Hivi kwanini tigo wanakuwa wasumbufu kuirudisha pesa iliyokosewa?

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
19,250
2,000
Wakuu hawa watu ni janga mno unaweza kutuma pesa kwa bahati mbaya ukawa umeikosea na ukawahi kuwapigia simu kisha wanakujibu tumeuzuia sasa usubir masaa 24 unaweza kusubir hayo masaa 24 na bado pesa isirudi hawa watu ni kichefuchefu.

Pia kuna suala najiuliza kwa mfano ulikuwa na shida ya muhimu kweli ambayo utatuzi wake hauhitaji yazidi masaa 24 je hapo sio kupotezeana muda kweli? Kwa nini hawajifunzi pesa ya mtu kuirudisha muda muafaka kuliko kumsubulisha mtu masaa 24 na jambo lako la muhimu likakwama?

Hii system ya hovyo sana ni muda muafaka kuiangalia upya ni upotezaji wa muda tu hamna namna na wizi.
 
Madihani

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
5,054
2,000
Mbona kabla ya kuhakikisha wanakuambia hakiki jina ndio uweke namba ya siri.
Kama ulikuwa unamtumia Anna Abdallah ukiona limetokea jina tofauti unaacha kuthibitisha muamala
 
radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
19,250
2,000
Mbona kabla ya kuhakikisha wanakuambia hakiki jina ndio uweke namba ya siri.
Kama ulikuwa unamtumia Anna Abdallah ukiona limetokea jina tofauti unaacha kuthibitisha muamala

Ndo mana kuna neno kosea au bahat mbaya halikubuniwa kimakosa.
 
radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
19,250
2,000
Mbona kabla ya kuhakikisha wanakuambia hakiki jina ndio uweke namba ya siri.
Kama ulikuwa unamtumia Anna Abdallah ukiona limetokea jina tofauti unaacha kuthibitisha muamala

Badala ya kusaidia namna ya kupunguza masaa 24 unawaza wakina anna abdala
 
Kiwembe 0

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
535
1,000
Huu ni uvivu wa kusoma
kabla ya kumtumia mtu pesa hakiki # kisha jina

Watanzania ni wavivu kusoma/kuhakiki muamala

Kukosea muamala ni uzembe
 
radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
19,250
2,000
Huu ni uvivu wa kusoma
kabla ya kumtumia mtu pesa hakiki # kisha jina

Watanzania ni wavivu kusoma/kuhakiki muamala

Kukosea muamala ni uzembe

ujuaji mwingi sisi wa tz kama hujui kitu omba ufanunuliwe umetuma pesa kwenye kampuni x kule mtandao upo down unawapigia tigo wanakuambia subir msaa 24 nayo yanapita hapo ni uvivu?
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
41,449
2,000
Mbona kabla ya kuhakikisha wanakuambia hakiki jina ndio uweke namba ya siri.
Kama ulikuwa unamtumia Anna Abdallah ukiona limetokea jina tofauti unaacha kuthibitisha muamala
Ukihama mtandao haitoi jina mpaka hela ikishaenda, mfano Tigo kwenda Voda jina linakuja baadae hela ikishafika.
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
41,449
2,000
Wakuu hawa watu ni janga mno unaweza kutuma pesa kwa bahati mbaya ukawa umeikosea na ukawahi kuwapigia simu kisha wanakujibu tumeuzuia sasa usubir masaa 24 unaweza kusubir hayo masaa 24 na bado pesa isirudi hawa watu ni kichefuchefu.

Pia kuna suala najiuliza kwa mfano ulikuwa na shida ya muhimu kweli ambayo utatuzi wake hauhitaji yazidi masaa 24 je hapo sio kupotezeana muda kweli? Kwa nini hawajifunzi pesa ya mtu kuirudisha muda muafaka kuliko kumsubulisha mtu masaa 24 na jambo lako la muhimu likakwama?

Hii system ya hovyo sana ni muda muafaka kuiangalia upya ni upotezaji wa muda tu hamna namna na wizi.
Hujasikia kuna mtu anauziwa kitu analipa kwa Tigo/m pesa baadae anapiga simu kwenye mtandao kuwa kakosea kutuma? Anafanya hivi kumuibia aliemuuzia kitu. Siku hizi mitandao huwa wanajirudhisha kabla ya kurudisha, wanasemaga 24hrs ila sonetimes hata nusu saa haifiki.
 
upalala

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
318
250
Kiukweli Hawa TIGO wanaboa sana mm Leo hii ni wiki karibu hela yangu haijarudishwa nikiwauliza wanasema wanashughulikia
 
radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
19,250
2,000
Hujasikia kuna mtu anauziwa kitu analipa kwa Tigo/m pesa baadae anapiga simu kwenye mtandao kuwa kakosea kutuma? Anafanya hivi kumuibia aliemuuzia kitu. Siku hizi mitandao huwa wanajirudhisha kabla ya kurudisha, wanasemaga 24hrs ila sonetimes hata nusu saa haifiki.

Nayo ni point mkuu rrondo.
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,314
2,000
Tigo wako sahihi

Kuna Mchezo umeibuka, kwa mfano unaenda kununua kitu then unamsema utalipa kwa Tigopesa na kweli unafanya hivyo
Baada ya Muda unapiga simu Tigo then unawaambia unekosea nao wanakurudishia fasta, baada ya Muda Yule Muuzaji anashangaa salio lake limekuwa reversed akipiga simu Tigo anaambiwa liliingia kimakosa Kumbe si kweli

Wanachelewesha ili kujiridhisha kwa taarifa ulizotoa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom