Hivi kwanini watu wengi wenye akili nyingi (genious)siyo waongeaji/huwa hawajui kujieleza?

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
19,352
14,381
Wakuu heri ya X-Mass na Mwaka Mpya,

Kama ambavyo heading inajieleza yenyewe,

Naomba tuelimishane jamani, nimejaribu kuchunguza sana nikagundua kuwa watu wengi (asilimia kubwa) ya watu wenye akili nyingi, maarufu kama genious people, huwa sio waongeaji na mara nyingi huwa hawajui kujieleza kabisa, hii ni tofauti na sisi akina simple mind, yaani watu tulio na akili za kawaida za kutafutia riziki ya maisha, sisi ni waongeaji sana, labda ndio maana tunaiweza sana siasa

Sasa naomba kujua ni kwanini hali ipo hivyo.
 
Mwl nyerere alikuwa Genius na alikuwa anajua kujieleza vizuri sana.Prof. Lipumba alipata division one point 3 A level EGM na UDSM alipata GPA ya 5.0 1983 na bado ni mzuri tu kujieleza japo alishiriki kwny uhalifu wa kijamii kuanzisha mtandao wa Kigaidi wa Ukawa.
 
mbona lowasa zamani alikiwa anajua kujieleza vizuri tuu hata ukiangalia clip zake YouTube.inamaana huo ujiniaz umempata baada ya kuugua ugonjwa wake huo hadi cku iz tunamuona hawezi jieleza vizuri???
 
Yaani nachukia watu wanojitangazaaaa yaani basi tu. Ati na weye umejiona kwenye kundi la simple minds! Haya baanaa so weye nawe upo kwenye kundi. Mbona nakuona ka wale dull kabisa wanaokaa kukodolea macho dirishan kuona ka wanaweza kutizama fulan wamjadili
 
Wakuu heri ya X-Mass na Mwaka Mpya??,Km ambavyo heading inajieleza yenyewe,naomba tuelimishane jamani,nimejaribu kuchunguza sana nikagundua kuwa watu wengi(Asilimia kubwa)ya Watu wenye Akili nyingi,maarufu km Genious people,huwa sio wangeaji na mara nyingi huwa hawajui kujieleza kabisa,hii ni tofauti na sisi akina Simple mind,yaani watu tulio na Akili za kawaida,za kutafutia riziki ya maisha sisi ni waongeaji sana,Labda ndio maana tunaiweza sana Siasa,Sasa naomba kujua ni kwanini hali ipo hivyo???.

Christmas siyo x-mas hiyo x-mas ni yawapinga christu kama wewe.
 
Simple mind discuss people, Greater mind discuss ideas. Genius silent act.
 
Back
Top Bottom