Hivi kwanini wasomi wa Tanzania wanaamini kuajiriwa ni Serikalini tu?

kasigazi kalungi

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
3,887
2,000
Kuna tatizo sana kwa watanzania wasomi kuamini kuaijiriwa mpaka upate kazi serikalini. Hii mindset tunaweza kuiondoaje kwa wasomi? Mfano hai ni kwenye hizi ajira za walimu na wafanyakazi afya idadi kubwa imejitokeza kuomba ajira hizo na kupelekea kuonesha kuwa hapa Tanzania kuna tatizo kubwa la ajira kwenye hizo kada kitu ambacho si kweli.

Mimi binafasi kuna jamaa zangu watano wameajiriwa shule binafsi na wengine wana maendeleo mazuri tu mpaka kujenga lakini kila ajira zikitangazwa wanakimbizana kuomba serikalini na kuwaaribia wengine ambao hawajapata pa kujishikiza,kuna mmoja nilimpigia nikamwambia kabisa usithubutu hata kidogo kutoka hapo kibaruani ulipo eti unakuja serikalini utajutia sna,maendeleo aliyonayo mimi niliyepo serikalini hata robo simfikii lakini wazazi wake wanamshinikiza aombe serikalini kila mara. Kuna jamaa wengine tunaofahamiana wapo hospitali binafsi na wana maisha mazuri lakini na wao wana hiyo mindset.

Ushauri kwa serikali. Iandae mpango kazi wa urasimishaji ajira kwenye sekta binafsi na mashirika pamoja na waliopo serikalini. Kwa uchunguzi wangu unaonesha kuwa hawa wafanyakazi waliopo sekta binafsi hawatambuliki popote hata kodi hawalipi lakini wapo wengi sana walioajiriwa sekta binafsi. Mwenye takwimu sahihi ya idadi ya mashule na vituo vya afya binafsi alete hapa uone idadi yao ilivyokubwa na bado shule na hospitali zinaongezeka kila mwaka lakini bado watu wanasema hakuna ajira. Mtu kuajiriwa sekta binafsi anajiona kama vile amejishikiza huku akiwainda kuingia serikalini.

Ushauri mwingine kwa serikali, izidi kuwabana hawa wamiliki wa hizo taasisi binafsi wahakikishe wakitimiza mahitaji yanatakiwa kwa muajiriwa kama bima,mkataba mzuri na usalama kazini.
 
reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,813
2,000
Hii ni kweli, Nina classmate wangu alikua anafundisha Private anakula 900k take home, akaomba ajira za serikali akapata bila kujiuliza akaenda,
Nikijana kabisa 28 yrs anakimbilia serikalini, kuanza kuwaza kiinua mgongo na vijisababi vingine vya kijinga Eti security.
 
kasigazi kalungi

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
3,887
2,000
Hii ni kweli, Nina classmate wangu alikua anafundisha Private anakula 900k take home, akaomba ajira za serikali akapata bila kujiuliza akaenda,
Nikijana kabisa 28 yrs anakimbilia serikalini, kuanza kuwaza kiinua mgongo na vijisababi vingine vya kijinga Eti security.
Ni upuuzi wa hali ya juu sana. Huyo muacha atajutia sana kama kungekuwepo na uwezekano ungeniunganisha nae tukabadilishana kazi.
 
May 11, 2021
53
125
Hili tatizo lipo sana hata mimi ni muanga. Nilikuwa shule binafsi,ninalipwa vizuri tu na ofa kibao kama nyumba na kutolipa bills, tukiwa huko taasisi binafsi tunadanganyana sana eti serikalini kuna security na kusahau kinachomata maishani ni kuishi vizuri. Sasa hivi nipo serikalini nimeshafanana mchimba chumvi. Watu wengi wapo sekta binafsi lakini wanajiona hawana ajira mpaka waajiriwe na serikali.
 
dadaake

JF-Expert Member
Jan 10, 2017
969
1,000

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
43,755
2,000
Tatizo ni serikali yenyewe inashindwa dhibiti private sectors

Kampuni hazilipi vizuri..
Mikataba hakuna..
Kampuni za outsourcing zinazidi ongezeka..

Wakati fulani Tigo ilikuwa mshahara unaanza 1milion..sasa wakaleta outsourcing company ukashushwa hadi laki kadhaa..

Huo mfano mmoja
Ukienda Vodacom hivyo hivyo

Nani ana ndoto za kuajiriwa Azam au Mo?

Wanakuwaje matajiri lakini kampuni zao hazivutii kabisa wafanyakazi?
Hata bonus Tu hakuna achilia mbali shares kwa wafanyakazi..
 
Hank_31

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
502
1,000
Hili tatizo lipo sana hata mimi ni muanga. Nilikuwa shule binafsi,ninalipwa vizuri tu na ofa kibao kama nyumba na kutolipa bills, tukiwa huko taasisi binafsi tunadanganyana sana eti serikalini kuna security na kusahau kinachomata maishani ni kuishi vizuri. Sasa hivi nipo serikalini nimeshafanana mchimba chumvi. Watu wengi wapo sekta binafsi lakini wanajiona hawana ajira mpaka waajiriwe na serikali.
Hahahahahahahahah
 
radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,120
2,000
Fursa nyingi zipo huko serikalini hata mabenk yangekuwa yanatoa mikopo sawasawa watu wa serikalini na kwenye sector binafsi kungekuwa level fulan ya kutia moyo halafu mikataba na uhakika wa ajira pia lingeangaliwa haiwezakan unaajiriwa unapewa kila mwaka mkataba au miaka miwili miwili huoni kama ni kichomi muda wowote ajira inakufa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom