Perry
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 10,043
- 2,000
Nilikua nabadilishana mawazo na mmama mmoja hivi mkenya ambaye ni HR kwenye NGO fulani ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kuhudumia wakimbizi kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara akawa ananiambia watz wengi hatupendi kujihangaisha na kuomba kazi za kimataifa.
Akatolea mfano NGO yao ilitangaza nafasi kama 8 kwa raia wa Tanzania tu, ila cha ajabu ni watanzania wawili tu waliojitokeza kuomba hizo kazi tena na wao baada ya kuwashortlist cha ajabu kwenye interview hawakutokea ikabidi nafasi zichukuliwe na wakenya..
Sasa naye akawa anashangaa watanzania tuna matatizo gani huku tunalia hakuna ajira lkn tunakuwa wazito kutuma maombi ya kazi pindi zinapotolewa..
Kwa kweli me nilichomjibu ni kwamba kwa watanzania ili uonekane una kazi basi ni lazima uajiriwe na serikali hivo wengi wao wanapenda kuomba kazi huko sasa sijui kama jibu langu lilikua sahihi au sio sahihi wakuu?