Hivi kweli mnyama Dragon anayetema moto alikuwepo duniani?

Series ya Game of Thrones yule mdada anatumia Dragoni kama silaha kuwateketeza adui zake, pengine ya madude yamewahi kuwepo.
 
Hakuna ni wa kufikirika kama zimwi. Nani keshawahi kumwona zimwi au sheitwani? Wote ni viumbe wa kufikirika na kiimani kama Mungu na malaika. Huwezi kuwaona katika umbo la kuonekana.
 
AFAIK hamna ushahidi kwamba ni kweli yupo au aliwahi kuwepo.

Hivi kwa sifa zake anaonekana kama "reptilia"? Sio mammalia?
Walikuwa wanataga. Wanakula nyama, wanapaa angani na wanatema moto.

Hakuna hata ushahidi wa mabaki ya mifupa.
Hizi hadithi twaweza sema ni hisia na uzushi wa watu.🚮
Ila movie zake huwa nazipenda.
 
Kama kuna samaki anaumeme itashindikana nini kwa dragons
Sawa kwani kila kiumbe kina Atoms kwenye miili yao, na ndani ya atoms Kuna Election, Pruton na Neutrons.. Kuna baadhi ya wanyama Kama huyu samaki electric eel anauwezo wa kucontrol sensitivity ya electrons zake, Hadi kuproduce volts 600 kwa ajili ya defense mechanism, hii yote kibiological proved, lakini sio Moto... Hata huyo samaki anaye generate umeme ukimweka kwenye Moto anakufa.
 
Walikuwa wanataga. Wanakula nyama, wanapaa angani na wanatema moto.

Hakuna hata ushahidi wa mabaki ya mifupa.
Hizi hadithi twaweza sema ni hisia na uzushi wa watu.🚮
Ila movie zake huwa nazipenda.
Kama movie gani na mimi niangalie?
Mimi nimeangalia tu Merlin.
 
aya mambo yapo mengi mengi ambayo yanaaminika yalikuwepo uko zamani. binafsi naona kama yalikuwepo lakin ndo hayana mtiririko mzuri wa stori na background zake..
tukiachilia mbali ayo ma dragon kuna mengine kama werewolf, vampires, mermaids na vingine hivi vinanitatizaga sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom