Hivi kweli kesho asubuhi TBC kutakuwa na kipindi cha kusoma magazeti?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Kwa kitendo chao cha kukatisha matangazo ghafla ili kuficha aibu ya waliowatuma,najiuliza kama kweli kesho wataweza kusoma magazeti maana bila shaka yatawaumbua. Naamini yataripoti walichokifanya kwenye front page hiyo kesho.

Kila mtu afuatilie tujue kama kweli TBC ni ukweli na uhakika.

TBC inaendeshwa kwa kodi zetu na nina fikiri kuna umuhimu wa kufanya uchunguzi ili umma ujue ni nini hasa kilitokea na kama kuna aliewatuma basi awekwe wazi ili umma umjue na yeye awajibike kwa kujiuzulu na akikataa awajibishwe.

Habari za bunge ni haki ya watanzania kuzipata.

Leo sijiu Mr. Luku na Weremaa walikuwa wapi kuokoa jahazi kama kawaida yao.
Ni laana inawasumbua na mwisho wao umefika.
 
Back
Top Bottom