Kwa kuwa mshauri karibu watu wamekuwa wakiniuliza kuhusu upatu mpya wa D9 Club na jibu langu limekuwa moja tu hiyo ni Deci nyingine ila inashangaza kuwa hao walioamua au waliotayari nikiwaambia hivyo mara moja wanapanick na kutaka kusema wewe hujui na maneno mengi ya kashfa.
Wengine wamefikia kusema huoni wengine wanapata na jibu langu limebaki kuwa hakuna upatu unakuwa na mwisho mzuri full stop. Ila hii trend imenipa muda wa kujiuliza hivi kwanini kila baada ya muda kunazuka vitu kama hivi kulikuwa na kitu kinaitwa Dollar general miaka ya 1999 to 2000, na kikaja kile cha Arusha miaka ya 2003 hapo , ikaja baba yao Deci 2008 to 2009 ikala wakutosha, ikatokea TELEFREE 2013 hii niliipiga vita nikatishiwa na maisha na watu niliowaona walikuwa wanainfluence za sasa 2017 D9 nayo imeshika kasi ubaya sana umekamata wasomi ambao watu wanawaamini sana ila hata kwa kufanya layman googling utaona shida tayari iko kwenye huu mfumo. (Soma hii link D9 CLUB IS A FRAUD – ALERT! - Online Business Training)
Sasa swali ambalo nimewauliza waliokuwa wanakuja kuniomba ushauri D9 inafanya biashara gani? Sport betting, hivi wewe unaweza kwenda kuweka fedha yako kwenye vibanda vya sport bet ukitegemea kuwa tajiri? Ambazo zipo hapa mtaani kwetu jibu lao wengi ni hapana sasa kwanini unaamini kwenye ambayo ina mtandao na lazima uingize mtu au ununue miguu mwenyewe?
Tatizo la upatu ni hili hapa siku biashara inaacha kuingiza watu wapya inakufa na inapokufa ni sehemu ambayo wewe umeshawashawishi ndugu zako hata 20 tuu wajiunge. Mfano saa hizi package iliyo maarufu ni ya $1,996 sawa na milioni 4 ya kitanzania ikiwa na promise ya kupewa $ 171 kila wiki ambayo kwa haraka haraka itakuchukua miezi mitatu ili urudishe hiyo hela ila katika kipindi hicho utakuwa umeingiza watu wengie sema mfano hao 20 watakuwa wameweka milioni 80 na hawa 20 wakitafuta wao 20 kwenye benki ya wenye upatu atakuwa na bilioni 1.6 sasa fikiri hao mianne wakitafuta 20 tena kwahiyo wewe wa kwanza unaufaika mpaka mwisho wa watu 400 kwa hata kudouble hela yako lakini umeshaingiza watu billion 1.6 ambayo wewe umepewa millioni nne.
Hapa ndio maana hakuna serikali duniani inakubali biashara ya upatu au PONZI SCHEME ni hatari kwa taifa, hakunaga hela ambayo unaweza kupata kwa kudhulumu ikakuacha ulale vizuri. Somo tutafute njia halali za kutengeneza fedha bila kuumiza wegine.
Usiku mwema ni kwa amani epuka maneno makali tafakari kwa kina at what expenses you want to acquire wealth,