Hivi kwanini uolewe au kuoa mtu ambaye unajua hata kwenye ndoa atakunyanyasa?

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Wanasema tabia ni uhalisia wa maisha ya mtu iwe mbaya au nzuri ndio uhalisia wake. Kama ulikuwa na mchumba mlevi na ukakubali kuolewa nae ukifikiri ukishaolewa utamfanya aache ulevi umekosea.

Kama ulikuwa na mchumba wa matusi na ukaamini ukimuoa au kuolewa naye ataacha umekosea. Kama ulikuwa na mchumba malaya au kicheche ukakubali kuoa au kuolewa kwa fikra akiingia kwenye ndoa ataacha umekosea.

Hivi ni baadhi tu najua viko vingi ila jua tu mateso unayopitia sasa na mchumba wako basi usifikiri ukiolewa nae au kumuoa ataacha achilia mbali kupunguza.

Ni rahisi kuvunja uchumba, usijitese kwenye ndoa bana kama haeleweki na umedhamiria kuolewa naye au kumuoa epusha shari kabla ya shari kamili.
 
Watu wanabadilika, ata ao unaowaona watulivu, watakatifu wanaeza badilika pia......

Uezi Amini shetani nae alikua ni malaika wa Mungu!
 
kisa tu ndugu jamaa na marafiki nao wacheze kwaito akhuu kwa kweli furaha yako nayo ni muhimu mwanamke usiolewe tu kisa binadam wasikuite majina mabaya
 
eden don't break people's heart for what might have happened on you. Things always change na tabia hubadirika either kwa kufuata ushauri wa mtu wako wa karibu, kuona mtu amepata madhara kwa tabia kama uliyonayo wewe au baada ya kupata tatizo lihusianalo na tabia husika.

Alafu kingine jua kuwa love is an intensive feeling over somebody that through a such unconditional feeling waweza usisikilize wala kujali lolote linalomhusu mchumba wako zaidi ya kutaka kureach the final life commitment which is marriage.

Don't be biased
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom