nguruka wa kig0ma
JF-Expert Member
- Jan 16, 2020
- 2,946
- 2,929
Wanajamvi saalam!
Nimekuwa nikitafakari sana juu ya viongozi wa nchi hii hasa ccm ktk awamu hii. Siwaelewi kabisa, kwanini wanapoona dalili za kuondolewa madarakani wanachanganyikiwa kuliko hata vichaa wanaookota chakula majalalani.
Wanabadirika rangi kila muda. Mfano mbunge wa Mtama, nimemsikia bungeni akimfagilia Mkuu wa Malaika, kuwa aongezewe muda ili akamilishe kazi walizomtuma na kuwa kuwepo kwenye nafasi ile hakubahatisha bali CCM ilimchangua.
Amechambua maeneo kadha ikiwemo uchumi. Nape amesahau kuwa mwaka jana tu alishirikiana na baadhi ya makada wa CCM kutaka kumwangusha Mkuu wa Malaika. Leo anabadirika rangi kumfagilia njia mkuu wa malaika, mahali pasipo stahili.
Kwanini hakumfangilia njia kwenye vikao vya chama ambavyo vina mamlaka ya uteuzi. JE, HUKU SIYO KUCHANGANYIKIWA?
Nape alipotumbuliwa kwa sakata la Makonda, watu wengi walikuwa nyuma yake,walisamehe kosa lake la kufungia bunge live, WALIMUHURUMIA SANA.
Watu walijua kuwa Nape ni mtu mwenye kusimamia kauli zake, hata yalipovuja yale maongezi yao, watu wakaendelea kumwamini. Nimepata taabu sana baada ya kumsikiliza jana aliyokuwa anatapika bungeni.
Ndipo najiuliza: Hawa viongozi wa awamu hii wapo kwa ajili ya kuusimamia ukweli au kujipendekeza ili wapate uteuzi?
Nini kinawachanganya? Mbona hatukuona viroja kama hivi awamu zilizopita?
Anayejua jibu sahihi karibuni.
Sent using Jamii Forums mobile app