Hivi kwanini Wabunge wa Vyama vya Upinzani wasiwe na kinga ya kubaki Bungeni kama sisi watu wa Kanisa kwani tunafanana sana kwa mambo mengi?

Oct 24, 2020
20
75
Kwa upande wa kanisa kunavituko vingi sana vya ajabu makanisani lakini hakuna mahara pa kusemea kwa sisi waumini labda kubadilisha kanisa lakini kwa wanasiasa na taifa kwa ujumla kila baada ya miaka 5 kuna sehemu ya kusemea hivi kwanini na hawa wanasiasa wa upinzani nao wapewe kinga kama ya maprofeti feki maana leo kanisania mara mtume au nabii anasema waumini wale majani, mara baadhi ya mitume na manabii kuwashika matiti dada zetu mara kuchukua sadaka kingivu, mara 1 or 1 yaani mchungaji kujifungia na mkeo ndani ya ofisi yake akinfanyia maombezi mazito na mengine.

Minaona hawa wapinzani pamoja na kuwa wanapinga kilakitu kama vitambulishoa vya mjasiliamali ambavyo wajasiliamali wadogo wamevionaona kama Mungu kashuka kwani waliteseka na mgambo na TRA huko nyuma.

Wapinzani wanapinga elimu bure, wanapinga ujenzi wa barabara, wanapinga Bwawa la umeme la JK. Nyerere. Wakwenda mbali hadi kutetea walarushwa na mafisadi nayo ni yakushangaza kama huku kwetu jamani, wapewe kinga kama vile kila baada ya uchaguzi kuisha hata kama hawakupata hata mbunge mmoja wapewe nafasi za wabunge wanaume 90 kuingia bungeni hili tuwe na usawa wa kidemokrasia na kuendelea kushuhudia wanavyo susa na kufunga midomo bungeni na kujifunza mitusi.

Freeman Mbowe apewe ukuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kama alivyopewa Urais wa maisha marehemu Kamuzu Banda wa Malawi. Huu ni ushauri wangu na ninalindwa na ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania. Lemi na Suga hawa wapewe hayo majimbo milele kwanza Suga yeye tayari alishajiita raisi wa jimbo lake, kuna ubaya gani mbona kanisani hata kama nabii au mtume akiua watu lakini bado anabakia na unabii wake na anakusanya sadaka kama kawa kwanini wanasiasa hawa wa upinzani asifanyiwe hivi kuwa na kinga.

Angalia sasa wanavyo lalamika kila saa katika mitandao tena wanaimani kuzidi ya Ibrahim baba wa imani maana wanaamini kuwa wazungu watawarudisha bungeni tu, tuseme amina. Imani hii imepata kutokea hata kwa Maalim Seif wa Zanziba mwaka 2015 alisema ataingia Ikulu dakika chache tu lakini mpaka leo hii bado ajaingia Ikulu, hii kwa sisi watu wa kanisa ndiyo imani tunayoitaka yaani imani ya kuuamisha mlima Kilimanjaro na kuuleta Kinondoni maana kule Moshi wakenya wanasema wakwao.

Kuwa na Imani kama kuamini katika nguvu ya umma ambayo huo umma wenyewe haupo hili pia ni jambo ambalo sisi watu wa kanisa tunathamini sana hivyo nao wapewe kinga. Kuna vitu vingine vya ajabu sana hata huku kanisani vipo, kama vile hapa TZ kuna chama kikuu cha upinzani ambacho kinataka kuchukua nchi na kinapata ruzuku ya 360,000,000/- kwa mwezi lakini hawana hata ofisi ila wamepanga kachumba pale Ufipa, bila hata ya aibu wanataka kuchukua nchi, jamani tuwape hili kuexasaizi demokrasia kwani CCM inataka kukaa madalakani milele ifike wakati itoe pande kama ofa jamani.

Hawa viongozi wa vyama vya upinzani wanafanana sana na viongozi wa kanisa kwani Mchungaji au nabii au mtume au askofu anakaa katika kiti chake na kukusanya sadaka mpaka Mungu atakapomchukuwa, vivyo hivyo viongozi wa vyama vya upinzani nao wanakaa ofisini mpaka Mungu atakapo penda na si wafuasi, jamani wapewe kinga ya kubaki bungeni hawa tunafanana sana nao.

Sisi huku kanisani kukusanya sadaka ndiyo jadi yetu kwani ukiingiza tu, lazima uache sadaka kapu kubwa sana na mnajipanga mistari kuona kama kunamtu kabaki katika kiti, nimeona vyama vya upinzani tena kikiongozwa na chama kikuu cha upinzani nao wanapitisha kapu kubwa kama kanisani jamani tunafanana sana nao wapewe kinga ya kubaki bungeni.

Jamani nalindwa na ibara ya 18 hivyo kunitusi utapata dhami bila msamaha, nawasilisha. Mtoto wa Mchungaji.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,447
2,000
Umejiunga hapa jukwaani mwezi uliopita kuja kuandika huu utoto hapa jukwaani? Nakushauri urudi shule ukajifunze kuandika maana sasa hivi elimu ni bure.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom