Hivi kweli Serikali hii imeshindwa kweli kuwapata kina Ben Saanane, Mwandishi wa Mwananchi na waliomwaga damu ya Lissu?

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Hivi ni kweli hii serikali inayodai kupenda raia wake na kujali kila mtu bila kutazama itikadi za vyama na eneo unalotoka ina uhalisia??Ni kweli hii serikali inayojinadi kila mara kuwa "Tumtangulize Mungu" au "Tuombeane" au "Msema kweli ni mpenzi wa Mungu" inayaishi hayo inayoyasema??

Serikali inayojinasibu kuwalinda watu wake na mali zake,watu wake na usalama wao,watu wake na uhai wao inaweza kuyatenda haya mbele ya macho ya raia wake??Hebu tuwe wakweli wa nafsi hata kama tunampenda "Baba",hii kweli inachanja mbuga akilini??

Huyu Ben Saanane,kijana mdogo,mwenye mtazamo fulani tofauti yetu.Huyu ni baba wa binti mmoja,ambaye mpaka leo hajui hatma ya baba yake,huyu ni mtoto wa Mzee Rabiu Saanane,ni kaka mwenye dada zake na ni mjomba mwenye wapwa zake.Amestahili nini lililo ovu mpaka leo asipatikane?Amekosa nini juu ya ardhi hii iliyojaa ubatili na chini ya mbingu iliyojaa haki kwa walio wema na waovu?

Ni kweli,katika nchi inayodai usalama na amani kwa raia wake imekosa hata "clue" moja mbili zinazomuhusu huyu na upotevu wake?Ni kweli hata TCRA wameshindwa kufahamu hayo maeneo ya Mikocheni karibu na Maghorofa ambapo namba yake ilionekana kupatikana kwa mara ya mwisho??Hii kauli ya msema kweli ni mpenzi wa Mungu,ina uhalisia gani ndani yake?

Ni kweli tunakaa kimya juu ya uhai na pumzi ya mtu mmoja kwa kiasi hiki?Kwetu Faru John anaweza kutikisa nchi na kuundiwa tume ya kubaini kifo chake kuliko kijana mwenye ujana na ubinadamu kama walivyo vijana wetu tuliowazaa??

Umewahi kujipa dakika kumi za kuvaa viatu vya baba wa kijana huyu na kuona huzuni yake katika moyo?Mwalimu Nyerere alivaa viatu vya wazazi wa vijana "watukutu" waliomshambulia na mabango pale Chuo Kikuu Mlimani.Washauri wake waliokuwa wanajipendekeza kwa Mwalimu,walishauri adhabu "kali" sana kwa wale vijana walioongozwa na kina hayati Samuel Sitta.Mwalimu alilainisha adhabu na kuwatandika viboko na kuwapumzisha vijana nyumbani kwa muda na baadae aliwarudisha chuoni.

Tuliozika watoto ambao walitangulia mbele za haki kabla ya sisi wazazi,tunajua nini maana ya kupoteza mtoto aliyetokana na kiuno chako.Ukiuvaa uhusika wa baba wa Ben,mpika supu na ndizi katika mji wa Moshi,aliyekuwa na mategemeo ya kusaidiwa na kijana wake baada ya kumsomesha kwa muda,utavaa viatu vyake na kuamua kuandika hiki tunachokiandika.

Hivi ni kweli huko juu kwa walio na mamlaka hamguswi na hili la huyu kijana?Kwa uovu gani hasa alioifanyia nchi hii na watu wake!?Kwa kauli na maandishi yake tu ndio anastahili hili yeye na familia yake??Vyeo ni dhamana tu.

Mwandishi wa Mwananchi amechukuliwa mchana kweupe.Tena ndani ya gari lenye namba zinazoeleweka.Wamemtoa kijiweni mpaka shambani,mbele ya macho ya mkewe na rafiki zake Azory Gwanda ametoweka.Ameacha uchungu kwa mke,ndugu na familia.Kwa "intelijensia" ambayo vyombo vyetu vya usalama huiona kabla ya mikutano na maandamano,imeshindwa kabisa kuwa na "ABC" ya kujua huyu ndugu yetu alipo?Kweli sisi kama Taifa tumeamua kukaa kimya kwenye matukio kama haya kisa hayatugusi sisi wala familia zetu?

Taratibu tunaanza kuukubali utamaduni wa kutekana,kuuwana na kupigana risasi.Tunaanza kuona kawaida kubaguana na kutesana kwa sababu ya tofauti zetu za kiitikadi na kimsimamo.Huu ndio utamaduni mpya tunaoupandikiza kwa watoto na vizazi vyetu.

Tunaenda nusu ya mwaka bila wale waliodhurumu afya ya Tundu Lissu kupatikana wala hata kuhisiwa.Uchunguzi haueleweki wala kelele za kidola kukemea "roho ya kisasi" ya aina ile hazisikiki.Stahiki zake za kimatibabu ambazo ni haki yake kisheria zinapigwa danadana,halafu anatokea mtu anasema "hii nchi ni yetu sote,maendeleo hayachagui chama,si Upinzani wala CCM,tumtangulize Mungu".Hivi kwa Wakristo na wacha Mungu,kuna upendo mkubwa kama ule wa kumpenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe??

Kwenye haki huwa hakuna hisani,tukijenga utamaduni wa kupeana haki kwa hisani,ipo siku na wewe unaweza kukosa haki yako kisa umetofautiana kimtazamo na kimsimamo na yule mtu aliyepewa dhamana tu ya kutoa haki yako.

La Msingi unalopaswa kujua,cheo ni dhamana tu,cheo hakidumu wala hauendi nacho kaburini.Stahiki za huyu mtu kama mbunge hazitolewi kwa pesa ya mtu toka mfukoni,ni kodi ya Watanzania wote.Unapotumia cheo chako ambacho ni dhamana tu kukandamiza haki za wengine,ipo siku kama si wewe basi uzao wa kiuno chako utakuja kuyalipa hayo unayoyatenda.

Kuna laana na mabalaa huambatana na matendo ya mtu katika uzao wake,hata kama si yeye,wapo katika ukoo wake watakaolipwa.Kama mlishindwa kwa bunduki,hii ya pili haitawezekana.

Thamani ya uhai wa mtu ipo katika mikono ya aliyemuumba.Ukiichukua dhamana hiyo kwa niaba ya aliyemueumba,itakuandama mpaka ndani ya futi sita za udongo.Uhai na kifo,ni dhamana ya aliyevito.

Siku walipopokea jeneza la mzee fulani alipata kuwa kiongozi wa muhimili mmoja wa serikali,pale juu ya jeneza lake paliandikwa "These are the Remains of Mr...," yaani "Haya ni Mabaki ya Bwana Fulani".

Hakuwa yeye tena,bali ni mabaki ya mwili wake katika jeneza,hesabu ya matendo yake ilishafungwa.Ikatupa fundisho,kuwa licha ya kuondoka kwenye daraja la kwanza la ndege kwenda katika matibabu ambayo katika hospitali walizozijenga wao hayapo,bado mtu huyo amerudi kama mabaki tena na kuwekwa chini sehemu ya mizigo ya ndege.Huko hakuna daraja la kwanza wala la pili.

Hakuwa na thamani ya kuwekwa tena daraja la kwanza,bali katika mizigo na mabegi ya abiria.Hakupita tena kwenye korido za ukumbi wa watu maarufu,bali kwenye vibambaza vya jengo la mizigo na kupimwa kama mizigo mingine.

Huu ndio mwisho wa binadamu,iwe alikuwa na cheo cha kuamlisha majeshi yote ya nchi,iwe alikuwa na cheo cha kufukuza watu bungeni au iwe alikuwa na cheo cha kuidhinisha malipo ya tiba ya mwenzake,ipo siku atabaki kama "mabaki" na haikawii akatangulia kabla ya yule aliyemdhulumu haki yake ili kumpa mateso na kumfanya atangulie mbele za haki mapema.

Wajuzi wa "Political Economy" wanasema maendeleoo ya kiuchumi huenda sambamba na demokrasia,tunapokimbizana kuleta maendeleo tusiiache nyuma demokrasia na heshima ya "Political Pluralism"...nchi zote zilizoendelea,maendeleo na demokrasia vilienda pamoja!Viongozi wanapoonyesha kuheshimu maamuzi,uhai na maisha ya watu ndio watu wanapozidi kuonyesha imani kwa serikali.

