Hivi kwanini wali wa mkaa ni mtamu kuliko ule wa 'rice cooker'?

Mimi naamini kwenye upishi wa wali ni kama inatengemea na mikono ya mtu, ukipika kwa rice cooker wali unatoka vizuri sana, unakuwa kama vile umejichambua chambua hivi unakuwa mtaam, ukikutana na demu wa Tanga au Mpemba aiseee anakupikia kitu kitamuuu, hadi ufikiria labla ni mpishi wa The Gleneagles Hotel.....
 
Hahahahah braza, wali wa mkaani utabaki kuwa noma tu.
 
Wasalaam,
Mimi bwana huwa napikia wali kwenye Rice Cooker lakini juzi nimeenda kumtembelea dada moja ni Mzenji wali wake kwenye mkaa na wakati unapikwa nikasikia harufu ile nzuri nzuri kabisa na wali wake ulivyotoka aisee niliona kabisa utofauti na ule wa Jiko la mzungu. Sasa wadau ili wali uwe vizuri ni lazima nifanye mabadiriko au mimi ndiyo sijui kupika ???
Kutokujua kupika mbali, ila muhimu uelewe kila aina ya jiko ina ladha yake ya chakula. pia kila aina ya chombo unachopikia kinaleta ladha tofauti. Sufuria, chungu, mwiko wa mbao, chuma....
 
Jiko la mkaa, chungu vinaongeza ladha ya chakula. Maharage au mchuzi uliopikwa kwenye chungu hauwezi kufananisha na kitu cha sufuria.

Nafikiri namna ya nishati ya joto inavyopenya na kuivisha chakula, kuna tofauti sana kati ya jiko la gesi, rice coocker zinatofautiana japo vyakula vyote vitaiva.

Ndio maana mkaa utatumia muda mrefu kulinganisha na umeme na hapo ndio siri ya mahanjumati ilipolala.
Always chakula kitamu hakitaki pupa.ndo maana mm huwa napenda kupika wali kwenye jiko LA mkaa coz unaiva taratibu. Yaani unachambuka vizuri. Nakuwa nimetoa kitu wali na sio ubwabwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam,
Mimi bwana huwa napikia wali kwenye Rice Cooker lakini juzi nimeenda kumtembelea dada moja ni Mzenji wali wake kwenye mkaa na wakati unapikwa nikasikia harufu ile nzuri nzuri kabisa na wali wake ulivyotoka aisee niliona kabisa utofauti na ule wa Jiko la mzungu. Sasa wadau ili wali uwe vizuri ni lazima nifanye mabadiriko au mimi ndiyo sijui kupika ???
Gas cooker ipo vizuri pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sa kwa viungo vyote hivyo si bora upike tu pilau ilaa tuseme ukweli rice cooker nminakuwaga kama inababuaa mchele ukiiva unakuwa kama spnge flani yaan kuna kitu kinakosekana smae applied to jiko la umeme ilaa mkaa ni balaa

umenena...mbwembwe nyingi kwenye wali bora upike pilau tu sasa
 
Raha ya wali ukipika upunguze moto uweke makaa juu ya mfuniko
MATANDU.

Muda wa kupakuliwa Chakula, ni raha pale yanapoanza kuondolewa MATANDU.

Hiyo kama upo karibu na Mpishi lazima uombe kuonja MATANDU.

Kama ni Mpishi mwenye gubu, anakutimua, "toka,"mtoto wa KIUME unaleta HILA jikoni" "toka".

MATANDU yakimwagiwa MCHUZI, au MAHARAGE na ROJO yake, acha tu.

Jamani
 
Huwezi amini sasa hivi kupika wali kwenye mkaa siwezi natoa bokoboko, ila kwa rice cooker natoa kitu konki na ukoko laini wa chini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom