Hivi kweli mpaka hapa watanzania tumeridhika na hali hii?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Hivi kweli tumeridhika na ukubwa wa madaraka ya Raisi wa nchi? Hi kweli ndio tumeridhika Rais wa nchi kkutoshtakiwa mahakamani pindi akikiuka kiapo chake cha kuilinda katiba ya nchi?

Nimegundua kua wanasiasa wengi ni maslahi tu hakuna lingine! Inakuaje kelele nyingi bungeni lakini haya hatuyakomalii kwa nguvu zote? Tunasubiri kulialia tu wakati wa uchaguzi kama watoto yatima!

Tuna idadi kubwa sana ya wawakilishi wa Wananchi bungeni Lakini hajawahi kutokea mwanasiasa wa kujitoa muhanga maisha yake kuhakikisha hiki kitu kinaondoka ka kabisa Tanzania, Alikua marehemu Mtikila japo kuna watu limwona kama chizi lakini alikua ni mpiganaji wa kweli.

Tutalia mpaka mwisho wa dunia tena kwa nchi iliyojaa wasomi wengi wa kada mbali mbali wenye uwezo mkubwa wa kuhoji haya.Zaidi kazi ya wasomi wetu ni kujipendekeza pendekeza kulialia kua hawana pa kuanzia kimaisha! Hii ni aibu kubwa kwa taifa tunalosema linaendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia.

Haya mamlaka ya mkuu wa nchi yalikua sawa wakati wa chama kimoja na sio sasa! Mkuu kutohojiwa mahakamani hata skishastaafu as if yeye ni Mungu yalikua wakati nchi inapata uhuru lakini sio sasa.

Tunadanganyana na vifungu vidogo vodogo vilivyowekwa na wa watawala kiwoga woga eti Rais anaweza kushtakiwa mahakamani! Nani kasema?
 
Inawezekana kabisa watanzania hawajaridhika lakini hamna mbadala wa CCM vyama vya upinzani Tanzania vimejaa maghumashi.
 
Sababu ya Samwel sita, kama sio yeye sasa hivi tungekuwa na katiba nzuri sana, namchukia sana mzee huyu
 
Pale bungeni au Tanzania tukiwa na wasomi wenye akiri kama ya Tundu Lisu ujue hili taifa linaelekea kwenye neema,kinyume
na hapo ni maigizo tu.Nafikiri elimu yetu ina matatizo ndio maana hatujitambui
 
Hakuna taifa la watu wanaolalamika kama la watanzania! Ningekua rais wenu ningefanya mdahalo wa kitaifa kila mtanzania atoe dukuduku lake ili muishi maisha marefu. Kuna hoja nyingine ni za msingi lakini watakuambia ''kelele za churaaa.....'''
 
Inawezekana kabisa watanzania hawajaridhika lakini hamna mbadala wa CCM vyama vya upinzani Tanzania vimejaa maghumashi.
Sasa wewe mkuu Ritz Mwana CCM kabisa huamini kwamba kazi ya kutetea Wananchi hata CCM wanaweza mpaka wapinzani nimekudharau sana! Hongera kwa kutambua kua CCM hawawezi kutambua matatizo watanzania.
 
Hakuna taifa la watu wanaolalamika kama la watanzania! Ningekua rais wenu ningefanya mdahalo wa kitaifa kila mtanzania atoe dukuduku lake ili muishi maisha marefu. Kuna hoja nyingine ni za msingi lakini watakuambia ''kelele za churaaa.....'''
Kila kitu kisichokua na maslahi huchukuliwa kama mzaha tu!
 
Sasa wewe mkuu Ritz Mwana CCM kabisa huamini kwamba kazi ya kutetea Wananchi hata CCM wanaweza mpaka wapinzani nimekudharau sana! Hongera kwa kutambua kua CCM hawawezi kutambua matatizo watanzania.
Nani alikuambia mimi nipo hapa JF kutafuta kuheshimiwa wewe endelea kunidharau ndivyo navyopenda tena usijaribu kuniheshimu sawa.
 
Jaribu sana kureview unachokianfika!
 
K
Hivi kweli tumeridhika na ukubwa wa madaraka ya Raisi wa nchi? Hi kweli ndio tumeridhika Rais wa nchi kkutoshtakiwa mahakamani pindi akikiuka kiapo chake cha kuilinda katiba ya nchi?

Nimegundua kua wanasiasa wengi ni maslahi tu hakuna lingine! Inakuaje kelele nyingi bungeni lakini haya hatuyakomalii kwa nguvu zote? Tunasubiri kulialia tu wakati wa uchaguzi kama watoto yatima!

Tuna idadi kubwa sana ya wawakilishi wa Wananchi bungeni Lakini hajawahi kutokea mwanasiasa wa kujitoa muhanga maisha yake kuhakikisha hiki kitu kinaondoka ka kabisa Tanzania, Alikua marehemu Mtikila japo kuna watu limwona kama chizi lakini alikua ni mpiganaji wa kweli.

Tutalia mpaka mwisho wa dunia tena kwa nchi iliyojaa wasomi wengi wa kada mbali mbali wenye uwezo mkubwa wa kuhoji haya.Zaidi kazi ya wasomi wetu ni kujipendekeza pendekeza kulialia kua hawana pa kuanzia kimaisha! Hii ni aibu kubwa kwa taifa tunalosema linaendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia.

Haya mamlaka ya mkuu wa nchi yalikua sawa wakati wa chama kimoja na sio sasa! Mkuu kutohojiwa mahakamani hata skishastaafu as if yeye ni Mungu yalikua wakati nchi inapata uhuru lakini sio sasa.

Tunadanganyana na vifungu vidogo vodogo vilivyowekwa na wa watawala kiwoga woga eti Rais anaweza kushtakiwa mahakamani! Nani kasema?
Kwenye bunge la katiba walijipendekeza sasa akina Kange wanaisoma namba.
 
Back
Top Bottom