Tusifurahie kasi ya "maendeleo" isiyoendana na demokrasia ya kweli,binadamu ana hulka ya kupenda na kukitafuta kile anachokikosa zaidi ya kile anachokipata,ndio maana kuna wanawake wanapewa kila kitu,lakini kama wananyimwa "uhuru" hata wa kuchangamana na jamii ya wanawake wenzao wanageuka "micharuko".

Uongozi bora ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya watu,mitazamo kinzani,kukosolewa na hata kukataliwa na wachache.Ivory Coast iliwahi kuwa tulivu,pengine tulivu zaidi hata ya Tanzania.
 
Ni pande zote mbili kwa maoni yangu kwani hata chadema hawataki kutoa ushirikiano wowote ule na Serikali yetu na wameshaishutumu live tena kwenye foreign media in a foreign country kwamba Serikali yetu ndiyo ilimpiga risasi Tundu Lisu na kumuuwa huyo Saanane, sasa iweje tena unailalamkia Serikali yetu kutokuchunguza wakati tayari mmeshaishutumu kuhusika?

Je, ni jibu gani ambalo Serikali yetu watakuja nalo ambalo mtalikubali kama tayari mmeshahukumu kuhusika kwake?
 
Dhaman ya uhai wa mtu ipo katika mikono ya aliyemuumba.Ukiichukua dhamana hiyo kwa niaba ya aliyemuumba,itakuandama mpaka ndani ya futi sita za udongo.Uhai na kifo,ni dhamana ya aliyevito.

Sizonje Ni mtu was ajabu sana
 
Mashairi ya kidato cha nne ya Summons kuna ushairi unaitwa Development.....

Kuna vesi inasema...

'Do you plead incapable to bring about development'?
 
lini jambazi kajichunguza nwenyewe
 
Matukio ya utekaji,uteswaji,kupigwa risasi za moto wakosoaji wa serikali,kuzikwa kwenye sandarusi na mengine yanayofanana na hayo ndiyo yule ajuza aitwaye pole pole anayaita "Tanzania mpya". Hajakosea,hakika hii ni Tanzania mpya ya watekaji,watesaji na wauwaji!
 
Watu wamepotea kwenye mazingira ya kutatanisha,,na wamechukuliwa na watu wasiojulikana..hiyo serikali itawatoa wapi??
Ila kwa wahusika ni lazima vizazi vyao vitabeba hatia hio,maana haki ya MTU kama amezulumiwa nafsi haipotei urudi kutafuna kizazi cha muhusika. Ndo maana unakuta wazazi wana uwezo lkn watoto wametoka nje ya mstari, watoto hawana baraka, ni maumivu kwa wazazi, Mara nyingi huwa wazazi walishiriki kuzulumu nafsi ya mtu,maana nafsi ya MTU aiendi bure,hivo wahusika wasubirie majibu kwenye vizazi vyao.
Kwa mujibu wa laws of nature.
 
Ilitakiwa kila anapopotea mtu Chadema basi na upande wa pili apotee mtu.
Kila anapopigwa mtu wa Chadema risasi basi na upande wa pili apigwe mtu.
Hapo tungeelewana!
Lazima kila muonevu ajue kila anapoonea basi anakosa haki ya kurudi nyumbani na kuonana na familia yake.

Hii tabia ya Chadema kulalamika tu ina athari mbaya sana!
Kwanza kabisa inafanya watu wanaoshikilia misimamo ya chama wasijisikie salama!
Pili inajenga taswira kwa jamii kuwa siasa za upinzani sio halali, hazitakiwi na ni fungu la kupoteza.

Nimeshaandika sana humu lakini watu hawaelewi!
Sasa tukipewa dhamana ya kuongoza nchi halafu watanzania wakaonewa au kuuawa si tutabaki kulalamika?

Uongozi ni dhamana ndio, na Mbowe umepewa hiyo dhamana!
Hebu mtu ndani ya chama aonyeshe kwamba Chama kinaweza kutoa amirijeshi mkuu!
 
