily kwenye gas ya Mozambique. Kwa wendawazimu wa ajabu, tunaamini tutafaidika na mafuta ya Uganda kutokana na ushuru wa kupitidha bomba!

Kwa nini hatukuweka sheria nzuri na mazingira yanayovutia uwekezaji ili tufaidike na mapato ya uchimbaji wa gas yetu?

Ni sawa na mtu una nyumba yako ya kupangisha, unawafukuza wapangaji wako ambao wangekulipa sh 1m kwa mwezi halafu kutwa nzima unatangaza kufurahia eti mwenye nyumba mwenzio ana wapangaji ambao wamekubali watakuwa wanalipa ushuru wa sh 1000 kila mwezi wa kuegesha magari yao kwenye uwanja wa nyumba yako iliyokosa wapangaji kutokana na ukorofi wako.

Back
Top Bottom