Hivi kwanini vipindi vya radio na Tv zote Tanzania vinafanana, anaandaa mtu mmoja?

chiumbimnungu

Senior Member
Mar 25, 2017
151
217
Ni mfatiliaji mzuri sana wa vyombo vya habari Tanzania ila kitu nilichojifunza ni kuwa kwanini vipindi vingi vya radio na tv Tanzania vyote ni kama vinafanana tu, kiasi kwamba ukiamka asubuhi kila kinachofanyika radio na tv flani basi ni kile kile kuanzia asubuhi hadi usiku. Pia katika tv za Tanzania imefikia wakati ikifika kuanzia saa 4 hakuna jipya zaidi ya kila Chanel kupiga mziki hivi hawa hawa jamaa hawajui kuwa kuanzia saa 4 ndio muda wa watu wazima kuwa wametulia majumbani mwao?

Inaboa inapofikia muda huo kila Chanel ni mziki tu nilikuwa nawafatilia TV 1 walikuwa wanaenda vizuri ila nao sasa naona hakuna jipya kabisa wameshaungana na wengine.
 
Wanaigana sana.

Tofauti ni majina ya vipindi tu ila yaliyomo ni yaleyale.
 
Wote wana hangover ya Redio Tanzania.

Wote taarifa ya habari saa mbili.

Wote wanaanza na za kitaifa,kimataifa,biashara,michezo

Wote hawaongezei chochote katika habari,zaidi ya habari za fulani kasema,unaweza kutaraji kwa mfano wakati anasema habari za ujio wa waziri mkuu wa Ethiopia,ivutwe Ramani ya Ethiopia ikionyesha majirani zake,historia, na walau video mbili tatu za sehemu muhimu za Ethiopia,pia unataraji waandishi wanakuwa wameshamtafuta balozi wa Ethiopia Siku moja kabla na kufanya mahojiano nae. Pia unataraji waandishi wawe wameenda ofisi ya taifa ya takwimu ili kujua tuna mahusiano kiasi gani kibiashara na kijamii.

Waandishi wote wakianza kusoma taarifa ni kama kasuku,atasomaaaa weee, huoni intelligence ya msomaji na pia wengi hata lugha ya maumbile huioni usoni mwao wala mikononi,huwezi jua anatangaza habari ya huzuni,furaha ama nini.

Kimsingi wanatakiwa wawe na ubunifu,
 
nakushauri uangalie azam tv habari utaona utofauti mkubwa sana kwenye upangaji wao wa habari na hata yale mambo ya reporters kubana pua na kuvuta sauti huwezi kuyaona pale
 
Nafikiri ni product ya guidance ya mamlaka mbovu ya usimamizi ya TCRA, kusimamia maadili ambayo pengine ni irrelevant, na Sio hivyo tu, bali wanaongea pumba mwanzo mwisho....
Yani radio presenter badala asome story anatoa ushauri wa maisha na kuendeleza ushabiki wa kijinga...

Mara ya mwisho kusikiliza radio hata ckumbuki ni lini
TV ndio kabisa.. Labda ITV dk kumi za mwanzo wa News...

Kwa mbaali nadhani ETV watakuja vizuri.
 
Yaani TV zote lazima wapige mabongo fleva..Wanataka kufanya kila kitu ilhali wangeweza kujikita eneo moja na kuliboresha mfano Aljazeera na siasa za mashariki ya kati..
 
Tatizo ni copy and paste kwa TV na Redio nyingi.

Ila Azam TV wako makini sana na wako tofauti na TV nyingi sana ktk vipindi vyao.

Ujue Tanzania tuna ugonjwa inaitwa
ITV Syndrome
 
Wote taarifa ya habari saa mbili.
Wote wanaanza na za kitaifa,kimataifa,biashara,michezo
Wote hawaongezei chochote katika habari,zaidi ya habari za fulani kasema,unaweza kutaraji kwa mfano wakati anasema habari za ujio wa waziri mkuu wa Ethiopia,ivutwe Ramani ya Ethiopia ikionyesha majirani zake,historia, na walau video mbili tatu za sehemu muhimu za Ethiopia,pia unataraji waandishi wanakuwa wameshamtafuta balozi wa Ethiopia Siku moja kabla na kufanya mahojiano nae. Pia unataraji waandishi wawe wameenda ofisi ya taifa ya takwimu ili kujua tuna mahusiano kiasi gani kibiashara na kijamii.
Waandishi wote wakianza kusoma taarifa ni kama kasuku,atasomaaaa weee, huoni intelligence ya msomaji na pia wengi hata lugha ya maumbile huioni usoni mwao wala mikononi,huwezi jua anatangaza habari ya huzuni,furaha ama nini.
Kimsingi wanatakiwa wawe na ubunifu,[/QUOTE]
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
1. Wamiliki ni wabahili kuajiri watu wenye vipaji, elimu na weledi wa taaluma, ulishawaza mtu kama SAN MAELA au EMEDI KIVUO utakuwa analipwa bei gani? sidhani kama unazidi laki 5/month (Take home), ndo maana hakuna innovation zaidi ya kuishi kwa posho za kwenye bahasha za press conference.

2. Klauz Habari msomaji wake Wali Nazi, anaeleweka ni mganga njaa so hakuna ubunifu pale zaidi ya kutafuta soko.
3. Kidoogo AZAM japo naiangaliaga baa, maana sina king'amuzi chake home.
4. Star TV (nimebaki kuangalia BBC na STRAIGHT TALK AFRICA tu)
5. TBC (labda nisikie wanazindua mbio za mwenge kitaifa, au sherehe za muungano).
NB: Vizuri vinaundwa kwa pesa.
 
Wewe umenena. Hivyo hivyo hata taarifa ya habari ya saa mbili uck chaneli zote habari ni .moja tu . Ipoje hapo ?
 
Tatizo wasimamizi wa hivyo vituo na watangazaji washageuka mawakala wa maduka ya nguo na saloon
 
nakushauri uangalie azam tv habari utaona utofauti mkubwa sana kwenye upangaji wao wa habari na hata yale mambo ya reporters kubana pua na kuvuta sauti huwezi kuyaona pale
Tofauti ni ndogo sana pale.
Ushindani wa kina ni sifuri usibishe.
Kwa mfano kuna mantiki gani chanel zote nchini isipokuwa chanel10, kusoma taarifa za habari muda mmoja?
Tv tuzitumiazo ni "multi chanel" tunageuzageuza kuangalia chanel zote jinsi mtu ajisikiavyo.
Kungekuwa na ubunifu wa kishindani, kila chanel (station) ingetangaza taarifa kwa muda wake, pamoja na kuprogram vipindi kivyao tofauti na chanel nyingine, hapo "walaji" tungeangalia taarifa za habari kwa mapana bila kupitwa na jambo lolote.
 
kwangu mi naona saa moja na saa mbili ni perfect time kwa news bulletin maana watanzania asilimia kubwa wanakuwa washafika majumbani mwao wana-watch kideo ila kutoka saa mbili na kuendelea utazamaji unapungua mkuu rejea ripoti za watu kama Geopoll na wengineo. kinyume na hapo ni vyema mtu akaangalia itv habari za saa mida ya saa nne,saba,saa kumi na saa jumi na mbili jijiletu/Hapa na pale au tbc nao wana rusha habari timing kama hizo za wa ITV au channel ten. Kuhusu vipindi mi nadhani ubunifu ni kweli kabisa hakuna radio/tv shows za kutosha na ndiyo maana radios na tvs nyingi wanaamua kupiga miziki na kujiunga na other channels kama dwtv/bbc/cnn. Mtu akibuni sana basi utakuta amekopy shows za nje kisha anabadili jina tu. Nimependa programing ya azam tv kwenye habari wanachanganya na katikati ya habari kunakuwa na mahojiano LIVE kitu ambacho wengine baadhi wanafanya system moja tu ile ile kitaifa,kimataifa,africa,bizness,michezo,utabiri,OVER!
 
Wamekosa ubunifu kwasababu Hakuna ushindani. Angalia salim kikeke na bbc swahili habari zao zimeshiba facts na uchambuzi wa kutosha. Itv wanasoma habari utafkiri wanakimbizwa. Unakuta habari kimataifa wame record kutoka aljazeera au CNN wameshindwa hata kutafsiri. Unakuta habari inasomwa kwa kiswahili ila trump anaongea kiingereza.
 
kwangu mi naona saa moja na saa mbili ni perfect time kwa news bulletin maana watanzania asilimia kubwa wanakuwa washafika majumbani mwao wana-watch kideo ila kutoka saa mbili na kuendelea utazamaji unapungua mkuu rejea ripoti za watu kama Geopoll na wengineo. kinyume na hapo ni vyema mtu akaangalia itv habari za saa mida ya saa nne,saba,saa kumi na saa jumi na mbili jijiletu/Hapa na pale au tbc nao wana rusha habari timing kama hizo za wa ITV au channel ten. Kuhusu vipindi mi nadhani ubunifu ni kweli kabisa hakuna radio/tv shows za kutosha na ndiyo maana radios na tvs nyingi wanaamua kupiga miziki na kujiunga na other channels kama dwtv/bbc/cnn. Mtu akibuni sana basi utakuta amekopy shows za nje kisha anabadili jina tu. Nimependa programing ya azam tv kwenye habari wanachanganya na katikati ya habari kunakuwa na mahojiano LIVE kitu ambacho wengine baadhi wanafanya system moja tu ile ile kitaifa,kimataifa,africa,bizness,michezo,utabiri,OVER!
Chalz Hillary amesaidia kuboresha
 
Radio ndo shida....
Ukifungulia radio mbalimbali kuanzia saa 2 o 3 asubuhi hadi saa 6 mchana hivi..ni vipindi fulani vya umbea umbea tu..na majungu
Yani inakera
 
Back
Top Bottom