Hivi kweli mpaka sasa hakuna mwanasiasa hata mmoja aliestahili kuwajibika?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,679
149,864
Kila siku ni Wakurugenzi, Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma tu ndio wanaowajibisha ili hali waliokuwa mabosi wao (wanasiasa) hakuna hata mmoja alieguswa wala kutajwa kwa lolote mpaka sasa.

Sasa wadau, hii kweli inaingia akilini?!

Ni haki?

Hamna siasa hapa?

Binafsi nina shaka na dhamira hii ya huyu mh. katika kuchukua hatua.
 
Umeuliza swali la msingi sana,sijui anaogopa nini kuyatumbua hayo majipu badala yake anatumbua vijipu.
 
Ndio hao wakurugenzi wawataje, ikifika hatua ya kupelekwa Mahakamani nafikiri watu wataanza kujumuishwa
 
Na ukion

Na ukiona hawatajwi aanza kujiuliza juu ya hatima ya kesi/tuhuma zao.
 
Kiuhalisia ni dharau kubwa kwa mkurugenzi wa taasisi kuacha kufuata weledi na kusikiliza wanasiasa ambao wengi wao hawana utaalamu unaohusiana na shughuli za taasisi.
Ni mara chache sana watu wapo tayari kukaa pembeni wanapoona wanapelekeshwa au kulazimishwa kufanya visivyo, ndio maana wengi wanakufa na tai shingoni.
 
Rais wetu alituahidi kuwa atakula sahani moja na watendaji wa serikali ambao walikuwa hawaguswi pindi wanasiasa walipowajibika kisiasa. Sasa zamu yao
 
Na ukion

Na ukiona hawatajwi aanza kujiuliza juu ya hatima ya kesi/tuhuma zao.
Tuhuma zinazowakabili ni za kiutendaji zaidi. Wanasiasa wanategemea watendaji katika kazi zao. Watendaji ndio washauri wa wanasiasa. Kama ukiona mambo hayaendi sawa basi ujue watendaji wanapwaya
 
Kama ni hivyo mbona kila siku unamlaumu Lowassa na kumuita fisadi?
 
Hawezi wagusa hao anaogopa chama hebu cheki Mwanza si angemsimamisha na mkuu wa mkoa ni kuonea watu utadhani wanasisa wana damu ya dhahabu
 
Kama ni hivyo mbona kila siku unamlaumu Lowassa na kumuita fisadi?
Lowasa alikuwa anatoa maelekezo kwa Watendaji. Kumbuka Waziri Mkuu pamoja na kwamba ni mwanasiasa, ni Mtendaji pia. Ndo maana alikuwa anacommand kampuni ya kuchukuliwa kwenye ile sakata la Richmond. Unakumbuka vile vimemo alivyokuwa anaandika kwenda kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini?
 
Rais wetu alituahidi kuwa atakula sahani moja na watendaji wa serikali ambao walikuwa hawaguswi pindi wanasiasa walipowajibika kisiasa. Sasa zamu yao
Unajua Bavicha wana ugonjwa wa kusahau kabisa...
 
Kila siku ni Wakurugenzi, Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma tu ndio wanaowajibisha ili hali waliokuwa mabosi wao (wanasiasa) hakuna hata mmoja alieguswa wala kutajwa kwa lolote mpaka sasa.

Sasa wadau, hii kweli inaingia akilini?!

Ni haki?

Hamna siasa hapa?

Binafsi nina shaka na dhamira hii ya huyu mh. katika kuchukua hatua.

Vibaka wengi wa kisiasa tulishawpiga chini kwenye kura...mfano yule mzee wa kule kaskazini
 
wanasiasa wanawajibishwa na wananchi moja kwa moja (sanduku la kura) au bunge. umesahau juzi tumetoka kwenye uchaguzi na luwasa kawajibishwa kwasababu ya richmondii
 
Ndio hao wakurugenzi wawataje, ikifika hatua ya kupelekwa Mahakamani nafikiri watu wataanza kujumuishwa

Wawataje akina nani?!
Kwani hao mabosi ambao ni wanasiasa hawajulikani?
Hivi wewe unaamini mkurugenzi peke yake anaweza kucheza deal la Billions bila kiongozi wake wa kisekta kwenye wizara kula mgao?! Unaamini hilo?!

Ifike mahali wataalam nao wale sahani moja na wanasiasa, hawa ni tatizo sana kwa Ustawi wa bara zima la Afrika
 
Lowasa alikuwa anatoa maelekezo kwa Watendaji. Kumbuka Waziri Mkuu pamoja na kwamba ni mwanasiasa, ni Mtendaji pia. Ndo maana alikuwa anacommand kampuni ya kuchukuliwa kwenye ile sakata la Richmond. Unakumbuka vile vimemo alivyokuwa anaandika kwenda kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini?
Nani aliemzuia Lowassa kusitisha mkataba wa Richmond?Alikataa ushauri wa kuvunja mkataba huo wa maslahi ya nani?
 
Kila siku ni Wakurugenzi, Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma tu ndio wanaowajibisha ili hali waliokuwa mabosi wao (wanasiasa) hakuna hata mmoja alieguswa wala kutajwa kwa lolote mpaka sasa.

Sasa wadau, hii kweli inaingia akilini?!

Ni haki?

Hamna siasa hapa?

Binafsi nina shaka na dhamira hii ya huyu mh. katika kuchukua hatua.
Wanasiasa wanawajibishwa na wapiga kura.
 
Back
Top Bottom