Hivi kweli reports za cag huwa zinafanyiwa kazi kweli??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kweli reports za cag huwa zinafanyiwa kazi kweli???

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by IROKOS, Apr 13, 2012.

 1. IROKOS

  IROKOS JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,193
  Likes Received: 2,626
  Trophy Points: 280
  Wakuu nilikuwa napitia moja kati ya taarifa sita za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali zilizopostiwa leo na Pasco. Nimepitia taarifa ya ukaguzi wa ufanisi za Mamlaka za uzambazaji maji mijini, matengenezo ya magari ya serikali, Mfuko wa bima ya afya (NHIF), Uvunaji wa misitu n.k na kujikuta nauliza swali hilo hapo juu kwa sababu taarifa zote nilizozipitia kwa haraka zote CAG amehitaimisha kwamba kuna matatizo makubwa, upotevu wa fedha na mambo kibao!!! Mifano michache:
  1.Mamlaka za maji mijini (UWSSAs) hupoteza karibu 50% ya maji wanayozalisha na hivyo kupata hasara ya mapato ya sh.2.5 bill kwa kila mwezi;
  2.Pamoja na records za usajili kuonyesha kuwa kuna jumla ya magari na pikipiki 65,252 ya serikali hakuna records kamili inayoonyesha ni magari mangapi yanafanya kazi na ni yapi bado yanamilikiwa na serikali, hivyo ni vigumu sana kufuatilia uengenezwaji wake. Wizara ya ujenzi (kupitia TEMESA) hawana mfumo wowote wa kusimamia utengenezaji wa magari ya serikali wala haina viwango vilivyoweka au ukaguzi maalumu kwa gereji binafsi zinazotengeneza magari ya serikali. Karakana za serikali (TEMESA) zilizotembelewa wakati wa ukaguzi ni kama zimekufa!
  3.Mfuko wa Bima ya afya (NHIF) wagonjwa batili waliopatiwa huduma za afya (2009-2010) Muhimbili walikuwa 753 (ambao walifika hospitali mara 26,725 kwa ujumla wake na hivyo NHIF ililipa 503,920/=). Na maengine mengi tu ambayo kwa ujumla wake yanaonyesha mapungufu makubwa sana ambayo kama kweli yangekuwa yanafanyiwa kazi basi matatizo mengi yangekuwa yamepatiwa ufumbuzi. Taarifa hii pia inasema CAG ameshafanya jumla ya chunguzi 11 tokea 2007 mpaka sasa na inaonekana mambo yanayoibuliwa ni haya haya, JEE TAARIFA HIZI ZINAFANYIWA KAZI KWELI??? KAMA HAZIFANYIWI KAZI NI ZA NINI SASA??
   
Loading...