Hivi kweli kuna watu wanapiga hela online? Mimi naona kama uzushi tu!

Kipindi cha mwaka 2014 hadi 2015 kikweli ilikuwa kipindi kizuri wakati huo nafanya google adsense hizi $150 hadi $300 zimenivusha sana nilikuwa na blog yangu so kuna trick tulikuwa tunapeana lakini account sometimes zilikuwa zinafungwa, washkaji wengine walikuwa wanafika hadi $1000 kwa mwezi, siku nilipoenda kutoa pesa pale bank ya posta kwa mara ya kwanza kupitia Western Union hapo posta maeneo ya posta Dar sikuamini macho yangu, so online kuna pesa sio uongo lakini yakupasa kuwa makini.
Mkuu bado una blog
 
Habari wakuu

Maisha kwa sasa yanaenda kasi sana, Sisi vijana katika harakati za kutafuta pesa tunakutana na changamoto nyingi sana ,sasa kuna hii njia inaitwa "kupiga hela online ,ukiwa na simu yako na bando " Mimi nimeshafanya uchunguzi sana online businesses wanazosema ni zipi hizo au ni hizi ...

Cryptocurrency (sarafu za kidigitali)..

Forex ..

Betting ..

Nyingine ni network marketing ,huku utakutana na website zinatokea na kucollapse watu wanapigwa hela ,ila kutwa status kupost eti wanapiga hela eg ,pamafund ,smarthela ,global alliance ,qnet ,forever living ....

Kuna mengine mengi yanaibuka na kutoweka kwa kweli mpaka nabaki mdomo wazi na watu wanaweka hela huko ,wanapigwa ,ila ni full kujipa moyo et wanapiga hela ,wanasema wanapiga hela wakiwa wamelala kitandani ....

Hawa watu wa online wanawaona wauza mihogo ,machinga ,wauza migahawa ,wauza matunda ,chips ,washona viatu ,wapiga debe ,....hao wote wanawaona kama hawana akili ya kutafuta hela ,ila wao ndio wanajua hahaaaaaa....

Kusema kweli kama online business watu wanazosema ndio hizo hapo juu ,sina budi kusema kuwa ,watu wanaofanya hayo mavitu ni wavivu wa kufikili na "HAWATAKUJA KUFANIKIWA MPAKA MWISHO WA DUNIA"...

Yaani wanapigwa pesa mpaka akili ziwakae sawa, ..

Hakuna pesa za bure online, Fanya kazi kwa bidii, jitume, ndio njia ya kupata pesa ..

Forex ingekuwa biashara, serikali ingechukua $100,000 ikawaintrade na kutengeneza pesa ,...

Sarafu za kidigital zingekuwaa deal, hakuna tajiri ambaye angepoteza pesa kufungua kiwanda ,kulipa wafanya kazi, kodi, aridhi, na mabilion ya pesa wakati angeweza kununua hizo sarafu ..

Mh Raisi naamini atashauriwa vizur kuhusu hizo sarafu ..

Vijana tokeni nje, mkafanye kazi, ardhi ipo, mashamba yapo, mbegu zipo, hizo smart phone zinawadanganya, hakuna pesa utaingiza umelala kitandani ....

Uzi tayari
unawazungumziaje wakina ontario , elikana fx , kina john jackson succes, mkuu mona washkaji wako vizuri na walikuja hapa bongo kupiga lecture halafu kuna wale wanaoitwa 255millionaire forex wao mbona wameweza?
 
Screenshot na loss mkuu ...

Mbona unatuaminisha unapigaa hela ...

Hakuna kitu sijui kuhus forex..

Lazima upigwe tu whether you like or not ...

Yaani huwa ndio mlivo ,kupiga picha profit ,huku loss zipo chini ya carpet
Duu. Kwa hiyo mkuu unajua kila kitu kuhusu forex? We ni noma. HONGERA ZAKO
 
Nilikutana na mshikaji mmoja kazini akaniletea hizi stori. Ati Kaka yake anafanya onlone forex. Kwamba nikimpa milioni 3, nitakuwa napewa faida ya laki 5 kila mwezi na nitakapoamua kuchukua mtaji wangu nitapewa muda wowote. Akaongeza kwa kusema hata Mke wake kaacha kazi maana anaingiza karibu mil 1 kila mwezi so kaona vikazi vya lako tatu anajichosha tu.

Nikamwangalia mtu mwenyewe anayenishawishi na hali yake ya maisha nikampotezea. Baada ya miezi kama mitatu akanijia nimuuzie gari yangu ati kaipenda. Tukakubaliana bei. Aisee kumbe jamaa tapeli tu hana iasue ya maana mjini. Pesa iliyobaki kwenye mayzo ya gari 1.5M alinizungusha mwaka mzima.

