#COVID19 Hivi kwanini viongozi karibu wote wa Afrika kule UN walikuwa wanaomba chanjo za UVIKO? Mimi mtoto wa mchungaji sijaelewa

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
279
480
Kila Rais aliye simama pamoja na vitu vingine lakini kubwa ilikuwa kuomba vasinesheni ilikuwa kwa viongozi karibu wote kutoka Afriaka hivi hii imekaaje, Afrika kunani maana mpaka jana tarehe 29/09/2021 watu waliokufa na Korona duniani ni 4,790,321

Afrika jumla ya watu waliokufa na Korona mpaka leo 160,339
Afriaka inatakribani nchi 52
Ukichukuwa 4,790,321 - 160339 = 4,639,987 hawa wamekufa nje ya Afriaka.
Ukigawanya 160,339 kwa 52 = 3086 wastani wa kila nchi ya Afriaka waliokufa.
Dunia nzima ina nchi 198.
Ukitoa 198 - 52 = 146 nchi nje ya Afrika.

Ukigawanya 4,639,987 kwa 146 = 31,000 na ushee, ina maana nje ya Afria kila nchi imepoteza watu 31000 wakati sisi 3000
Marekani inakadiliwa wamekufa watu 700,000
Brazil inakadiriwa wamekufa watu 400,000
Itali au Uroma watu 300,000
Uingereza kama 84,000
Ujerumani kama 90,000
Iran kama 100000. nk

MALERIA Afrika inaua watu 3000 kila siku ikiwemo watoto wadogo.
Kwa wiki Afrika wanakadiliwa kufa watu 21000 kwa maleria
Kwa mwezi wanakufa waafrika 84,000
Kwa mwaka wanakufa waafriaka 1,008,000
Nje ya bara la Afriaka wanaokufa kwa maleria hawazidi 2500 kwa mwaka.
Na ulaya yote hakuna na hawaujui ugonjwa huu wa malaria.
Nisaidieni mimi mtoto wa mchungaji ambaye ni mwafriaka mwenzenu sielewi, sisi waafrika tulikosa nini kwa Mungu na ukizingatia dunia nzima sisi ndiyo tunaongoza kwa kusali na kuomba kuliko bara lingine lolote kupitia dini za kigeni.

Je, ni kweli sisi tatizo letu kubwa ni Korona?

Je, ni kweli hawa viongozi wetu wa Afrika wanajua kuwa tatizo letu ni korona? Kweli!

Ninabonyeza kinanda huku machozi yananitoka, Afrika, Afriaka tukimbilie wapi.

Nawasilisha na kila mwenye akili na atafakari,

Mtoto wa mchungaji.
 
Na huenda hakuna nchi ya Afrika inajaribu kutengeneza chanjo ya UVIKO. Ni kuomba tu. Yaani unakuwa mnyonge wa kudumu daima dumu!
 
Na huenda hakuna nchi ya Afrika inajaribu kutengeneza chanjo ya UVIKO. Ni kuomba tu. Yaani unakuwa mnyonge wa kudumu daima dumu!

Kwani ile chanjo alikuwa akiongelea Prof Mchembe kwenye hatua za mwisho iliishia wapi?
 
Back
Top Bottom