Hivi kweli kaya masikini inaweza kuchangia kuinua uchumi wa viwanda?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,329
6,447
Kwa kiwango gani kweli kaya masikini ichangie kuinua uchumi wa viwanda? Kama kuinuka kwa uchumi wa viwanda unategemea kaya masikini, basi Tanzania ingekuwa na viwanda vya kumwaga. Ila swali la nyongeza, ni viwanda vya aina gani? Je, ni kama hicho kwenye picha?

PIC+KAYA+MASKINI.gif

Source: Mwananchi Communications Ltd

Kaya maskini kuchangia kuinua uchumi wa viwanda
 
kiwanda kidogo cha sabuni kinahitaji sufuria nne tu, hata kwa masikini zipo.
 
kiwanda kidogo cha sabuni kinahitaji sufuria nne tu, hata kwa masikini zipo.

Ingekuwa vyema kama ungetoa mchanganuo mzima wa kiwanda kidogo cha sabuni ikiwemo utaalamu wa kutengeneza sabuni, na gharama za kupata utaalamu huo ikiwemo kiwango cha utaalamu husika.
 
Watu wa nchi hii kazi yao kukurupuka na kuropoka ka machiz tu hivi tuna pori kubwa kias gani ambalo ardh yake bado ni bikra majitu hayawaz kufanya kilimo cha kisasa na uborshaji wa masoko yenyew yapo kwenye porojo tu! Hatuna hata kampuni yeyote ya maana ambayo ni multinational ad leo af tunadanganyana tunakua kwa kasi kiuchumi mi naona huu ni ubakaji wa uongoz tu hamna chochote.
 
Kwa kiwango gani kweli kaya masikini ichangie kuinua uchumi wa viwanda? Kama kuinuka kwa uchumi wa viwanda unategemea kaya masikini, basi Tanzania ingekuwa na viwanda vya kumwaga. Ila swali la nyongeza, ni viwanda vya aina gani? Je, ni kama hicho kwenye picha?


PIC+KAYA+MASKINI.gif

Source: Mwananchi Communications Ltd

Kaya maskini kuchangia kuinua uchumi wa viwanda
Wakikubali kuondoa umaskini wa fikra, wakajiamini na kutumia akili zao kisawasawa, wakafanya biashara au kilimo kwa mbinu stahiki, hakuta kuwa na Kaya maskini. Tatizo kubwa kwa hizo kaya zinazoitwa maskini kuonekana duni kupindukia sababu nyingi zinazopelekea hali hiyo ni uvivu, uzembe na kujiendekeza kwa kufanya mambo ambayo hayana tija. Kisa: ipo kaya moja inayoitwa maskini maeneo ya mkoa wa pwani ambayo wakazi wake wengi ni wanufaika na mfuko wa kusaidia kaya maskini TASAF, eneo hilo ni maarufu kwa kilimo cha mahindi na ufuta, wakazi wake wengi ni wakulima, ila wakati wa kuvuna mazao yote huuzwa na pesa kutengwa kwa sherehe za kucheza watoto nk. Changamoto ninayoiona kwenye huo uchumi wa viwanda ni uelewa wa wadau. Amri na magizo yangepungua, mpango na dhana ukaelekezwa kwa wahusika ili kuelewa ndiyo mipango ya uanzishaji iendelee. wengi wanadhani hivyo viwanda vitapelekwa na wachina kwenye maeneo yao ili ajira na vibarua vipewe wakazi wa eneo hilo!!!! nilikuwa napita tu jamani
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom