Hivi kweli Rais Samia umedhamiria kuleta maendeleo nchini?

Halafu kwa uelewa wangu, nilikuwa najua ma DED angalau ni wale waajiriwa wa serikali wenye uzoefu, mfano wakuu wa idara katika halmashauri. Kwa sababu mkurugenzi anaenda kusimamia uchumi wa halmashauri. Ngoja tusubiri tuone.
Pastor masanja mkandamizaji apewe UDED wa dar,,kajitahidi sana kutetea chama.
 
Kwa namna ulivyoteua ma-DC sioni kama uko serious. Nafasi ya u-DC inashuka hadhi kila kukicha, kwa sababu inaonyesha kila mtu anaweza kitu ambacho si kweli.

DC ni mtu ambaye anatakiwa atoe dira ya maendeleo ya wilaya yake lakini kwa baadhi ya hawa uliowateua ni sawa na wapiga debe wa daladala! DC ni mtu ambaye anatakiwa kumshauri RC kudumisha amani ndani ya wilaya yake lakini hawa ni ma-DJ watakaokesha katika kumbi za starehe. DC ni mlezi wa vijana katika wilaya yake lakini hawa ni comedians.

Kwa kifupi hakuna uongozi katika wilaya, hakuna mlezi, hakuna busara uliyopeleka wilayani bali kuna washereheshaji! Tafadhali Rais Samia hebu kuwa serious kidogo wananchi tupate imani! Nalilia nchi yangu inavyoangamia! Hawa vijana wako angalau wangepewa orientation ya uongozi!

Mungu ibariki Tanzania!
hapa atakuwa analengwa Nikki wa pili na Chiponga :D
 
Dira ya maendeleo iko na DISTRICT EXECUTIVE DIRECTOR siyo DC. DC majukumu yake ni kuhamasisha utendaji kazi, kuratibu shughuli za kiserikali kama mapokezi ya viongizi, kuzuia migogoro ya kivikundi. Ni majukumu ambayo yanaweza kuwa embedded kwa DED.

DC ni nafasi iliyorithiwa kutoka mfumo wa kikoloni wa indirect rule. Katiba mya ya wananchi rasimu ya Warioba ilipendekeza nafasi kama hii kufutwa. Viongozi wa watu wanapaswa kutokana na watu wenyewe kama walivyo kwenye nchi jirani ya Kenya.

Kwangu mimi na watu makini nafasi hii imekuwa ikitumika kama shukrani kwa baadhi ya watu ambao wamemsaidia Mteuzi au Chama Tawala.

Ningeona vizuri tupaze sauti KUFUTA nafasi za ma DC kuliko kuanza kuangalia nani kapewa u- DC.
Ni sawa lakini kwa mujibu wa sheria zetu DC anaweza ku-overule maamuzi ya DED na Baraza la madiwani. DC ana nguvu ya ushawishi na maamuzi katika masuala mbalimbali ya kijamii. Hivyo kuwa na DC kilaza katika wilaya ni mzigo!
 
Mimi nimelia sana nikamkumbuka magufuli, huku tunakopelekwa mmh
Nimekusoma hapa mkuu...; halafu na hapa chini!
Mwachen mama afanye kazi , Mama 50 tena
Nikawaza..., kumbe wewe ni DC mteule?

Lakini huwa sipendi utani au unafiki kwenye mambo ya msingi kama haya.

Kwa hiyo nikaona nikupe stahiki yako: watu kama nyinyi ndio maadui wakubwa wa Tanzania kuliko hao wanaotutawala.
Siku tukifanikiwa kupata njia za kuwashughulikia nyinyi taifa letu litapona.

Baada ya hayo, nichukulie vyovyote uonavyo inafaa kwako.
 
Ni sawa lakini kwa mujibu wa sheria zetu DC anaweza ku-overule maamuzi ya DED na Baraza la madiwani. DC ana nguvu ya ushawishi na maamuzi katika masuala mbalimbali ya kijamii. Hivyo kuwa na DC kilaza katika wilaya ni mzigo!
Umeongelea nguvu ya "ushawishi", Ina maana hana nguvu "kisheria". Basi tena hakuna ulichonipinga
 
Umeongelea nguvu ya "ushawishi", Ina maana hana nguvu "kisheria". Basi tena hakuna ulichonipinga
Soma vizuri nimeandika kwa mujibu wa sheria zetu DC anaweza ku-overule maamuzi ya DED na Baraza la madiwani.
 
Soma sheria iliyoanzisha mamlaka ya halmashauri za wilaya na ile ya halmashauri za miji na majiji.
 
Acha hizo ww mkuu wa idara, watz wote wanastahiri hata waliopo private sector 😜! Tena wa private sector ndio wanafaa kuja inyoosha mifumo mibovu yenye ukiritimba ya halmashauri 😜!
Halafu kwa uelewa wangu, nilikuwa najua ma DED angalau ni wale waajiriwa wa serikali wenye uzoefu, mfano wakuu wa idara katika halmashauri. Kwa sababu mkurugenzi anaenda kusimamia uchumi wa halmashauri. Ngoja tusubiri tuone.
 
Nimekusoma hapa mkuu...; halafu na hapa chini!

Nikawaza..., kumbe wewe ni DC mteule?

Lakini huwa sipendi utani au unafiki kwenye mambo ya msingi kama haya.

Kwa hiyo nikaona nikupe stahiki yako: watu kama nyinyi ndio maadui wakubwa wa Tanzania kuliko hao wanaotutawala.
Siku tukifanikiwa kupata njia za kuwashughulikia nyinyi taifa letu litapona.

Baada ya hayo, nichukulie vyovyote uonavyo inafaa kwako.
Huyu mtu wala hujamwelewa aiseee,labda umemsoma Leo Leo.

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

55 Reactions
Reply
Back
Top Bottom