Hivi kweli jk anastahili kura za watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kweli jk anastahili kura za watanzania?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by majata, Oct 12, 2010.

 1. majata

  majata JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Ahadi alizo zitoa 2005 zimetimia kwa 3%, na ni baadhi tu ya ahadi hizo ambazo zimetimia kwa kiwango hicho, mfano wa ahadi zilizotimia kwa kiwango hicho ni ahadi ya kutoa mikopo kupitia mamilioni ya jk ambayo haikuwa na tija na haijatusaidia bado watanzania kupunguza umasikini wetu ila imeongeza kadhia.

  jk huyu alitoa ahadi nzito sana ikiwemo maisha bora kwa kila mtanzania, ahadi ambayo ilimfanya si tu kupendwa sana na watu bali kuonekana kama musa wa watanzania, ila kwasababu jk alikuwa anaongea kisiasa hakuona uzito wa hilo hivyo alidhani ni mchezo uleule wa kuwahadaa wananchi kwasababu wengi hawajaelimika vilivyo, leo hii watu bado maisha ni magumu tena sana amekuja na kubadili kauli nakusema watu hawana maisha bora kwakuwa hawafanyi kazi ni wavivu tu, haya nimatusi kwani watanzania tunajituma sana lakini mambo bado kwetu sana kwatu tofauti sana na akina liz1 na wengineo.

  sitampigia jk kura pamoja na kwamba mimi ni mwanaccm kwasababu zifuatazo:

  1- jk alitudanganya mwaka 2005 kwamba ataboresha maisha lakini hamna kitu.
  2- Ameshindwa kuchukua hatua kwa watu wanaohujumu nchi yetu waziwazi.
  3- Ametugeuka watanzania kwamba ni wavivu ndio maana maisha yetu mabovu.
  4- Amepelekea chama kiwe na maamuzi ya kifamilia badala ya utaratibu tulio uzoe tangu kipindi cha mwlimu.
  5- Ameshindwa kuiga roho ya uzalendo ya mwalimu na mwinyi kujali maslahi ya mtanzania kwanza.
  6- yeye pia amejilimbikizia maali sana, mijengo kibao, mahoteli,hivyo nivile tu tuonavyo.
  7- ameachilia wawekezaji waendelee kuchukua mali zetu huku wakitutumia sisi wenyewe kuchukua mali hizo kwa ujira mdogo sana na manyanyaso juu.
  8- Ameongoza serikali kisanii sana kwakufwata upepo uvumiako.
  9- badala ya kusimama kama mkuu wa nchi katika maeneo ambayo alistahili kufanya hivyo badala yake mpaka leo anaondoka madarakani ameendelea kukaa na list za wauza madawa ya kulevya bila kuwachukulia hatu.

  10- Anapenda sana upopularity wake na familia yake, kuliko maendeleo ya watu anao waongoza.

  Nimeamua kumpigia kura yangu DR Slaa wa Chadema awe rais wangu mpya tar 31 oct 2010.:nono:
   
 2. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Big nooooo.... Mwenye macho haambiwi tazama kazi kwako kumchagua slaa
   
 3. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hata yeye mwenyewe anajua kuwa hastahili kura za watanzania
   
 4. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haitaji kura ya watanzania walio wengi, isipokua atapata ya mkewe, Riz 1, Makamba na kinana !!! Nadhani
  hata Mama Kilango hatampa kura yake !!!
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nyingine ni kuwa yu Mgonjwa anaitaji kupumzika
   
 6. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hata ya kwake mwenyewe hatakiwii kupata
   
Loading...