Hivi kwanini sisi Watanzania tunapenda kutembea taratibu kama konokono?

"Muda unakwenda muda unarudi"... sijaelewa hapo
Kumbuka pia, hali ya hewa uchangia. Ulaya ni baridi ukitembea taratibu ndo mwili unazidi pata baridi zaidi. Niliishi kidogo Ulaya nilifanya utafiti juu ya hili ulisemalo. Hivyo hii imewajenga muda wote kuwa katika mwendo wa haraka. Na pia wenzetu mambo mengi uwachanganya. Wazungu ni tofauti na waafrica sisi tunauwezo wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Lakini wenzetu daah! Anaweza jichanganya. Hivyo ujaribu kufanya kitu kimoja kwa haraka ili apate muda wa kufanya jingine. Na vilevile wametawaliwa na muda. hii uwasumbua sana, kulingana na majira na msimu katika maisha yao. Sasa wewe fikiria mara saa ziende mbele mara zirudi nyuma. Africa hiyo hatuna. Najivunia maisha yetu ya Africa yasiyo na pressure! Ndo maana wa Ulaya wamejaa msongo wa mawazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?
Hii ni tabia ya watu wasio na lakufanya.
 
Nilisha experience hiki kitu,siku ambayo sina mishe yoyote town huwa najivuta sana huku naangalia angalia bidhaa na watu,ila nikiwa na mishe ni vurugu mechi naona kama sifiki jinsi foleni isivyosogea.KWA HIYO MIMI KWA MAWAZO YANGU UKIMUONA MTU ANATEMBEA KWA KUJIVUTA VUTA JUA HANA SHUGHULI YA KUFANYA KAENDA KUPOTEZA MUDA TOWN na kinyume chake ni sahihi!!!
Kwanini Mtu Apoteze MUDA?

Bado ni ujinga tunao Wabongo.

Yaani mtu anaenda mjini kupoteza muda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii tabia inaboa sana. Kuna wakati unakuwa Kariakoo unaharaka zako ile mbele yako kuna mtu anatembea utadhani ana mabusha 4. Kwa mazingira ya Kariakoo huwezi kumwovateki kirahisi, basi newewe unaanza kuchechemea.
 
Ni kwa sababu tabia zetu na kazi zetu hazijali muda sana…. pia kufanya mambo bila mpango au kuwa na shughuli zenye kujali muda. mambo mengi ni "olela olela".
 
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?

Umesema kweli,ukitaka kuona pita barabara za chuo kikuu cha Dar es salaam hasa wakati wanafunzi wanavuka zebra cross , ndio tunatakiwa kusimama na tunafanya hivyo, lakini wanafunzi wanatembea kama wanaenda disco. Na sio objectively at all.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom