Hivi kweli kuna Mtanzania mwenye akili zake timamu anaweza kuichagua tena CCM, kwa Lipi?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,

Declaration of interest, mimi pia ni mwanachama wa chama cha siasa!.

zikiwa zimabaki siku 14 tufanye uchaguzi wetu, naomba kuuliza, hivi kweli kuna Mtanzania, mwenye akili zake timamu, anayefahamu maana halisi ya maendeleo, tangu tulipopata uhuru, tulikuwa na rasilimali gani, tungepaswa kuwa wapi, na kulinganisha na hapa tulipo sasa, halafu ukaelezwa sababu ya sisi Tanzania kuwa hapa tulipo, ni CCM, then hivi kuna Mtanzania kweli, mwenye akili zake timamu, bado angeichagua CCM hivi ilivyo kama mgombea wake angekuwa sio JPM?.

Hili ni swali tuu!.


Mimi si miongoni mwa wale wanaodai CCM haijafanya kitu, no!, CCM imefanya mengi, makubwa, mazuri, but it is not enough!, Tanzania tuko hapa tulipo, kwa sababu kuna things CCM should have done, but it didn't, as a result, ndio tuko hapa tulipo!, ila sasa CCM imepata mtu, kwa kumsikiliza Magufuli, you can see his genuinity to change things for the better, tatizo la nchi hii lilikuwa ni CCM, na dawa ya kulitibu ni CCM!. Sasa dawa imepatikana na soon matibabu yataanza.

Hivyo wale wote wenye ufahamu na uelewa wa Tanzania tumetoka wapi, tunakwenda wapi na tulipaswa kuwa wapi, naamini hakuna hata mmoja anaweza kuichagua tena CCM, kama mgombea wake asingekuwa JPM, unless yuko kwenye moja ya makundi haya.

  1. Wana CCM wenyewe, ambao CCM ni chama chao, pamoja na madhaifu yote ya CCM ya hapa na pale, Watanzania bado wanaipenda CCM kwa dhati na ili kuonyesha upendo wa kweli kwa CCM, Watanzania wataichagua CCM, na kuipatia ushindi wa kishindo, despite all the odds!.
  2. Wako wana CCM waliojiunga na CCM sio kwa sababu tuu wanaipenda sana CCM, bali wamejiunga CCM kwasababu CCM ndicho chama pekee nchini Tanzania chenye fursa za kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli, hivyo wamejiunga CCM ili kuunganisha nguvu za kuleta maendeleo, hawa wataendelea kuichagua tuu CCM ili kulinda maendeleo yaliyokwisha patikana kupitia CCM.
  3. Kuna watu ni waelewa kabisa wa CCM imelifanyia nini, tangu tumepata ihuru, tena wanaitambua fika kuwa kuna baadhi ya maeneo, CCM did not do the best, but its the only one we have, hivyo ni kama zimwi, hivyo bado wataichagua tuu CCM kwa sababu hili ndio the only one we have, ni zimwi likujualo, halikuli likakwisha. Hawa wataendelea kuichagua CCM siku zote daima dumu.
  4. Sababu za why CCM lazima iendelee kuchaguliwa kuongoza taifa hili, nitaendelea nazo wiki ijayo, ila ukisoma baadhi ya hoja hapa chini, utakubaliana na mimi ni muhimu kuendelea kuichagua CCM, ila sasa itakuwa ni CCM mpya, na ukitokea mtu bado una mashaka na hii CCM mpya, wewe you seriously need your head to be examined!, kwa sababu, utakuwa hauko makini na maendeleo ya kweli ya taifa hili, bila wewe mwenyewe kujijua.
  5. Chini ya CCM hii, kumejitokeza kashfa na operesheni saba kubwa zilizotikisa taifa ni pamoja na Operesheni Uhujumu Uchumi, ufisadi katika Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka Nje ya Nchi (Commodity Import Support CIS) na Kashfa ya Rada. Nyingine ni ufisadi Akaunti ya EPA, kashfa ya Richmond, Operesheni Tokomeza Ujangili na ile ya uchotaji mabilioni katika akaunti ya Escrow, japo zimefanyika chini ya utawala wa CCM, zimefanywa na Watanzania individually na sio sera za CCM.
Kama una muda, take time kufanya rejea
  1. Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi ...
  2. Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!.
  3. Yametimia!, CCM Imechokwa!, CHADEMA Ikulu Njia Nyeupe 2015!-
  4. Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target!,
  5. Kuelekea 2015: Ni Mbio Za Magari Kati ya "Mkweche" na
  6. Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa..
  7. Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya
  8. Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed
  9. Edward Lowassa sio lazima yeye tu ndiye awe Rais wetu 201
  10. Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi
  11. Kufanya Kosa Sii Kosa, Kosa Kurudia Kosa!. Je Mwaka 2010 Tu
  12. Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa ..
  13. Topic: Hata ikithibitika Fedha za Escrow ni za Wizi, Nawahakikis
  14. Matokeo ya Serikali za Mitaa: Ni mwanzo wa mwisho wa CCM?!
  15. Escrow: Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!.
  16. Kama Kashfa Escrow ni "Richmond", Then, Lowassa Alionewa
  17. Kagoda, Meremeta, Deep Green, Buzwagi, Bandari, nk
  18. Tanzania na tuhuma za rushwa:Kashfa ya fedha za EPA
  19. Meremeta & TANGOLD Revealed!
  20. ZAFANANA: Kashfa Zote Kubwa Zinaungwa na Nyuzi Zile Zile
Nawatakia Jumapili Njema.

Paskali
 
Mtu kama Mbowe ukimuangalia machoni tu anaonekana sio muaminifu halafu eti ndio umpe uwaziri mkuu kwenye serikali inayoongozwa na fisadi. Acheni mzaha jamani, sumu haionjwi...

Mbowe mashine kubwa,hamtamuweza. Mmejaribu kila mbinu kupitia mamluki wenu wasaliti ili kumng'oa Uenyekiti ikashindikana. Mnajua kabisa aking'oka Mbowe CHADEMA kwisha. Nawaambieni achaneni na Mbowe , huyo ni habari nyingine kabisa.
 
Mbowe mashine kubwa,hamtamuweza. Mmejaribu kila mbinu kupitia mamluki wenu wasaliti ili kumng'oa Uenyekiti ikashindikana. Mnajua kabisa aking'oka Mbowe CHADEMA kwisha. Nawaambieni achaneni na Mbowe , huyo ni habari nyingine kabisa.

Ni kweli mashine kubwa. Angekuwa mashine ndogo vikao vya chama vingemzuia kuuza chama. One man show ya kuuza chama inaweza kufanywa na mashine kubwa tu...
 
Watanzania wengi tumejielewa baada ya kuwa utumwani kwa muda wa miaka 54 chini ya mkoloni CCM. Tunamshukuru sana Mzee BWM kwa hotuba yake pale jangwani kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM. Wengi wetu bado ni Malofa na wapumbavu na kwa mara ya kwanza kabisa ifikapo Oktoba 25, 2015 basi tutaudhihirishia ulimwengu kwamba watanzania wengi ni Malofa na wapumbavu! #mabadiliko
 
Chadema imeshauzwa, ukichagua Chadema unakuwa bidhaa.
Halafu hawa ndio wanaofurahia wakiona vijana wanafagia na kupiga deki barabara ili "viongozi" wapite, na hapo hapo wanadai wanataka kumkomboa mtanzania toka kwa mkoloni mweusi. Wamechanganyikiwa mpaka wameamua kujiita malofa na wapumbavu.
 
Halafu hawa ndio wanaofurahia wakiona vijana wanafagia na kupiga deki barabara ili "viongozi" wapite, na hapo hapo wanadai wanataka kumkomboa mtanzania toka kwa mkoloni mweusi. Wamechanganyikiwa mpaka wanajiita malofa na wapumbavu.

Ile ni fasihi. Unaelewa maana ya kufagia?
 
Halafu hawa ndio wanaofurahia wakiona vijana wanafagia na kupiga deki barabara ili "viongozi" wapite, na hapo hapo wanadai wanataka kumkomboa mtanzania toka kwa mkoloni mweusi. Wamechanganyikiwa mpaka wameamua kujiita malofa na wapumbavu.

Mtu akitulia kidogo tu kutafakari, hawezi kuchagua Chadema mwaka huu...
 
Kitu nilichogundua ni kwamba Watanzania huwa tunashabikia siasa kama tunavyoshabikia mpira wa miguu! Kwamba mimi kama ni mshabiki wa Man U au Yanga basi natakiwa kuishabikia na kuitetea timu yangu. Ishinde, isishinde, ifanye madudu isifanye mi nitaitetea tu..!
Tunachosahau ni kwamba, tofauti na ushabiki wa MPIRA ambao hauna athari zozote kwa shabiki, ushabiki wa siasa una kila aina ya athari kwa kila Mtanzania. Siasa ndio inaayohamua mustakabali wa maisha ya kila mtanzania. Mimi kwa mfano, huwa siwaelewi kabisa watu wanaoishabikia sisiemu halafu wakirudi nyumbani wanaenda kulala gizani kisa hakuna UMEME! Ila acha tuendelee kuchapika. Ipo siku watu wataelewa tu, kama sio mwaka huu ni baada ya miaka mitano au kumi au ishirini.. Kwasababu ninachoamini mimi sisiem HAITABADILIKA KAMWE!
 
Swali hilo hilo watu werevu wanajiuliza. Hivi kuna mtu na akili zake atachagua fisadi papa awe rais? Labda tuwe tumerogwa na freemasons
Na ndio maana Lipumba aliamua kujitoa na kusema nafsi yake inamsuta. Baada ya hapo aliamua kwenda Maka kuhiji, ili ajitakase roho. Lakini hawa akina Kingunge na genge lake, wasioamini dini bali pesa, wamepofuliwa macho ili wasione kipigo kinachowasubiri. Hizo "nyomi" wanazotengeneza kila kukicha zitawatokea puani mwaka huu.
 
Kitu nilichogundua ni kwamba Watanzania huwa tunashabikia siasa kama tunavyoshabikia mpira wa miguu! Kwamba mimi kama ni mshabiki wa Man U au Yanga basi natakiwa kuishabikia na kuitetea timu yangu. Ishinde, isishinde, ifanye madudu isifanye mi nitaitetea tu..!
Tunachosahau ni kwamba, tofauti na ushabiki wa MPIRA ambao hauna athari zozote kwa shabiki, ushabiki wa siasa una kila aina ya athari kwa kila Mtanzania. Siasa ndio inaayohamua mustakabali wa maisha ya kila mtanzania. Mimi kwa mfano, huwa siwaelewi kabisa watu wanaoishabikia sisiemu halafu wakirudi nyumbani wanaenda kulala gizani kisa hakuna UMEME! Ila acha tuendelee kuchapika. Ipo siku watu wataelewa tu, kama sio mwaka huu ni baada ya miaka mitano au kumi au ishirini.. Kwasababu ninachoamini mimi sisiem HAITABADILIKA KAMWE!
Wewe mwenyewe hapo ulipo unaandika kiushabiki shabiki.
 
kama waalimu wanaweza kuichagua ccm na kilicho nimaliza zaidi ni pale nilipoona wale watoto wa mitaani wanaolala kwanye milango ya uwanja wa sheikh Amri abeid pale Arusha wamevalishwa nguo za ccm ili kumpokea Pombe alafu wanaimba hapa kazi tu,
 
CCM, kwa rekodi yake hii, ni Tanzania tu [na labda vinchi vingine hohehahe] ndo inapoweza kuchaguliwa tena na tena.

Tena kwa kiasi kwamba hata upinzani tulio nao waliamua wasubiri kura za maoni za CCM wakope mgombea wa CCM wamsimamishe kwa ticket yao.
No choice at all. Unataka CCM au CCM? That's the choice on the menu!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom