Hivi kwanini Vijiji vya Ujamaa havikufika Kilimanjaro na Bukoba?

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
Nimekuwa nikijiuliza hili swali muda mrefu bila kupata majibu,kwanin Vijiji vya Ujamaa havikuwahi kufika Kilimanjaro hususani Uchaggani na Bukoba?

Kama nakosea ruksa kunisahihisha,lakini sijawahi kusikia kama sehemu hizo zimewahi kuwa na vijiji vya ujamaa.

Je, Nyerere alikuwa anawapendelea ama alikuwa anawaogopa au kuwatenga watu wa sehemu hizo?

========

Natumaini muuliza swali aliposema Bukoba na hapo hapo akasema Kilimanjaro alikuwa anataka kusema Kagera badala ya Bukoba!

Na pia kwamba kwa kusema Bukoba labda aliataka kusema, kule kwa Wahaya peke yake(Wilaya za Bukoba mjini, Bukoba Vijijini na Muleba tu).

Sasa, ikiwa ni Kagera au kwa wahaya, jibu ni kwamba katika Mkoa wa Kagera kulianzishwa vijiji vya ujamaa sawa na sehemu zingine. Mfano ninaoufahamu kwa uhakiki ni Kijiji cha Ujamaa cha Rushwa.

Hiki kiko wilayani Muleba. Pia mfano mwingine ni katika wilaya ya Biharamulo. Vijiji vingi tu vya ujamaa. Kama walivyosema waliotangulia, watu waliokuwa wakikaa mbalimbali ndio waliokuwa wanatakiwa wakae pamoja ili imwe rahisi kuwahudumia.

Pengine wengi wenu hapa ni vijana ambao mlikuta ama kusikia tu habari ya vijiji vya Ujamaa, hivyo maswali haya yanatokana na kutofahamu umuhimu uliokuwepo ktk kuanzisha vijiji vya Ujamaa. Nadhani kwanza ni tuelewe kwa nini vilianzishwa, hizi habari za kushindwa hazina maana yoyote ikiwa lengo lilikuwa bora kwa mendeleo ya nchi yetu.

Waswahili wanasema unaweza kumpleke pumba mtoni kunywa maji lakini huwezi kulazimisha kuyanywa... Hapa wazo la kumpeleka Punda mtyoni ni zuri na kwa faida yake lakini akikataa kunywa maji haina maana yalikuwa ni mawazo mabaya ndio maana Punda amekataa kunywa maji.

Zipo sababu mbili muhimu sana ktk uanzishaji wa vijiji vya Ujamaa, Kwanza kabisa nataka muelewe ya kwamba baada ya Uhuru wetu asilimia 90 ya wananchi walikuwa wanaishi vijijini na asilimia 80 ya pato la Taifa lilitokana na kilimo, lakini asilimia kubwa ya matumizi ya maendeleo ya nchi yetu yalikuwa mijini na sii vijijini. Hivyo, kwa kuwa Tanzania ilikuwa nchi ya kilimo, na watu wengi wakiwa wanaishi katika vijiji vya asili, alibainisha kwamba ingekuwa njia nzuri ya kupeleka maendeleo vijijini kwa kupitia mfumo wa ujamaa (Lengo).

Pili, Kama alivyosema Mchambuzi, jamani siku zote vision ndio huzaa ideas na muhimu sana kutazama WATU na MAZINGIRA kabla hujaweka Azimio na kutunga strategies zinazohitajika kulingana na vigezo hivyo. Katika kutazama wingi wa vijiji hivyo ilikuwa sii rahisi kusambaza maendeleo kwa kila kijiji nchini ikiwa vijiji vingi vilikuwa vimesambaa hovyo nchi nzima. Hivyo, ikatazamwa mikoa ambayo vijiji vyake viko sehemu ambazo azma hii mpya itakuwa kazi kufikisha huduma ya maendeleo, vijiji hivyo vivunjwe na kujenga vijiji vipya karibu na maeneo ya uzalishaji na ama sehemu zilizokusudiwa kujengwa barabara kuwezesha ujenzi wa vijiji vipya ambavyo leo hii vingekuwa miji..

Kwa hiyo wakuu zangu lengo lilikuwa kupeleka maendeleo vijijini na huwezi kuanzisha vijiji tu bila mipango miji..Wenzetu Ulaya miji yao yote imepimwa, maeneo yote yamewekwa ktk hesabu za maendeleo ya nchi zao na hata sehemu zilizowazi tayari zimewekwa hivyo kwa makusudio ama kuna mipango itafuatwa miaka ijayo..Kwa hiyo mpango wa mwalimu kuanza kujenga vijiji vipya ambavcyo leo hii vingekuwa miji mipya yenye maendeleo tulishindwa kuafiki mpango ule kama Punda aliyepelekwa kunywa maji mtoni.

Hadi leo hii baada ya miaka 50 ya Uhuru, kuna vijiji ambavyo havina kabisa huduma za maji, maduka, shule zahanati, viwanda wala na wala magari hayawezi kufika. Naweza kusema Tanzania nzima leo hii haina ramani.. watu wanjijengea tu wanavyotaka, wanakotaka na kuvamia maeneo maadam yako wazi. Wengine hata hudai urithi wa ardhi ambayo haikuwahi kuwa yao wala ya wazee wao ili mradi awepo shahidi tu wakubainisha uongo huo..

Tunaijenga Tanzania siyokuwa na ramani, tazama hadi mijini nenda ukajionee Kariakoo maghogora yaliyojengwa hayana hata elevator, hakuna maji wala nafasi baina ya nyumba na nyumba..Kaitazame Sinza mji mpya ulivyokjjengwa inasikisha kwa sababu watanzania hatuna Utamaduni wa kujenga kwa ramani..

Sasa utakuta ya kwamba zipo sehemu nyingi sana Tanzania vijiji vya Ujamaa havikufika. Sio Kilimanjaro, Bukoba na Mbeya tu bali mikoa mingi sana ambayo vijiji vyake vilikuwa ktk maeneo mazuri na yenye kufikiwa kirahisi hawakuwa na vijiji vya Ujamaa. Tazama Mwanza, Musoma, Mbeya, Tanga na Tabora, mikoa ambayo ilikuwa ya uzalsihaji mkubwa wa kilimo nchini wakati wa mkoloni...vijiji vyao vimekuwepo ktk maeneo mazuri na wakazi waliishi ktk maeneo ambayo tayari huduma zilikuwa zinawafikia..Vijiji vingi ktk maeneo hayo vilijengwa na wakoloni kutokana na kwamba walikusanya mazao kutoka mikoa hiyo ya uzalishaji hivyo hapakuwa na sababu ya kuunda vijiji vipya wakati wananchi waliishi tayari ktk vijiji ambavyo huduma zilikuwa zinawafikia.

Katika mipango miji, serikali ni lazima ichore ramani ya miji yetu. Nasikia ukienda ofisi ya Ardhi utakuta ramani ya mji wa Dar kama ulivyokusudiwa na Mjarumani - Utalia kilio cha kughafirika kwa sababu mji huo unaonekana mzuri ulopangwa vizuri lakini leo hii Dar Es Salaam ni mji tofauti kabisa na ule ulokusudiwa, kisha tunalalamika usafiri mbaya, hakuna maji, umeme shida, mvua zikinyesha mji wote mafuriko na kadhalka.. Hii yote ni kwa sababu tumeujenga mji wetu pasipo kufuata ramani bali kipenda roho..Zile zile tabia tulokuwa nazo kabla ya Ujamaa na kujitegemea - Watu kuvamia maeneo, kujenga hovyo hatutaki kupangiwa sheria ya kuishi... Halafu tunajiuliza sheria iko wapi viongozi wanapokiuka sheria. Nani kweli anafuata sheria nchini kwetu? Utamaduni huo tumeupata wapi ikiwa sheria kwetu ni utumwa wa kutawaliwa...

Lakini ikitokea serikali kutaka kuwahamisha wanalalamika kuhamishwa maeneo yao kwa sababu inatakiwa kujengwa barabara, viiwanda, mji mpya na kwa kutumia dhana hiyo serikali imeweza kuwahamisha watu pasipo hiari yao na kuwapeleka ktk maeneo mapya. Majuzi tu Machinga huko Mbeya wamekiwasha hawa wana tofauti gani na wananchi waliokataa kuhamia vijiji vya Ujamaa!... Na kweli serikali imeshindwa kuwaondoa machinga mijini, wameshindwa kuondoa vibanda vilivyojengwa mbele ya nyumba kujenga maduka ambayo yamechukua hadi sehemu za barabara. Residential areas zimekuwa ndio sehemu za biashara, maduka, viwanda na kadhalika..

Je, kutokana na kiburi hiki cha Wadanganyika, kutokuwa na ustaarabu unaweza kuita ndio kushindwa kwa serikali iliyopo madarakani
!
 
Kwani ni characteristics gani zinazokifanya kijiji kiitwe "Kijiji cha Ujamaa"?

Ukijibu hilo inaweza kusaidia wengi kujuwa kama vilikuwepo ama lah.!
 
Maeneo yaliyolengwa sana sana ni yale yaliyokuwa sparsely populated; mikoa ya kilimanjaro, Bukoba ilikuwa densely populated; lengo la vijiji vya ujamaa ilikuwa kuwakusanya watu waliokuwa wanakaa mbali mbali na kwa uchache uchache waje kwenye eneo moja ili iwe rahisi kuwapelekea huduma za kijamii na pia iwe rahisi kuendeleza vijiji ili vije kuwa miji baadae iwapo mapinduzi ya kilimo yangefanikiwa na kupelekea uanzishwaji wa viwanda n.k;
 
Kijiji cha ujamaa Chekereni kiko wapi? Sijui kama watu walihamishwa kama sehemu nyingine ila najua kipo moshi vijijini, na kumbukumbu zinaonyesha ni kati ya vijiji vya ujamaa vya Nyerere.
 
kinepi_nepi

Ndio maana nikasema hususan Uchaggani mdau,soma sawasawa usikurupuke.Chekereni iko Uchagani?
 
Last edited by a moderator:
Eeeeh!mi nimeuliza na wewe unaniuliza mimi tena!!kweli sisi ni wabongo asilia....
Ndiyo maana ya mjadala usiwe mwepesi ku conclude na unajuwa hii ni JF.

Ni sawa tu na kwamba nilitaka uongezee nyama kidogo kwenye hoja yako.

Kwa mfano ni vitu gani haswa vinakifanya kijiji cha ujamaa kiitwe hivyo?

Kuna vijiji vingi tu Kilimanjaro vilikuwa vya kijamaa na hata vyenye hulka ya kijamaa,hata uko upareni nk.

Kuna vijiji vina mashamba yao yaliyokuwa yakiitwa "mashamba ya kijiji" na maduka ya vijiji nk,sasa hiyo haivifanyi viwe vijiji vya ujamaa?Ndo maana nikauliza.

Nia yangu ilikuwa kusaidia mjadala,lakini wewe ndo mbongo asilia,sijui nia yako ya kuanzisha mjadala ni nini haswa kama hutegemei mswali kwa wasomaji.

Ujifunze JF usiropoke tu.
 
Ndiyo maana ya mjadala usiwe mwepesi ku conclude na unajuwa hii ni JF.

...

Mimi nimeuliza kwa great thinkers swali ambalo nimekosa jibu lake miaka nenda rudi....jamaa aliefuatia chini yako huyo alievaa nguo za magamba amejibu vizuri sana na angalau amenipa picha;na kama ungesoma bila kukurupuka ungeelewa kwamba nilikua nauliza swali ambalo nilitegemea majibu sio maswali tena,na pia usingetaja habari ya upareni kwa kuwa nimetumia neno "hususan" uchaggani,hapa siwezi kukulaumu sana inawezekana neno hususan lilikua ni neno gumu kwako!!!ni la kiswahili lakini linatumiwa zaidi na waswahili wenyewe kwa maana ya watu wa pwani,maana yake ni "zaidi"!
 
Angalia sasa,futa basi heading na useme uchaggani badala ya Kilimanjaro,mimi nilidhani wewe ni mtu makini.

Eeeh kwa hiyo umakini wangu unautilia shaka kwa kuwa sijasema uchagani badala yake nimesema kilimanjaro kwenye heading!acha uvivu wa kusoma jenga tabia ya kusoma post yote sio kukurupuka na heading tu basi.
 
Eeeeh!mi nimeuliza na wewe unaniuliza mimi tena!!kweli sisi ni wabongo asilia....

Siyo kila wakati uulizwapo swali wakati unategemea jibu eti ni sababu ya Bongo, kuna nyakati humaanisha kuwa hujaeleweka.
Hivyo lisome tena swali lako utagundua linakosa some Ingedients.
 
Siyo kila wakati uulizwapo swali wakati unategemea jibu eti ni sababu ya Bongo, kuna nyakati humaanisha kuwa hujaeleweka.
Hivyo lisome tena swali lako utagundua linakosa some Ingedients.

Utakuwa huna majibu tu mzee!wala sio zambi kutokua na majibu,mbona bwana mwenye kivazi cha magamba pale juu ameelewa na amejibu?

Ina maana nyie ndio mnaakili sana kuliko yeye au?Mimi majibu yake nimeyaelewa na kuyakubali,nyie je au nae majibu yake hayaeleweki kama swali langu!
 
Unataka kutengeneza kitu ambacho hakijaharibika? Jamaa walikuwa wakiishi kwenye vijiji hivyo tayari. Ulitaka waende wapi?
 
Mwenye kuuliza swali ni kama vile alitegemea jibu fulani ambalo jmushi anaenda kinyume. Ila ukweli utabaki palepale.
 
Hapa pangekua bungeni na mm ningekua spika (bi kiroboto) ningekwambia mh hii sio hoja kaa chini. Na kwenda kwenye thread nyingine.
 
Vijiji vile havikuangalia kabila, vilitafuta eneo linalofaa kwa kuzalisha mali, kwa hio unaweza kufafanua zaidi defn ya uchagani au ukawa tayari kuwa unajibu maswali madogo madogo yanayojitokeza bila hasira.

Kwa taarifa tu jmushi nae ni kati ya magreat thinkers hata kama anakupa kamwiba
.
 
Haika

Huyu yeye kachagua angle ya ukabila!!kweli kazi ipo leo,mama au sijui baba limetumika neno uchaggani sio kuonesha ukabila bali ni katka kuleta tofauti kwa maana mkoa wa Kilimanjaro unakaliwa na makabila mawili,Wachagga na Wapare na kila moja lina maeneo yake.

Sikua na tatizo sana na upareni ambako najua vipo vijiji vya ujamaa,tatizo langu lilikua ni kilimnjaro sehemu ya uchaggani,na sio kilimnjaro tu niliyoigusa upo mkoa mwingine nimeutaja lakini kwa kuwa humu mko wengi naona wote mmenda kwenye angle hiyo hiyo tu na wengine kuanza kuleta hisia za ukabila.

Mimi pia naelewa hapa ni nyumbani kwa ma great thinker akiwemo huyo wako,lakini mpaka sasa aliejibu swali ni mmoja tu,bwana mvaa nguo za magamba!sasa sitaki kuamini kwamba yeye pekee ndio great thinker na pengine msinifanye niamini hivyo
.
 
Last edited by a moderator:
Maeneo yaliyolengwa sana sana ni yale yaliyokuwa sparsely populated; mikoa ya kilimanjaro, Bukoba ilikuwa densely populated; lengo la vijiji vya ujamaa ilikuwa kuwakusanya watu waliokuwa wanakaa mbali mbali na kwa uchache uchache waje kwenye eneo moja ili iwe rahisi kuwapelekea huduma za kijamii na pia iwe rahisi kuendeleza vijiji ili vije kuwa miji baadae iwapo mapinduzi ya kilimo yangefanikiwa na kupelekea uanzishwaji wa viwanda n.k;

Yalishindwa kufanikiwa eenhh? kumbe kuna idea za Nyerere zilishindwa. Hivi kuna ipi iliyoshinda kati ya idea za Nyerere?
 
Mbona hata enzi za Ujamaa kulikuwa na settlers sehemu kama Arumeru?
 
Yalishindwa kufanikiwa eenhh? kumbe kuna idea za Nyerere zilishindwa. Hivi kuna ipi iliyoshinda kati ya idea za Nyerere?

Labda "kujenga nchi" maana tuliimbishwa sana tanu(ccm)yajenga nchi enzi zile lakini mimi nilikua najiuliza hivi inatakiwa kujenga nchi au maisha yetu wananchi??
 
Back
Top Bottom