hivi kwanini umaaarufu huja/huongezeka baada ya kifo?

Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
10,413
6,570
mara nyingi sana nikisikia mtu fulan amefariki basi ntasikia sifa lukuki kwa marehemu tena unakuta sifa nyingine hata hazimuhusu marehemu hivi hii husababishwa na nini?
 
Baada ya kufa huwezi fanya kosa tena, Hivyo kila mtu anapata uhakika kwasababu huwezi geuza hiyo misifa unayopewa
 
Kwa kawaida sisi binadamu hujawa na roho za huzuni na kumbukumbu ya mazuri ya marehemu wala siyo mabaya , mabaya ya marehemu siyo huwezi kuyafikiri lasivyo utakuwa kichaa
 
Tunawasifia marehemu hata kama hawakustahili sifa kwasababu sisi wenyewe ni WATUPU...hatuna la kujisifia, hatujiamini na tunaogopa tukifa hatutakumbukwa kwa lolote. Kuwasifia marehemu kwetu ni kuweka akiba ili nasi tukifa waliobaki watusifie hata kama katika uhai wetu hatukuwahi kufanye jambo lolote la kuisaidia jamii.
 
Back
Top Bottom