Hivi kweli matrekta ndicho kipaumbele cha kila wilaya ili kufanikisha kilimo kwanza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kweli matrekta ndicho kipaumbele cha kila wilaya ili kufanikisha kilimo kwanza?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Feb 28, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ijumaa nilisikitishwa na taarifa ya Radio One kuwa serikali imezionya halmashauri za wilaya ambazo hazitajumuisha ununuzi wa matrekta kwenye bajeti zake za 2011/2012 kuwa bajeti zake hazitapitishwa na serikali.

  Kwa maana nyingine ni kuwa halmashauri zitakuwa zikishindana kununua matrekta ili kusudi kuwalidhisha "wakubwa" kwani kutonunua trekta ni kutokuunga mkono sera ya kilimo kwanza.

  Kwa maoni yangu, matrekta siyo kipaumbele cha kila wilaya. Angalau nina uhakika na mikoa ya Shinyanga, Mwanza, na Mara kwa kiwango kikubwa matrekta siyo kipaumbele namba moja kwani wanatumia plau za kukokotwa na ng'ombe/punda na wanalima kwa kiwango kikubwa bila kuvuna kadri ya jitihada zao kwa sababu hakuna uhakika wa mvua, nadhani kilimo kwanza ingekuwa na maana zaidi kwa wakulima hawa kama wangejengewa mabwawa na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji badala ya kununuliwa matrekta.

  Kuzilazimisha kila wilaya zinunue matrekta siyo kuwakomboa watanzania masikini bali ni kuwanufaisha watengenezaji wa matrekta haya pamoja na mawakala wao. Umefika wakati sasa viongozi wetu watusaidie kupinga sera zinazolenga kuwanufaisha wachache na kuwaacha walio wengi wakitweta katika umasikini uliokithiri.

  Ifike mahali sasa wananchi ndio waamue nini wanataka badala ya wanasiasa kuja na kauli mbiu zisizokuwa na kichwa wala miguu ambazo zina malengo ya kuwanyonya watanzania badala ya kuwasaidia.. Kwangu mimi RUZUKU inayotolewa kwa matrekta yatakayouzwa kwenye wilaya ambazo matrekta siyo kipaumbele cha kwanza ni UFISADI
   
 2. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Viongozi wetu kwa kushirikiana na wanaojiita wasomi bila elimu ndo wametufikisha hapa. Wanakurupuka kwa kutojua ama kwa kujua kuwa watanzania wote tuko kama misukule tu! Ni jambo la kushangaza kuona mtu anatilia mkazo power tiller wakati chaqnzo cha umasikini wa kilimo na mkulima ni ukosefu wa soko la uhakkika.

  Hivi leo ni maeneo mangapi tanzania kwamfano matunda yanaozea mashambani? Je hakuna maeneo Tanzania ambako kuna mchele unauzwa kwa bei ndogo tu?

  Nadhani haka ni kaufisadi kanakopigiwa debe nasi pasipokujua tumeingia mkenge!

  Leo hii wange weka so la maana kwa mazo yote aidha kwa kutafuta wanunuzi kutoka nje moja kwa moja kila mtu angelima na kununa trector mwenyewe.

  Lakini ni wakulima wangapi wanaweza kuendesha power tiller? Kununua fuel? Kulipa dereva? Kulinunua....

  Huu ni USHENZI TU
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yaani hizi power tillers na tractors zinazopigiwa debe ni mradi wa kifisadi ambao kwa bahati mbaya tumepumbazwa kuupigia makofi. Kama kweli kulikuwa na nia ya kweli kuondoa umasikini wa mkulima, serikali ingeangalia changamoto ya kila kanda/mkoa/wilaya/kata/kijiji na kuzitatua kuliko kuja na sera za jumla jumla kwamba kila wilaya lazima iweke bajeti ya kununua matrekta ndipo waidhinishiwe bajeti zao... Huu ni ufisadi
   
Loading...