Hivi kweli kuna wataalamu wa IT Tanzania?

foreign er

Member
Jul 19, 2016
81
125
Japo wapo ila sio sana hata mazingira haiwasapoti kivile tunahitaji jitihada zaidi has a ukizingatia kila kitu ni technology, wenzetu wako mbali yaani unakuta dogo mdogo tayari ni software engineer,web developet,app developer na hacker mzuri tu.
Kama unamtoto wako anza kumnoa fresh demand ya hawa watu inahitajika sana hasa kwenye military, political and industrial espionage etc.
I hope WWWIII Itategemea sana IT
Fact... Hasa hapo kwenye WWIII..... haitakuwa ya mabomu na marisasi!!..

Sent using POSTA
 
foreign er

Member
Jul 19, 2016
81
125
Wapo..... Ila ni uthubutu na dhana za kutaka kuajiriwa... Ndo kunawaficha ila wpo wengi sana!....

Sent using POSTA
 
sjosh4

JF-Expert Member
Apr 10, 2020
547
500
Watu wapo, shida ya IT bongo sio wanafunzi tu. Tatizo linaanzia kwenye mitaala na wizara ya elimu kwa ujumla.
Limited course,
Pia wizara kuna vitu kama vile hawataki vitu vifundishwe
 
MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
18,710
2,000
Hapa nachangia bila kuweka utaifa wala nini, mimi Mkenya hapa ila nimefanya miradi ya kutengeneza systems Tanzania na kwa ushirikiano wa wataalam wa Kitanzania. Nilichokiona Tanzania, na pia kipo kwa baadhi ya Wakenya huku ni kwamba wateja wa Tanzania hawadhamini kabisa wataalam wao. Unakuta mtu yuko radhi kulipa mhindi dollars za kiajabu ila ikitokea hiyo hiyo kazi inapewa Mtanzania, anashusha bei balaa kishenzi.
Nililiona sana hilo, kwamba mnapo andaa proposal ya kuomba mradi halafu humo kwenye majina ya timu mnayokusudia kuwahusisha kufanya hiyo kazi mtaje wazungu na wageni wengine na muorodheshe sifa zao za shahada ya uzamili/masters yaani mnasklizwa faster, ila mradi unaweza ukaishia kufanywa na vijana wazawa maana wale wazungu watakuja na kuboronga, wanapiga piga kwa kasi na kujiondokea kwa ubabaishaji mwingi, mnabaki mkihangaika.
Kunao wageni tuligombana nao na sikuwalipa hela yote, ilbidi mradi tuutekeleze wenyewe from scratch.

Mkiwa na desturi ya kudhamini wataalam wenu, na kuwalipa vizuri mbona watajituma tu, hamna kikubwa kwenye IT, cha msingi ni kukeshehea haya mavitu na kujifunza kila siku, lakini kama unalipa hela kiduchu, nitakuja na kutupiamo frameworks kama Yii au Laravel na kujiondokea bila kujali full system design and architecture.
 
Akili_nyingi

Member
Oct 21, 2019
9
45

Umesema vizuri sana MK254
Watu wapo wenye skills vzuri tu ila Industry haiwapi wazawa thamani wanayostahili.
Unakuta upo kwenye kampuni nafasi inatokea unanyimwa anakuja ngozi nyeupe anapewa hyo nafasi na Bado wewe ndio unatakiwa kumtrain kazi halafu huyo ndo anakua boss wako.
Hili jambo lina discourage sana kugrow.
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
9,641
2,000
Nikili kuwa mimi ni mkeleketwa ama mdau mkubwa sana wa IT na teknolojia kwa ujumla

Leo nimekabiliana na mdau mmoja akikandia sana tasnia hii hasa hapa nchini kwa madai kuwa hakuna wataalamu na mifumo mingi hata ya serikali kama vile ule wa malipo umeundwa na wazungu je ni kweli? Kama ipo mifumo iliyoundwa na watanzania ni ipi hiyo na ni akina nani hao walioiunda
Naomba kuwasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Si kwei mfumo wa malipo wa serikali umeundwa na vijana wa kitanzania na ni waajiriwa wa hazina
 
rodian

JF-Expert Member
Feb 23, 2016
231
500
Tupo,mifumo mingi ya serikali imetengenezwa na watanzania,ukitaka kujua I.T wa Tanzania wapo ingia kwenye mtandao wa gethub na n.k uone mifumo waliyotengeneza na wanaiuza Kama ukihitaji.
 
Unicorn

JF-Expert Member
May 30, 2020
370
500
Watu wapo nilishashuhudia watu wakifanya mabalaa acha hapa hapa bongo sema wengi hawataki kuajiliwa..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom