Hivi kwanini Tanga hainyang'anywi hadhi ya kuwa Jiji? Ni sehemu ya ajabu sana

Huwa nacheka sana kiswahili chao, magari yakiwa mengi wanaita mijigari, taa nyingi wanaita mijitaa!
Niko kiwandani kuna issue nafanya kwa Muda wamiezi 3 mpka January 31, Sasa wamama wahuku utasikia mkwee, uncle, wamama wanauliza eti uncle umeoa?. Kama hujaoa mwanangu huyu nikupe naishia kucheka.

Wakiona mtu mwenye ahueni ya maisha kidogo, wanataka wakutongozee mpaka watoto wao, sema nasikia niwashirikina sana..
 
Niko kiwandani kuna issue nafanya kwa Muda wamiezi 3 mpka January 31, Sasa wamama wahuku utasikia mkwee, uncle, wamama wanauliza eti uncle umeoa?. Kama hujaoa mwanangu huyu nikupe naishia kucheka.

Wakiona mtu mwenye ahueni ya maisha kidogo, wanataka wakutongozee mpaka watoto wao, sema nasikia niwashirikina sana..
Huko ni balaa, watu wengi huko hasa watoto lazima wavae hirizi.
 
Mahali napenda nikiwa hapo Tanga ni hapo mkwakwani kwenye pezwa mida ya jioni.
Niko kiwandani kuna issue nafanya kwa Muda wamiezi 3 mpka January 31, Sasa wamama wahuku utasikia mkwee, uncle, wamama wanauliza eti uncle umeoa?. Kama hujaoa mwanangu huyu nikupe naishia kucheka.

Wakiona mtu mwenye ahueni ya maisha kidogo, wanataka wakutongozee mpaka watoto wao, sema nasikia niwashirikina sana..
 
Tanga huwezi fanya kitu bila kushirikisha ushirikina, sawa tu na wana Mbeya. Kule Mbeya kila baada ya nyumba moja kuna kanisa la kisanii na bado wanaongoza kwa uchawi hapa Tanzania
Nini maana ya kanisa la kisanii. Ebu naomba unieleweshe
 
Kweli mkuu, kuna Ushongo Beach Club, Emayani, Mike Hotel ule ukanda wote wa Ushongo kuna fukwe na hotel nzuri kama upo Ibiza au Coppa Cabbana.
Yaani wakati naenda tu club beach resort mwenyeji akaniambia kabla ya kufika utazipita hotel kama mbili hv, dah sikuamini ila ni kweli unakuta hotel ina mbuga za wanyama automatically, sio kama wale wa maonyesho, yaani wenyewe wanaishi tu humo na huruhusiwi kuwapiga maana ndo kivutio cha watalii
Mi nikajisemea, "Ndo maana wazungu ni wengi sana Pangani".
Pia room zao sasa, ndo utajua kweli hii ni hotel ya kitalii,
Yaani ukitaka Room kama Kilimanjaro Hotel utapata, ila wazungu wanataka room za asili, sasa wamejenga kama mahema flani hv mazuri sana ukiingia ndani unakuta kupo full kuna kila kitu na vingi ni vya asili
Ukiwa unajua kuongea english sasa ndo utafurahi, kazi yako ni kuongozana na wazungu tu, kuna jamaa yangu wazungu wakataka waongozane nae zenji huko, jamaa akachangamkia fursa, baada ya kuwarudisha hotelini akapewa dollar kadhaa na kazi akaacha akaenda kusomea udaktari,
Sa hv yupo mkuranga hapo ni dokta

Kifupi kule ukiwa mwongeaji mzuri wa English we tafuta mtu akuunganishe kwenye hotel za kitalii, ila kama umeshazoea amsha amsha za Dar Tanga achana napo

Ila kiukweli nadiliki kusema Tanga ni moja kati ya majiji makubwa Afrika Mashariki, ukitaka kuijua jinsi Tanga ilivyojengeka wee tafuta mwenyeji mwambie akupeleke maeneo ya kishua

Ila UWE NA HELA LAKINI

Tatizo wenyeji wamepooza sana hawajachangamka yaani wamekaa kizembe sana lakini akienda mtu mwenye kutaka kufanya kazi za Hotelini au Bandarini, aisee atatoboa tu muhimu ajue kuongea kiingereza maana ndo kigezo kikubwa haswa kwenye Hotel za kitalii maana wageni wao ni wazungu tu, na kwenye Hotel za kitalii kuna uhaba wa wafanyakazi haswa wanaotakiwa kuwa wenyeji wa wageni (sijui wenyewe mnawaitaje)
Yaani wale watu ambao kazi yao ni kutembeza watalii
 
