Hivi kweli hawa ccm hawatataka tutumie vitambulisho vya taifa kupiga kura 2015??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kweli hawa ccm hawatataka tutumie vitambulisho vya taifa kupiga kura 2015???

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimweli, Jul 18, 2012.

 1. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kutokana na Mwamko wa watu kutaka kujiandikisha kwenye dafutari la wapiga kura siku yoyote itakayotanganzwa. Naona kama serikari-CCM watatumia njia ya ili uandikishwe lazima uwe na Kitambulisho cha Taifa na nimesikia ili ujiandikishe ni razima uwe na miaka 18. Mimi naamini kwa jinsi watanzania walivyo na hasira na Serikari-CCM watasusia kujiandikisha nikiwemo na mimi sina mpango kabisa wa kujiandikisha labda kama itahusisha Kupiga kura. Kwa ninavyoamini mimi wa Tz wengi watasusia hili zoezi na hii ndiyo njia pekee itakayotumiwa na CCM, ili mtu upige kura lazima uwe na kitambulisho cha Taifa. Na je 2015 wataandikisha tena?? Na kwa nini wasingefanya vyote kwa pamoja Kura+Kitambulisho cha Taifa kwa sababu walegwa ni walewale!!!?

  Wataalaam lioneni hili na mshauri
   
 2. S

  STIDE JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu binafsi sijakuelewa!!

  Kitambulisho cha Taifa kipi ambacho utatakiwa uwe nacho ili uandikwe?

  Alafu kuandikwa kwenye daftari la wapiga kura mbona ni kawaida lazima uwe na 18yrs? Au kuna mabadiliko!?

  Chondechonde Watanzania msiwe na hasira za mkizi!! Itakuwa faida kwa mvuvi(ccm)!! Hawa dawa yao ni kukomaa nao hadi dakika ya mwisho!!

  "PAMOJA TUTASHINDA!!"
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Nimekuelewa vema mkuu, kwa kuwa wanaosimamia zoezi zima la kuandikisha wananchi wenye sifa ya kupata kitambulisho cha taifa, naamini wanahakikisha wanachama wao (ccm) wanapata hivyo vitambulisho, wakiisha hakikisha hilo watapeleka muswada bungeni kurekebisha utaratibu wa uandikishaji wa wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapigakura, ambapo kipengele cha qualification itakuwa uthibitisho wa utaifa wako kupitia hicho kitambulisho, sheria hiyo itapitishwa kutokana na wingi wa wabunge wa ccm, na sheria hiyo itawafungia nje wakereketwa wengi wa chadema au wenye mrengo wa kushoto, hiyo karata ni turufu kwa ccm.
  Nashauri M4C pamoja na mambo mengine iwahamasishe wananchi kuchangamkia vitambulisho hivyo.
  Sehemu niliyopo naona wanazi wa ccm wanavyojipanga kujiandikisha.
  TAKE IT VERY VERY SERIOUSS.
   
 4. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu kwa jinsi vuguvugu la kisiasa nchini lilivyo nakubaliana na wewe, umewaza mbali sana, hawa magamba wanaweza kutumia huo mwanya ili kukandamiza demokrasia inabidi M4C iwaelimishe watu na hilo.Hongera sana
   
 5. D

  Davie Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Umewaza na kuongea kitu muhimu sana..ccm wana mbinu sana na bila shaka hiii ilikuwa ipo jikoni wawakamatie wanachi hapo..
  CDM walione hili na wawaelimishe wananchi..
   
 6. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Inabidi twendi kisayansi kabisa kupambana na hawa watu, mimi naamini wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kufanya kazi hawategemei CCM ili waishi na nijuhudi zao ndizo zinawaongoza na ni hawako CCM ni either wako CDM or hawana chama. Please let us go go, Ni kweli kabisa M4C inabidi wasisitize sana watu kwenda kujiandikisha. Mimi ninaswali moja hivi ni kwa nini wameweka lazima uwe na miaka 18?????? Kwani under 18 hawana haki ya kuwa raia??
  Mungu fungua watanzania wako hawa wafanye kama unavyotaka wewe. HAKIKA CCM HUU NDIO MTEGO WAO
   
Loading...