Hivi kweli soka ni mchezo maarufu tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kweli soka ni mchezo maarufu tanzania?

Discussion in 'Sports' started by Liwolo, Jun 8, 2011.

 1. L

  Liwolo Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mtizamo ambao sio timamu sana wabongo wengi tunafikiri soka ni mchezo maarufu sana,upande wa serikali ndio kabisa hakuna mipango endelevu kabisaa chukua mfano,tunawanunua makocha kwa pesa ya kutupwa kufundi mpira watu wenye miaka zaid ya 25 wakati kwa wale wanaojua soka la kimataifa mchezaji akitimiza umri huo maana yake ndio amezeeka.Bado hata hao makocha wakifika hakuna jipya tunaloliona zaid ya ule ule mpira wetu wa Anao,anao BUSARA ingekuwa kuwachukua wazawa kuwapeleka nje kwenye koz za ukocha na warudi kuimarisha kwanza soka la watoto mfano tunao kwenye nchi kama GHANA &NIGERIA kuliko kupoteza mapesa mengi kwa kuwalipa hao makocha wa nje.Tukirudi katika mfumo wa lig yetu ndio kichekesho hakuna soka la maana linalochezwa uwanjan zaid ya majigambo kwenye vyombo vya habari.Lig imekosa matangazo kitaifa na kimataifa ingawa sisi wenyewe tunajivunia utumbo huu.Ukija kwenye zawad! Masikini utatamani kulia kwan lig inachezwa zaid ya miezi 6 lakini bingwa anapata kombe na fedha isiyozid 50mil wakati huo huo mshindi mmoja wa BONGO STAR SEARCH(BSS) anapewa zaidi ya 30mil,hv kweli soka litakuwaje maarufu kwa mtizamo wetu dhaifu usio na hoja angavu na zenye mantiki.?,nadhani tunahitaji mabadiliko.
   
 2. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kwa maelezo uliyotoa hapa naona heading ingesomeka vingine, lakini kwa umaarufu, soka ni mchezo maarufu sana hapa Tz, kwa vile ndio unapendwa sana, unavuta hisia za watu, unajaza watu viwanjani, timu ikifanya vizuri mapokezi yake yanafunika vibaya mno, hata mkitofautiana kwenye siasa kwenye soka mnakuwa wamoja, wasanii wa kisiasa wanagawa mipira na jezi na ufadhili wa kimagumash ili wapate umaarufu kupitia soka, hebu jiulize jinsi gulamali, dewji(azim),virani, manji(yusuph), hata Juma Nkamia umaarufu wao unatokana na soka.

  Kasoro ulizotaja hazipunguzi umaarufu wa soka ndo maana watu wakichoshwa na soka ya bongo wanashushia maumivu ughaibuni!
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,300
  Likes Received: 22,089
  Trophy Points: 280
  serikali na viongozi wake imeweka kipaombele kwenye ule mchezo wa kuongeza kujilimbikizia mali na kuongeza umasikini kwa wanyonge
   
Loading...