Nenda kaangalie movie ya pembe kumwibia senga redio kisha akamshawishi senga atoe dau kubwa wamtafute mwizi wa redio kupitia kwa mganga maarufu ambaye senga ndo anamjua.
Senga anaingia line na kutoa pesa akimpa senga.
Hatimaye senga anaenda kuchukua redio kwenye shamba la miwa la senga alikoficha na kuirudisha kwa senga huku asijue senga keahamuona pembe.
Unayemlaumu ndiye chanzo cha matatizo yako.Waambie wamuachie huko aliko akiwa mzima au mfu.
Ni vema pia wale watu waendelee kukumbushwa wakatubu.
 
Watu wamepotea kwenye mazingira ya kutatanisha,,na wamechukuliwa na watu wasiojulikana..hiyo serikali itawatoa wapi??
Serikali na vyombo vyake ilijuaje hao watu ni wale wasiojulikana?!!

Serikali inayokamata na kushitaki watu kuanzia whatssap na Facebook hata kwq kupost picha tu ya jengo Le ye Ufa ndio inashinda kutambua watu na magari yao meupe yanayofanya uhalifu kama wa Lissu ama mwandishi wa Mwanannchi?!!

Vipi na wale jamaa waliomtolea Nape bastola mbele ya media na askari then wakapanda gari jeusi na kupotea nao hawajulikani?!!
 
Ni pande zote mbili kwa maoni yangu kwani hata chadema hawataki kutoa ushirikiano wowote ule na Serikali yetu na wameshaishutumu live tena kwenye foreign media in a foreign country kwamba Serikali yetu ndiyo ilimpiga risasi Tundu Lisu na kumuuwa huyo Saanane, sasa iweje tena unailalamkia Serikali yetu kutokuchunguza wakati tayari mmeshaishutumu kuhusika?

Je, ni jibu gani ambalo Serikali yetu watakuja nalo ambalo mtalikubali kama tayari mmeshahukumu kuhusika kwake?

Usiwe msahaulifu, Kwa mfano suala la Ben Saanane Chadema kupitia Tundu Lissu walitoa hadi namba za simu alizokuwa anatumiwa meseji za vitisho lakini Serikali yenu haikuchukua hatua zozote.

Tundu Lisu mwenyewe alitoa number za gari lililokuwa linamfuatilia lakini hamkuchukua hatua zozote, mnataka watoa ushirikiano gani?

Mnachofanya kinajulikana na muda ndio utakaosema.
 
ningekutukana aisee lakini naogopa ban, ushirikiano gani wanaotaka wao wa dereva, yaani .......
 
Usiwe msahaulifu, Kwa mfano suala la Ben Saanane Chadema kupitia Tundu Lissu walitoa hadi namba za simu alizokuwa anatumiwa meseji za vitisho lakini Serikali yenu haikuchukua hatua zozote.

Tundu Lisu mwenyewe alitoa number za gari lililokuwa linamfuatilia lakini hamkuchukua hatua zozote, mnataka watoa ushirikiano gani?

Mnachofanya kinajulikana na muda ndio utakaosema.

Tundu Lisu ameishutumu Serikali yetu kwenye vyombo vya Habari vya nje kwamba imehusika na kumpiga risasi na pia Serikali yetu inateka na kuuwa raia, Tundu Lisu amesema hayo, sasa mnataka nini kutoka kwa Serikali yetu?
Si mlishasema inawaua iweje leo hii mnataka Serikali inayohusika kuwaua tena ichunguze na kutafuta wahusika?
 
Ni pande zote mbili kwa maoni yangu kwani hata chadema hawataki kutoa ushirikiano wowote ule na Serikali yetu na wameshaishutumu live tena kwenye foreign media in a foreign country kwamba Serikali yetu ndiyo ilimpiga risasi Tundu Lisu na kumuuwa huyo Saanane, sasa iweje tena unailalamkia Serikali yetu kutokuchunguza wakati tayari mmeshaishutumu kuhusika?

Je, ni jibu gani ambalo Serikali yetu watakuja nalo ambalo mtalikubali kama tayari mmeshahukumu kuhusika kwake?
Ni vyema iwapate wahusika ili kuondoka na dhana kwamba serikali yetu sio iliyohusika. Ikisusia ndio wanaharibu kabisaa. Ushauri wako ndio unaitumbukiza Serikali yangu pendwa kwenye tuhuma. Najua wanao huo uwezo kabisa wakiamua lakini.
 
Back
Top Bottom