Hizo online bussness ni kazi za wavivu.
Kazi za kitapeli ndio kazi za wavivu. Hzo forex na affiliate marketing zina utapeli mwingi. Online pesa ipo ila inahitaji dedication na skills. Sio kulala na kutengeza pesa.

Kma unaona ni kazi rahisi tu jaribu kuchukua gig ya kutengeneza Mobile app for Android & iOS kwa $1500 na dedline ya ndani ya mwezi alafu uone kma utatoboa kma ni kazi ya wavivu. Ila wapo watu wanafanya hzo kazi online za kihalali na wanapata hela vizuri tu. Sio kila hela online ni rahisi. Zilizo rahisi ndio utapeli.

Tatzo tunategemea kuingia tu kwenye haya mambo leo na kesho kutengeneza mahela. Hyo kitu haipo. Hata kwenye forex, affiliate marketing na Bitcoin kuna watu wanaotapeli wenzao na ndio wavivu. Ila kuna watu wanaozielewa vizuri ndio wanapiga hela.
 
Habari wakuu

Maisha kwa sasa yanaenda kasi sana, Sisi vijana katika harakati za kutafuta pesa tunakutana na changamoto nyingi sana ,sasa kuna hii njia inaitwa "kupiga hela online ,ukiwa na simu yako na bando " Mimi nimeshafanya uchunguzi sana online businesses wanazosema ni zipi hizo au ni hizi ...

Cryptocurrency (sarafu za kidigitali)..

Forex ..

Betting ..

Nyingine ni network marketing ,huku utakutana na website zinatokea na kucollapse watu wanapigwa hela ,ila kutwa status kupost eti wanapiga hela eg ,pamafund ,smarthela ,global alliance ,qnet ,forever living ....

Kuna mengine mengi yanaibuka na kutoweka kwa kweli mpaka nabaki mdomo wazi na watu wanaweka hela huko ,wanapigwa ,ila ni full kujipa moyo et wanapiga hela ,wanasema wanapiga hela wakiwa wamelala kitandani ....

Hawa watu wa online wanawaona wauza mihogo ,machinga ,wauza migahawa ,wauza matunda ,chips ,washona viatu ,wapiga debe ,....hao wote wanawaona kama hawana akili ya kutafuta hela ,ila wao ndio wanajua hahaaaaaa....

Kusema kweli kama online business watu wanazosema ndio hizo hapo juu ,sina budi kusema kuwa ,watu wanaofanya hayo mavitu ni wavivu wa kufikili na "HAWATAKUJA KUFANIKIWA MPAKA MWISHO WA DUNIA"...

Yaani wanapigwa pesa mpaka akili ziwakae sawa, ..

Hakuna pesa za bure online, Fanya kazi kwa bidii, jitume, ndio njia ya kupata pesa ..

Forex ingekuwa biashara, serikali ingechukua $100,000 ikawaintrade na kutengeneza pesa ,...

Sarafu za kidigital zingekuwaa deal, hakuna tajiri ambaye angepoteza pesa kufungua kiwanda ,kulipa wafanya kazi, kodi, aridhi, na mabilion ya pesa wakati angeweza kununua hizo sarafu ..

Mh Raisi naamini atashauriwa vizur kuhusu hizo sarafu ..

Vijana tokeni nje, mkafanye kazi, ardhi ipo, mashamba yapo, mbegu zipo, hizo smart phone zinawadanganya, hakuna pesa utaingiza umelala kitandani ....

Uzi tayari
Kuna best yangu mdada kanambia habari hizi jpili i just brushed her away, it sounded with too much of yanga-sliperly i mean utopoloz
 
Yaan ww jamaa ilibid uulize jinsi ya kupata pesa kwenye online investment. Sio unakuja kutuambia eti huwezi tajiri, nakuhakikishia mkuu ww huna Elimu yoyote juu ya hizi issue trust me Kuna watu wanatengeneza Hadi Million 2 per day via fx. Ni vile tu watu hawana Elimu juu ya sehem sahihi ya kuinvest ndomaana wanapigwa. Lakn Kuna wanaume hawali kwa jasho kabisaa kisa hizi business.
Mze muache tuu😆 maana hat ukodishe spika hatakuelewaa!!
 
Screenshot na loss mkuu ...

Mbona unatuaminisha unapigaa hela ...

Hakuna kitu sijui kuhus forex..

Lazima upigwe tu whether you like or not ...

Yaani huwa ndio mlivo ,kupiga picha profit ,huku loss zipo chini ya carpet
Loss zipo hatukataii, Ila Kuna money management labd we ulikua hujuii kufany hii kitu vzurii
 
Information is the single greatest asset in this era,a friend of mine who is Bible scholar often says,"without knowledge my people will perish".Today I think many people are perishing they are without knowledge about money
-Information is the single greatest asset in this era which you can use it to achieve your wildest dream.....
 
yawezekana ni akili yako au elimu uliyonayo hukuwahi kujifunza IT na related courses ata kidogo now dunia inaenda kasi sana kwa wenzetu digital jobs ni ishu sana yaan ni hot cakes kabisa..
kenya kuna mpaka ATM ya BITCOIN huko kwa wenzetu ndio zimejaa kila mahali sasa ukisema cryptocurrency ni scam cjui kama umeongea baada ya kufanya research hiv unaijua YFI ni nn??

watu wameinvest billions of USD kwenye kutengeneza hzo crypto currency alaf mTZ fulan hv unazi underrate .
alaf ukisikia kujiajiri digital kuna uwanja mpana sana mfano:
-Direct jobs kama upwork, freelance, fiverr etc.

- Affiliate jobs (kuuza vitu vya watu na kupata commision) hii weng wanaifanya sana ata kariakoo utofaut ni kuwa ukifanya online unaonekana ni utapeli but ukichukua nguo kwa mking kariakoo na uuze upewe 3000 kwa kila nguo utakayouza kariakoo unaonekan ni sawa... shame!!!

  • Blogging, vlogging etc
  • Dropshipping (hii ni sawa na affiliate tu)
  • kuuza vitu vyako online kama vitabu, nyimbo, vitu vya kushikika kama unavyoona ebay, aliexpress, amazon nk.
  • Forex exchange, Cryptocurrency (buying and holding then selling or trading). Hii inahitaji ujifunze sana ili atleast uweze kuona matunda ata kidogo.
  • Hosting website and domain selling (tech professionals mostly) unakuwa reseller na unaanza biashara kama vle una server yako.

- Create a system ambayo inaweza kutatua matatizo ya watu (creativity inahitajika)

- Utaleli kama kufungua HIYP programs kama hzo D9, pamafunds, smarthela ukiwa mjanja utatoboa kieahisi na unatakiwa uwe na capital kidogo.

NB: Usilinganishe online business na kilimo ndugu, agriculture ni series mpaka uje upate pesa inahitaji uvumilivu na unaweza ukaweka 5M ardhin na ukaikosa yote.. naongea coz nmepitia na bado some amount nawekaga kwenye mpunga ili mrad tu usije ukaanmbiwa unauza madawa ya kulevya ukiulizwa unasema nalima.

HZO Pamafunds and like zinalipa sana tena sana ila ujue muda wa kuingia kuna system niliweka $300 ikiwa una cku 3 tangu ianze ilivyofika miez mi3 uwez amini nilitengeneza kama $ 3000 na capital yang nikavuta nikaacha mwez wa 5 wakafunga so lazma ujue muda wa kuingia na kutoka kama DECI vle na nmejenga kwa pesa za ONLINE so ukiniambia huwez kutoka nitakuona CHIZI kwangu ila kila mmoja abaki na ANACHOKIAMNI
Pamafinds iko vipi sijaipataa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
online kuna watu wanapiga hela kaka kuna watu wana page za umbea tu kama kina Carry mastory na ndio zinawaweka Mjini kazi yao ni kushinda instagram na kutafuta habari za umbea tu wanapiga hela kupitia matangazo, pia kuna watu wanapiga hela kupitia kufanya udalali tu wa vitu au kuuza vitu vyao wao wanakuwa kama Link kati ya muuzaji na mnunuzi lakini wanapiga hela mkuu, Tatzo hapo linakuja katika Mindset Ni kwamba wengi wanaoingia katika Forex hawafanyi self learning ya kutosha Kwanza na wanaishia kuwasikiliza Mabroker wanaojiita Nyangumi wa Forex na kuishia kupigwa, Forex ile ni biashara kama zingine lakini inahitaji Kusoma kwa kipindi kirefu na kuielewa sana ndipo utaanza kuona matunda na nikwambie tu chunguza kwa makini watu wanaojifanya Kupiga hela kupitia Forex ndio wanaongoza Kupigwa vitu vizito.

Yote kwa yote Pesa sio rahisi, unahitaji sacrifice za kutosha , sleepless nights na uwe Fully committed na unachofanya
 
Habari wakuu

Maisha kwa sasa yanaenda kasi sana, Sisi vijana katika harakati za kutafuta pesa tunakutana na changamoto nyingi sana ,sasa kuna hii njia inaitwa "kupiga hela online ,ukiwa na simu yako na bando " Mimi nimeshafanya uchunguzi sana online businesses wanazosema ni zipi hizo au ni hizi ...

Cryptocurrency (sarafu za kidigitali)..

Forex ..

Betting ..

Nyingine ni network marketing ,huku utakutana na website zinatokea na kucollapse watu wanapigwa hela ,ila kutwa status kupost eti wanapiga hela eg ,pamafund ,smarthela ,global alliance ,qnet ,forever living ....

Kuna mengine mengi yanaibuka na kutoweka kwa kweli mpaka nabaki mdomo wazi na watu wanaweka hela huko ,wanapigwa ,ila ni full kujipa moyo et wanapiga hela ,wanasema wanapiga hela wakiwa wamelala kitandani ....

Hawa watu wa online wanawaona wauza mihogo ,machinga ,wauza migahawa ,wauza matunda ,chips ,washona viatu ,wapiga debe ,....hao wote wanawaona kama hawana akili ya kutafuta hela ,ila wao ndio wanajua hahaaaaaa....

Kusema kweli kama online business watu wanazosema ndio hizo hapo juu ,sina budi kusema kuwa ,watu wanaofanya hayo mavitu ni wavivu wa kufikili na "HAWATAKUJA KUFANIKIWA MPAKA MWISHO WA DUNIA"...

Yaani wanapigwa pesa mpaka akili ziwakae sawa, ..

Hakuna pesa za bure online, Fanya kazi kwa bidii, jitume, ndio njia ya kupata pesa ..

Forex ingekuwa biashara, serikali ingechukua $100,000 ikawaintrade na kutengeneza pesa ,...

Sarafu za kidigital zingekuwaa deal, hakuna tajiri ambaye angepoteza pesa kufungua kiwanda ,kulipa wafanya kazi, kodi, aridhi, na mabilion ya pesa wakati angeweza kununua hizo sarafu ..

Mh Raisi naamini atashauriwa vizur kuhusu hizo sarafu ..

Vijana tokeni nje, mkafanye kazi, ardhi ipo, mashamba yapo, mbegu zipo, hizo smart phone zinawadanganya, hakuna pesa utaingiza umelala kitandani ....

Uzi tayari
Njia za kupata pesa online ni ngumu sana kuliko kutumia njia za kujishughulisha kawaida,
Kijana atashughulika na biashara zake atakua na maendeleo makubwa sana huyu wa online kila siku anapoteza muda kwenye bahati na sibu
 
Kupata hela online hakupaswi kuchukua muda wako mwingi wa kutafuta pesa kwa njia za kawaida, inapaswa uwe muda wako wa mapumziko. Kama una mshahara wa laki moja, hakikisha hautumii zaidi ya elfu tano kwenye uwekezaji au utafutaji pesa mtandaoni.
 
Habari,
Video Subtittling ni moja Soft Skills ambayo inahitajika sana katika majukwaa ya kazi za mtandaoni (Freelancing Platforms), kwa anayehitaji kuanza Skills hii ya video Subtittling nimeandaa training fupi na rahisi Zaidi kuelewa.
images (92).jpeg

Mafunzo utalipia 20,000 TZS pesa ambayo ukiipata Skills hii utaweza kuipata ukifanya video ya lisaa limoja tu Upwork, au kwenye Agency.

Kutokana na Tangazo langu la mwanzo baadhi ya wadau waliomba Training iwe online maana hawatakuwa na muda, nimejaribu kuandaa lessons kupitia Telegramu Group nimejitahidi kuelezea kwa urahisi sana na kwa Kiswahili.

WhatsApp Group
Screenshot_20220608-062937.png

Lesson zipo mbili
1) Kuweka Subtittles kwenye video
2) Kusevu Subtittles kwenye video (Burning)

Nimeelekeza Software Tools ambazo unatakiwa kuwa nazo na jinsi zinavyofanya kazi.

Lesson 01 (Outlines)
*Jinsi ya kuweka video kwenye program
*Jinsi ya kuandika Subtittles
*Jinsi ya kuediti Subtittles (Font & Location)
*Jinsi ya kuseti muda (Start & End time)
*Work concistency

Lesson 02:
Baada ya kutengeneza Subtittle yetu tutaangalia jinsi ya kuiunganish video na Subtittles kwa kutumia Software tool husika.

Training yote nimeshaiandaa kwenye TELEGRAM GROUP mafunzo haya ya Skills hii ya Video Subtittling ni 20,000 Tzs tu ukipitia maelekezo na lessons zote utakuwa na uwezo wa kuweka subtitle kwenye video yeyote Duniani iwe Nyimbo, movie, iwe slow iwe speed.

NI PM FOR IT
 
Njia za kupata pesa online ni ngumu sana kuliko kutumia njia za kujishughulisha kawaida,
Kijana atashughulika na biashara zake atakua na maendeleo makubwa sana huyu wa online kila siku anapoteza muda kwenye bahati na sibu
Offline unahitaji kuwa na mtaji
 
Back
Top Bottom