careenjibebe
JF-Expert Member
- May 28, 2020
- 1,604
- 1,646
Acha mambo ya ki_se_geju wewe karibu tanga! Ushamba na wivu achana navyo unapofika tanga..nyumbu_si weyeHivi kwa nini Tanga ni Jiji, maana naona pilikapilika kama za majiji mengine hazipo kabisa, ni Mji ambao umepoa mithiri ya Tabora, baiskeli huku ndio nyingi kuliko magari.
Vijiwe vya vijana vipo kila mahala, huku maisha ni mepesi sana, yaani ukiwa na 500 unakula ugali na mboga za majani.
Ukienda kula wali samaki unapewa kibua mzima na wali eti elfu 2. Nyumba za majani zipo mpaka katikati ya mji, nyumba zenye vibaraza vikubwa zile za kizamani ndio zimejaa.
Nyumba za matofali ya tope zipo kila mahala. Nyumba za miti pia bado zipo.
Wale wanawake wazuri wa Kitanga wala huku siwaoni kabisa, hivi hii ndio Tanga niliyokuwa naisikia nikiwa Dar es Salaam. Au kuna Tanga nyingine wakuu? Tofauti na hii ya Forodhani, Chumbageni, 16, Donge, Majani Mapana, Gofu Chini n.k.
Sehemu za kula bata Tanga hazipo kabisa. Wanawake wa huku wanapenda wageni sana kuliko wenyeji sijui kwa nini?
Kiukweli Tanga ni sawa na Tabora tu, Wala Tanga haina hadhi ya kuwa Jiji.