Tuangalie viwango vya Dunia vya Jiji kisha tufananishe na Tanga. Tutumie definition ya Wikipedia
View attachment 1626225
Hapo wikipedia wametaja sifa ya jiji kwamba ina extensive system ya
1. Housing
2.transportation
3. Sanitation
4. Utilities
5. Land use
6. Communication

Pia wameongelea uchumi usiohusisha kilimo na watu wengi kukaa kwenye eneo dogo la ardhi.

1. Tuanze na Housing, Tanga kuna makazi ambayo yamepangiliwa, nyumba nyingi mjini zina namba na hazijajengwa ovyo ovyo, zimepangiliwa kwenye mitaa na hata ukiangalia ramani ya Tanga mwenyewe unaelewa hili ni jiji limepangika, makampuni yana nyumba za wafanyakazi, mashule yana nyumba za walimu etc.

2. Transportation
Usafiri pia Tanga si shida kuna usafiri wa maji, barabara, wa ndege na hata reli, tuna connect na mombasa, pemba na zanzibar, wilaya na mikoa tofauti, na barabara za lami ukitoa ya pangani.

3. Sanitation
Mkuu tanga mjini pale jiji zima lipo connected na underground waste system, ukijenga nyumba una connect tu mifereji hio ya maji machafu huna haja ya kuchimba choo, na ni mifereji mikubwa ambayo mtu anaweza dumbukia, i doubt kama kuna mkoa Tanzania wenye system kama Hii,

Pia maji masafi Tanga ni nadra kukatika mjini, na ni masafi kweli unaweza kunywa bila kuchemsha.

Hospitali zipo, na Tanga ni moja kati ya majiji safi Tanzania.

4.communication, Tanga kuna mitandao yote tena 4g, tuna Broadband na Wifi zamani sana, Nipo mdogo city centre yote ipo covered na Wifi, una uwezo ukawa na Tablet ya wifi isiyoingia line na ukawa always connected.

5.land use
Hii inahusiana sana na maneno kutengwa kwa purpose fulani, ukienda Gofu, katikati ya kange na pongwe ama barabara ya pangani utakuta maeneo maalum ya Viwanda, hayaingiliani na makazi, ukienda maeneo ya forodhani utakuta la Casa, chichi, nyumbani hotel etc huko ni night club na starehe nyengine, ukienda barabara za namba ni makazi ya watu etc. Hii inaitofautisha Tanga na majiji mengine ambayo haijulikani wapi bar wapi makazi wapi shule etc.

6. Utilities
Huduma mbalimbali za uma kama maji, umeme, afya, shule, etc vyote vinapatikana kwa wingi na ufanisi Tanga.
Shukran kwa maelezo yenye hoja. Umenijibu si Mimi tu, bali hata muanzisha uzi!
 
Huwa nacheka sana kiswahili chao, magari yakiwa mengi wanaita mijigari, taa nyingi wanaita mijitaa!
Hii sio kweli, Labda uliwasikia vijana au hata watu warika lolote wakiongea kimasihara. Ni tamathali za semi tu. Lakini huwa wanatamka vizuri kabisa magari.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Nini maana ya kanisa la kisanii. Ebu naomba unieleweshe
Mtu anaifanya nyumba yake iliyo sheheni misukule kuwa nyumba ya ibada na kujaza watu lakini usiku anaruka kwenda kufinya watu mikoa mingine ama jirani zake hapo mtaani. Kuishi Mbeya kunatakiwa moyo sana.
 
Labda amemaanisha huu upande wa kutokea stendi kubwa ya zamani kupandisha barabara ya kwenda "Kwetu pazuri" ila nimepasahau jina kidogo nafikiri panaitwa Chuda wanakaa waarabu na kuna lodge nyingi nzuri nzuri
Uzunguni ndio wapi? Watu wenye Hela Tanga wanaishi
1. Raskazone
2. Sahare ya upande wa baharini
3. Mwambani

Raskazoni kuna nyumba kibao kodi ni zaidi dola 1000, sidhani kama kuna nyumba ya 180k kule hiyo ulioitaja.
 
Back
Top Bottom