eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,227
- 16,178
Wanasema tabia ni uhalisia wa maisha ya mtu iwe mbaya au nzuri ndio uhalisia wake. Kama ulikuwa na mchumba mlevi na ukakubali kuolewa nae ukifikiri ukishaolewa utamfanya aache ulevi umekosea.
Kama ulikuwa na mchumba wa matusi na ukaamini ukimuoa au kuolewa naye ataacha umekosea. Kama ulikuwa na mchumba malaya au kicheche ukakubali kuoa au kuolewa kwa fikra akiingia kwenye ndoa ataacha umekosea.
Hivi ni baadhi tu najua viko vingi ila jua tu mateso unayopitia sasa na mchumba wako basi usifikiri ukiolewa nae au kumuoa ataacha achilia mbali kupunguza.
Ni rahisi kuvunja uchumba, usijitese kwenye ndoa bana kama haeleweki na umedhamiria kuolewa naye au kumuoa epusha shari kabla ya shari kamili.