Hivi kweli swala la malawi lilikuwa ni hatari kiasi hiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kweli swala la malawi lilikuwa ni hatari kiasi hiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rodrick alexander, Aug 10, 2012.

 1. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,105
  Likes Received: 1,492
  Trophy Points: 280
  Kwa mwaka huu serikali imekuwa ikiandamwa na tuhuma nyingi kiasi cha kupoteza imani kwa wananchi tukianza pale mwezi wa nne walipotishia kumpigia waziri mkuu kura ya kutokuwa na imani,tuhuma za mawaziri kuchukua rushwa,kuvunjwa baraza la mawaziri, mgomo wa madaktari,kutekwa kwa ulimboka,mgomo wa walimu,mbunge kukamatwa na rushwa,wabunge kutuhumiwa kuchukua rushwa na wabunge kujiongezea posho maradufu wakati serikali inasema haina pesa hali hiyo imechangia wananchi wengi kupoteza imani kwa serikali na uongozi wake kuanzia rais wakati hali hiyo imepamba moto ndipo likaibuka swala la mgogoro wa mpaka na malawi.

  Naamini maadamu kulikuwa na tume ya pamoja na hasa ukizingatia juzi juzi kuna tume nyingine imeundwa kushugulikia tatizo la mto songwe kulikuwa hakuna sababu ya kulishupalia jambo hilo kitu kingine kinachotia mashaka wakati wa kusoma hotuba ya wizara ya mambo ya nje ambapo ilitegemewa serikali ingetoa msimamo wake kulikuwa na ugeni bungeni toka malawi ukiongozwa na naibu spika wa malawi.

  Kama kulikuwa na tishio la vita sidhani kama malawi wangethubutu kutuma ujumbe wao serikali wameshupalia jambo hili ili kuwasahaulisha watanzania tuhuma mbali mbali zilizokuwa zinaelekezwa juu yao na pia hata watu wengine waliokuwa wanachangia humu kusapoti msimamo wa serikali ya malawi walifanya makusudi ili mawazo yetu tuyaelekeze huko badala ya kutafakari juu ya nchi yetu kwani siamini kama mwananchi wa nchi husika naweza kutetea nchi jirani kuhusu vita na hasa swala lenyewe linapohusu mipaka
   
 2. brasy coco

  brasy coco JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 1,293
  Likes Received: 579
  Trophy Points: 280
  Hawa serikali wanaatufanya sisi Watoto tuliozaliwa leo na kutucheza shele sasa wala sisi hatudili na mambo ya Malawi tunataka kujua hatma ya Nchi yetu Tumechoka kuibiwa na Serikali ya CCM
   
 3. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hadi mwisho wa mwaka huu 2012, I bet tutashuhudia mazingaombwe ya Kutosha!
   
 4. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu mimi nadhani lilikuwa tishio dhahiri kwani ndege za Malawi zilikuwa zikiranda na makampuni ya utafiti yakiendelea na utafiti. Hii ni dharau kwa nchi yetu, japokuwa CCM wameitumia kama karata kutuliza fukuto la ndani, hata hivyo adui wa nje anatakiwa kupigwa kwanza. Naamini pamoja na udhaifu wa serikali ya CCM, jeshi letu liko imara na Malawi wanafahamu hilo otherwise wangetufanyia kama Kagame anavyowachezea Congo DRC, Hii ni njama ya kupora mipaka yetu kama alivyowahi kufanya Idd Amin
   
 5. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,342
  Trophy Points: 280
  Yes umenena mkuu!
  Ila CCM si dhaifu kama unavyofikiri.
   
Loading...