Private jobs hakuna security of employment. Wakati wowote unaweza kufukuzwa kazi. Mfano mwaka jana kipindi cha corona wengi waliachishwa kazi na hawajarudi kazini. Najua mtu mpaka leo anahangaika hajapata kazi. Kungkuwa na security nadhani watu wangeprefer kuajiriwa huko. Serikalini hakuna aliyefukuzwa na waliendelea kulipwa mishahara. Serikalini mpaka ufukuzwe ni process ndefu. Kwenye sekta binafsi unaajiriwa kwa mkataba wa miaka michache sana miwili nadhani. Mtu anataka akipata kazi iwe ya kudumu e.g unakaa 30 yrs na hata pensheni itakuwa nzuri. Ila kwa sasa fursa ni nyingi za kujiajiri. Tatizo kuijua hiyo fursa na nadhani mtaji pia ni tatizo. Wasomi wanaweza kujiajiri.Kuna tatizo sana kwa watanzania wasomi kuamini kuaijiriwa mpaka upate kazi serikalini. Hii mindset tunaweza kuiondoaje kwa wasomi? Mfano hai ni kwenye hizi ajira za walimu na wafanyakazi afya idadi kubwa imejitokeza kuomba ajira hizo na kupelekea kuonesha kuwa hapa Tanzania kuna tatizo kubwa la ajira kwenye hizo kada kitu ambacho si kweli.
Mimi binafasi kuna jamaa zangu watano wameajiriwa shule binafsi na wengine wana maendeleo mazuri tu mpaka kujenga lakini kila ajira zikitangazwa wanakimbizana kuomba serikalini na kuwaaribia wengine ambao hawajapata pa kujishikiza,kuna mmoja nilimpigia nikamwambia kabisa usithubutu hata kidogo kutoka hapo kibaruani ulipo eti unakuja serikalini utajutia sna,maendeleo aliyonayo mimi niliyepo serikalini hata robo simfikii lakini wazazi wake wanamshinikiza aombe serikalini kila mara. Kuna jamaa wengine tunaofahamiana wapo hospitali binafsi na wana maisha mazuri lakini na wao wana hiyo mindset.
Ushauri kwa serikali. Iandae mpango kazi wa urasimishaji ajira kwenye sekta binafsi na mashirika pamoja na waliopo serikalini. Kwa uchunguzi wangu unaonesha kuwa hawa wafanyakazi waliopo sekta binafsi hawatambuliki popote hata kodi hawalipi lakini wapo wengi sana walioajiriwa sekta binafsi. Mwenye takwimu sahihi ya idadi ya mashule na vituo vya afya binafsi alete hapa uone idadi yao ilivyokubwa na bado shule na hospitali zinaongezeka kila mwaka lakini bado watu wanasema hakuna ajira. Mtu kuajiriwa sekta binafsi anajiona kama vile amejishikiza huku akiwainda kuingia serikalini.
Ushauri mwingine kwa serikali, izidi kuwabana hawa wamiliki wa hizo taasisi binafsi wahakikishe wakitimiza mahitaji yanatakiwa kwa muajiriwa kama bima,mkataba mzuri na usalama kazini.