Hivi kwanini Wanawake wengi walioolewa wanapenda sana kuonyesha pete zao za ndoa tofauti na sisi wanaume?

Wanaume muda mwingi tunakuwa kwenye majukumu kwaiyo pete huwa inaleta changamoto kwenye kukamilisha majukumu alafu ukiongeza na kiasi cha joto duniani yani ndo kabisa ukivaa joto lina ongezeka mwilini

Kabisa mkuu, yaani sehemu yenye pete inatoka jasho la ajabu kabisa. kidole kinakuwa kama kimeungua na kinaweza kukatwa, kitaalamu inaitwa Fungiothessis Intolerablos Pandus
 
Kwanini hampendi mkuu?
Niliwahi kuwa mpenda pete na cheni sana wakati wa ujana na shule.

Neanda nyumba za muziki na mabling bling hayo basi nafurahi kwelikweli.

Lakini baadae nikajikuta sina hamu navyo na wala sivutiki navyo tena.
Kwahiyo nilishajiwekea kabisa, pete ya ndoa nitashauriana na mwenzangu kuwa baadae nitaivua.
Huwa naivaa kwenye matukia ya nadra sana kwa mfano kama mimi na yeye tunasimamia harusi.

Uzuri alinielewa japo kwa shida na baadae ameshazoea.
Nakumbuak ilibaki kidogo awaambie dada zangu kuwa nimekataa kuvaa pete.

Nilimwelewesha akaelewa.

Utaona hata maelezo yangu hapo hakuna sababu ya msingi ni basi tu sipendi pete.
 
Wengine huenda mbali zaidi kwa kujinunulia Pete na kujivalisha.

Mfano ni baadhi ya wafanyakazi wa banks n.k hujinunulia na kujivalisha wenyewe

Ndipo linakuja swala la mtu muongo hujidanganya mwenyewe nafsini mwake!
 
Wengine walishaachana na talaka mahakamani kutolewa lakini Pete bado wanavaa na vyeti vya ndoa bado viko kwenye mafaili.

Sijui maana yake ni nini?!
 
Back
Top Bottom